Wednesday, August 1, 2012

Sikujuwa Kamaa.........

Habari Rose, mimi ni msaichana wa miaka 24 wazazi wangu wamefariki nimebaki na kaka zangu wa nne na dada yangu mmoja, kaka zangu wote wameoa na dada yangu ndio yupo nyumbani naishi naye, mwaka 2010 nilipata mwanaume ambaye sikuwa naye kwenye uhusiano muda mrefu baadaye akasema anataka kunioa maandalizi ya mahari na utambulisho yakafanyika akaja kwetu akatoa mahari na kunivalisha pete ya uchumba.

Mwaka uapita bado tupo kwenye uhusiano mchumba wangu yule wala dalili za kuoa sikuziona bado tu nikawa natembea na pete ya uchumba, niliumia sana maana mtaani walishaanza kuongea na kunicheka kama unavyoelewa majungu yanavyokuwa.

Nikawa najisikia vibaya na kukosa amani nikaamua kwenda kuamia kwa mchumba wangu huyo, dada nimekaa huu mwaka wa pili sasa wala sioni dalili ya kuolewa zaidi kuupata ujauzito huu wa miezi mitatu nilionao sasa na nimeupata kwa mbinde maana bwana hatabiriki siku za kulala nyumbani, niliyoyakuta huko ni makubwa, mwanaume yule nikagundua kwamba kutokana na maneno ya jamaa zake wanaomfahamu kwamba ameshawavalisha wanawake nyumba pete za uchumba wengi na wala hawaoi, na sio hilo tu kwamba anamwanamke wake mama mtu mzima ambaye amekuwa naye miaka nenda miaka rudi yani kama amelogwa hawezi kumuacha kabisa, mpaka nikaelekezwa huyo mama anapokaa huko mabibo.

 mchumba wangu inaweza ikapita hata wiki harudi nyumbani yeye ananipigia simu tu, roho inaniuma lakini nitafanyaje inabidi nivumilie tu, mara haachi hela na akikuachia hela kidogo mpaka kukuona tena majaaliwa ninacho mshukuru MUNGU ni kwamba ninaujuzi mkubwa wa kusuka kwahiyo napata hela nyingi za kutumia nikisuka watu.

Kuna siku mwezi ulioisha simu yangu ikaita kupokea ikawa sauti ya mwanamke akiniambia anataka kuonana na mimi anamaagizo yangu kwamba tukutane mwananyamala kwa kopa maana itakuwa kwangu karibu kwasababu nakaa kinondoni, nikakubaliana naye na nikafika mpaka hiyo sehemu, kweli nilikutana na huyo mama ni mtu mzima ambaye bada ya kuongea naye niligundua mtoto wake wa kwanza amelingana na kaka yangu wa tatu.

Akaniambia kwamba yeye ni mwanamke wa mchumba wangu (nilivyosikia hivyo nilihisi kama nimekatwa na kisu tumboni, kwamba yule mwanamke niliyemsikia ndio huyu) na ananiambia yupo naye kwa muda mrefu sana kabla hata hajanivalisha mimi pete ya uchumba, na mpaka anafanya hivyo alikuwa anajuwa na akamruhusu maana naye anamume ndani hakutaka kumnyima kijana wa watu kuwa na mke ndani.

Lakini cha muhimu nilichokuitia hapa ni kwamba nataka ufahamu sababu ambayo siwezi kuachana na mchumba wako huyo ni kwamba yeye ni muathirika (niliona huyu mama anawivu tu na mimi ndio maana ananiambi hayo wala sikuyaamini) na aliniambukiza mimi na ndio maana nimeona ni heri nife naye mume wangu niliacha kukutana naye kimwili kipindi nilivyompata mchumba wako maana kipindi hiko alikuwa ananiridhisha zaidi ya mume wangu na kwakuwa mume wangu alikuwa ni mlevi na nguvu hana basi nikajikita kwake mzimamzima.

Kwahiyo uondoke, na ukae ukijuwa hayo na anapokuwa harudi nyumbani wala usijisumbue juwa tu yupo kwangu na kama huamini na simu yangu namba hii hapa chukuwa akiwa hayupo kwako nitakupigia simu usiku wa saa saba na nitfanya juu chini mpaka uongee naye upate uhakika ya haya ninayokuambia, kwahiyo wewe kaa kwa amani tu ujitunze, sikuwa hata na jibu lakumwambia alipomaliza kuongea nikainuka na kuondoka.

