Monday, October 22, 2012

Utamu wa biringanya maganda yake...

 Shoga unaambiwa siku hizi wanaume zetu hawa nguvu za kiume hawana, wanawake wengi wamekuwa wakilalamika kwamba wame zao kila muda unapoendelea wanakosa nguvu za kuhimili mzunguko, kama mwanzo alikuwa anakupa mara tatu usiku mzima sasa anatoa mara mbili ama hata mara moja.

Sasa basi tukaambiwa biringanya ni dawa kubwa sana katika kusaidia wanaume kuongeza nguvu zao utaitumiaje sasa, nunua biringanya lako ukiwa na asali na mdalasini wako kwako yani hivi vitu visikae kukosa ndani kwako ukiwa kama mama mwenye nyumba.

Nitakufundisha njia mbili za kutumia biringanya hizi, kwanza chukuwa biringanya zako zionshe vizuri usimenye maganda katakata kwa style unayopenda wewe chukuwa sufuria yako bandika jikoni tia biringanya zako uzigeuze geuze kwenye sufuria yako yenye mafuta zisiunguwe kidogo tu ukiona zimelainika zitoe tenga pembeni, pika chakula chako na unashauriwa kama umepika ugali wako kaanga na kuku wako pale pembeni unamchuzi wako wa kuchomvea na huku unakisosi cha biringanya muruwa ugali ushuke salama  hivi ni kwa wale wanaoshindwa kula biringanya kama lenyewe bila kushushia kitu.

Njia ya pili osha biringanya zako ziache pembeni zikauke maji zikiwa tayari tia kwenye blenda saga zisage mpaka ziwe unga kabisa chukuwa kidogo kwenye kikombe changanya na mdalasini na asali mpe mpenzio anywe na wewe chukuwa kikombe chengine piga cheers kunyweni baada ya dakikaa kadhaa majibu yake mtayamalizia chumbani na utauona utofauti.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment