Friday, August 17, 2012

Msaada Tutani..

Dada Rose, Samahani mimi nimeolewa na ninakaa nyumba moja na mama mkwe wangu, ninamtoto mdogo wa mwaka mmoja na miezi mitatu, mwanangu sijui amechelewa kutembea kama ninavyoambiwa na ndugu wa mume wangu ama kila mtoto anawakati wake ninavyoamini mimi.

Sio kwamba hatembei kabisa, anatembea ila akitembea hatua kama tano sita anadondoka miguu yake haina nguvu kabisa hata ukimuona, siku moja hivi wiki iliyopita ilikuwa jumamosi nikawa nimetandika mkeka kwenye baraza nimelala na mwanangu nimemkumbatia na miguu yake nimeiweka katikati ya miguu yangu.

Nikiwa usingizini nikamsikia mama mkwe akiniamsha kwa jazba nikawa nashangaa huyu mama vipi? akaniambia kumbe wewe ndiye unayemuaribu mtoto kisa nimelala miguu yake nimeiweka katikati ya miguu yangu, kwamba lile joto langu ndio linamvunja nguvu ya miguu!!!!!!!!!!!!!!!! mbona nilishangaa.

Kuuliza hapa na pale watu wanasema kama unamimba nyengine labda inaweza kumvunja miguu lakini kama huna wala hamna kitu kama hicho, lakini mama mkwe wangu yani kalichukulia ishu kubwa mpaka mume wangu alivyorudi baada ya salamu hilo ndio la kwanza kumwambia, na mume wangu ananiambia tu nimsikilize na kufanya kama mama anavyoniambia!!

Jamani heti hii ni kweli maana mimi napenda sana kila nikilala nimkumbatie hivyo mwanangu

Mama Zulpher

Reactions:

4 comments:

  1. Mama Zulpher, kwa sasa tupo kwenye karne ya 21 na si kama zamani watu tuna assume kwa kupitia experience. Embu mchukue mtoto mpeleke kwa daktari wa watoto wacheki hiyo mifupa na sio mama mkwe kudetermine nini kinamsumbua.Mpeleke mapema kabla viungo havijakomaa, unawezakuta yuko overweight na hapa daktari atakushauri vyakula gani vya kumpa.

    ReplyDelete
  2. Uongo mtupu mi wa kwangu alitembea na umri huo nae alikuwa hatembei kabisa tukamchongea kigari cha matairi badala ya kusimama ye akawa anapiga magoti ba kusukuma nikampeleka hospitali dr akasema mwanao ana mifupa mikubwa na mizito sana atachukua muda kutembea vuta subira hatimae akaja kutembea akiwa na umri huo wa mwanao na tena kwa kusuasua akitembea anaanguka sasa hivi ana miaka saba anatoka baruti balaa nikikumbuka huwa nacheka mwenyewe alivyotutia wasi wasi binaadam tumetofautiana, omba na mungu pia mana masimango ya mama wake nayaelewa sana.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli acheni kumdanganya mwenzenu.. Hii ni imani ya kweli kabisa hamna cha karne ya 21 wala 24 hapa. Zingatia ushauri wa mama mkwe wako sio kuwaona kila akuelekezacho ni ujinga

    ReplyDelete