Nilipofika nyumbani kama kawaida sikumkuta mchumba wangu jioni ikafika kwa bahati akaja nyumbani, wala sikumlazia kiporo nikampa makavu kama niliyopewa bila akiwa hana hata presha akanijibu hamna kitu kama hiko, nikamwambia basi tukapime akakataa akaniambia unaamka tu nakufikiria kupima kwanini hukufikiria hayo tokea tulivyokutana akafungua pochi yake akatoa hela akaziweka hapo mezani akaondoka zake.

MUNGU tu siku hiyo kweli hakurudi nyumbani baada ya kuondoka usiku wa saa saba yule mama akanipigia simu akaniambia kama uamini ndani ya dakika mbili nitampa mwanaume wako simu nijifanye amsalimie ndugu yangu ataongea na wewe, kweli nikasikia kwenye simu anaitwa jina lake Patrick hebu msalimie huyu ndugu yangu yupo Dodoma, nikataka kuzimia niliposikia sauti ya mchumba wangu ikijibu hallo shemeji kwenye simu!!!! niliikata simu na nikaanza kulia kwa uchungu nikifikiria kitu kimoja tu je nimeathirika??????? na kama ni hivyo nitafanyaje na huyu mtoto????

Ilinibidi nirudi nyumbani nikamuhadithia dada yangu hayo yote tokea siku ya kwanza maana hakuna ndugu hata mmoja aliyejuwa matatizo yangu na mchumba wangu, dada akanishauri nikapime lakini siwezi ninaogopa sana akaamua kuitisha kikao na kaka zangu wengine, kaka zangu walichoamua nikwamba nirudi nyumbani, na nikapime na hawataki kumuona huyo kaka tena, sasa ninachofikiria kazi ya maana ya kutunza mtoto sina, shule niliacha nikiwa form one sikutaka kuendelea, wazazi hawapo nimechanganyikiwa ndugu zangu wananiambia kila mtu anamajukumu na familia zao msaada ndio utapata lakini msaada mkubwa ni lazima uwe juu yako mwenyewe!!!!

Nitafanyaje mwenzenu, roho inaniuma laiti ningejuwa....

Na ninataka kuwashauri wote humu siyo kila unayemuona mwenye afya njema ni mzima, ukimpenda mtu mkapime kwanza, mchumba wangu na huyo mama mkiambiwa wameathirika huwezi amini walivyonenena na wanavyong'aa sikuwaza mara mbili niliona mwanaume si ndio huyu nimepata sikujuwa kama nimepatikana.

Email yangu kapuni please dada.Reactions:

7 comments:

 1. mmmh mpaka mwili umenisisimka hapa kwa kisa hiki. Pole kwa yaliyokukuta dada mpendwa,nakushauri ukapime ujue afya yako ili ujipange upya sasa hata kama umeathirika ama la! kumbuka sasa una kiumbe tumbon mwako kinachokutegemea wewe kwa asilimia mia moja kwahyo anza upya,kaa jipange ufanye nini na uishi vp kutengeneza maisha yako na mtoto na si kukata tamaa. Kuathirika sio mwisho wa maisha na kizuri una kipaji cha kusuka kinachoweza kukupa kipato hivyo dunduliza hela zako mpk zikufikishe ambapo unaona unaweza kufaanya kitu kingine zaidi ya kusuka kwa kupata hela. Mtumaini Mungu peke yake,mwambie shida zako,jitume nawe utafanikiwa! kila la kheri.

  ReplyDelete
 2. pole sana dada na majaribu haya hii ndiyo majaribu piga magoti na kumwomba Mungu akupe wepesi ktk majaribu haya maana ni mazito lakini kwake hakuna lisilo wezekana kwanza hukueleza kama umefikia muwafaka wa kupima au lah mimi ushauri wangu kwako ni kwamba jipe moyo nenda ukapime uwe na amani kwani inawezekana hukupata maambukizi ni wengi wanatembea na waadhirika lakini bahati nzuri hawaambukizi na hata kama ukikuta umepata sio mwisho wa maisha yako hutakufa leo au kesho wengi wanaukimwi lakini bado wanaishi na wanandoto zao bado kwa hiyo dada ukapime wala usiogope achana na huyo mwaume maana hata kama alikuwa hana maambukizi hakufai kwani anashugamami pole usiache kusali Mungu atakuonyesha njia katika haya God bless you

  ReplyDelete
 3. Pole shoga mi nakushauri kama ww ni mkristo kimbilia kanisani okoka na mgeukia Mungu atakuwa msaada wako pekee halafu sisi wasichana jamani tusiwe tunaforce sana kuolewa heri mtu akutolee mahari akuache hata ukichekwa wewe una amani binafsi kuliko kuvamia ndoia zenye mateso Mungu alikuepusha na kitu ndo mana hakutaka hiyo ndoa iwepo wewe ukalazimisha matokeo ni kuumia siku zote sio lazima uolewe jamani

  ReplyDelete
 4. Dah pole mwaya, wacha nikupe pole mwakwetu mtoto mdogo umekutana na makurumbembe ya mjini. Ninachokushauri nenda kapime tu kwa hiyari yako maana kwa kuwa umjamzito lazima watakupima ukimwi utake usitake na majibu utapewa. Kupima wewe kwa hiyari yako itakusaidia sana kwani kwanza utapata ushauri nasaha na utapima bila wasi wasi.

  Kingine ni hivi mdogo wangu inawezekana huyo mwanamke anatumia hiyo njia kuwafukuza wachumba wa huyo kaka kwa kisingizio cha HIV na wote wakifika stage ya kupima wanaogopa. Kwa hiyo wewe nenda zako kapime, majibu yoyote yapokee bila wasi wasi, na kupima itakusaidia kujua namna ya kumkinga mtoto wako asipate maambukizi. Kingine inawezekana hana au hajakuambukiza huo ukimwi. Mimi ninalea watoto 2 mmoja aliambukizwa na mmoja hakuambukizwa. Yule aliyeambukizwa sasa hivi ana miaka 8 (alizaliwa na virusi) na kadiri anavyotumia dawa na kutokupata maambukizi mapya ndivyo afya yake inavyoimarika, nafikiri karibu watasema yuko clear!! Tena ukimuona kanenepa vizuri kwa sababu ya dawa.


  Kwa kuwa mtu mwenyewe sio mume bado ni bora ujiondokee zako lakini kuhusu mtoto wake wala usimfiche mwambie wazi uko na mimba yake lakini huna haja nae kwa kuwa umethibitisha kuwa ni mzinzi!

  Uwe umeambukizwa au la na wewe Mungu atakujaalia utapata mwingine. Na hili liwe fundisho kwetu hata tulio ndani ya ndoa tupime afya zetu mara kwa mara.

  ReplyDelete
 5. pole sana mdogo wangu walimwengu ndivyo tulivyo kupenda kuharibu maisha ya wengine.. ila kikubwa mimi nakushauri uende ukapime kwa sababu hiyo huwezi kuiepuka maana ukianza clinic lazima utapima ukimwi.
  kuhusu matunzo ya mtoto mungu atakupa njia na atakuwa na pia wewe utakuwa umeshajifunza na utakuwa makini.. pole sana,

  ReplyDelete
 6. Ni mazito yalokufika binti mdogo sana,lkn kwa mungu ni madogo muombe atakufanyia wepesi.nenda kapime

  ReplyDelete
 7. poleee sana binti, kilichobaki ni kuacha ya nyumna uangaliembele, huyo mwanaume achana nae kabisa, kaa chini ufikirie mwanao utamleaje?? na usianze kuona maisha hayaendi tena kwavile uliacha shule mapema, hapana ndo kwanza uanze fikiria ufanye nn uweze kumlea mwanao, hata kama utafanya mamantilie, ilimradi unajishughulisha, ukiwa ni mchakarikaje, ideas zinakuja, maisha ni safari, na safari ni hatua. usikate tamaa ya maisha, unaweza kama unania, na mungu hakupi kilema akaacha kukupa na mwendo, amkaa na kataa kuwa tegemezi kwa mtu, la sivyo uatajikuta tena unaanza tafuta wanaume wengine waweze kukutunza.
  na ofcourse muombe mungu wako sana kwa kila jambo, mtangulize yeye mbele na ukikazana kwenye maisha hamna litakalokushinda.
  all the best

  ReplyDelete