Monday, August 20, 2012

Chezea Jiji wewe..Utaumbuka

Jamani kuna watu wawili nimekutana nao wakawa wanahadithiana jambo nikashindwa kuvumilia nimeona niliweke humu japo na wewe uweze kulijuwa na kwa njia moja najuwa linaweza kukusaidia.

Nyie wanaume msio ridhika na wake/wanawake zenu miye huwa napenda kuwaita magude gude mwanaume usione sketi imekupitia mbele mate yanakutoka!!! yani wewe tundu ni tundu kama ndio hivyo kajaze tundu la choo tuuone uwanaume wako!!!

Sasa wewe gude gude ukae kujuwa mjini sasa hivi wanawake wamecharuka, mwenzako mmoja juzi kaiibika  mume wa mtu mzima kaaga kwa mkewe anaondoka kikazi siku nne kumbe mwanaume kajichimbia kwenye hoteli moja mbezi kampata gume gume moja la hatari (chezea wanawake wa mjini wewe!!!!) basi kijana kalipia hoteli kajiingiza mzima na hilo gume gume lake siku ya kwanza fresh yule mwanamke sindio akaona mwanaume sindio huyu basi kijana alitoka kuelekea kula wakati mwanamke anamalizia kuoga yule shosti akapanga dili na rafiki yake wa kiume kwamba aje awafumanie na ajifanye yeye ndio mumewe akampa mpaka namba ya chumba kwamba aje na watu wajifanye waandishi wa habari usiku wa siku ya tatu.

Usiku wa pili pia ukawa mzuri malavidavi kibao, usiku wa siku ya tatu wakiwa wamelala saa nne usiku wakasikia hodi yule dada akasema ngoja nikafungue mpenzi, kufungua akajifanya mume wangu!! basi yule rafiki yake akaingia ndani na wale watu waliojifanya waandishi wa habari akampiga kibao kimoja cha hatari yule dada akadondoka na kuanza kumtukana sasa yule mume wa mtu akaanza kushangaa kumbe wewe mke wa mtu kabla hajajibiwa yule kaka akamfwata kutaka kumpiga watu ndio kujifanya wanamuamulia basi yule mume wa mtu ndio kuomba msamaha na kumuomba asitoe kwenye habari atalipa hela yoyote anayoitaka kwani akifanya hivyo atamuharibia ndoa yake na wadhifu wake kwa jamii.

Yule kaka mara kibao akawa anakataa madai yake anauchungu na mkewe baadaye wale waliojifanya waandishi wa habari ndio kumuomba akubali basi kijana akamwambia nataka milioni tano yule kaka akakubaliana nao kwmaba kesho warudi pale hotelini basi wale waandishi wa habari feki wakampiga picha akiwa na yule mwanamke ili hata akiwatoroka wazirushe zile habari.

Basi kweli kesho yake wakarudi tena bila yule mwanamke, kweli wakamkuta yule kaka na wakapewa millioni zao tano wakaondoka zao.

ONYO

Huu ndio umekuwa utapeli wa mjini siku hizi jamani sasa wewe unayejifanya chovyachovya ukiona mchuzi unatakaa kuutia kidole uonje ladha shaurilo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment