Thursday, August 2, 2012

Mama weeeeee....

Dada Rose, natumaini wote huku ni wazima dada naomba ushauri maana nimeona huyo dada wanyuma ameweza kutoa ushauri na watu wakamshauri nimepata moyo na kuweka pembeni aibu yangu na kuomba ushauri.

Dada mimi ninakaa na mwanaume ambaye kwa sasa nimeshazaa naye watoto wawili mapacha wanamiezi minne, kabla ya ujauzito mapenzi yetu yalikuwa motomoto lakini baada ya kubeba mimba mwanaume huyu akaanza vituko vya ajabu, mara anachelewa kurudi, hela ya matumzi hatoi hapo nikiwa na mimba mpaka najifungua vituko tu haviishi, kuna wakati siku moja akaniletea mwanamke ndani akaniambia ni dada yake mtoto wa baba yake mkubwa.

Yule dada nilimkaribisha vizuri nikijuwa ni wifi yangu kumbe alikuwa mwanamke wa huyo baba watoto wangu, nilikuja kujuwa baada ya siku moja nikamwambia baba watoto natoka kwenda kufanya mazoezi kunyoosha miguu nikawahi kurudi kabla ya saa yangu ya kawaida nikawakuta chumbani kwetu wakichuma tunda la ndoa!!!! sikuamini macho yangu nilijikuta nimenyanyua chupa ya pafyumu na kumpiga nayo baba watoto yangu ya kichwa ndipo waliposhtuka.

Nilipomuuliza akaniambia kwamba kwao wamakonde ni ruhusa kulala na dada ambaye sio wa tumbo moja, huku akiniomba msamaha nilipokataa kumsamehe akaniambia kama sitaki hawezi kunibembeleza niachane naye, akaondoka na huyo dada!!!!! wakarudi wamelewa nilikuwa nimelala kitandani akanishusha nilale chini wao walale kitandani kwakuwa nilikuwa na tumbo kubwa sikutaka kubishana naye maana angeishia kunipiga basi nilishuka nikalala chini, na hata nilipojifungua akawa ananiambia utalala na hivyo vipaka vyako chini usitubane kitandani!!!! kweli leo mimba tuliyoitunga kwa furaha imezaa vipaka???

Siku nikajifungua yule dada hapo hajaondoka bado, nikawa nalala sebleni sasa na watoto maana tulikuwa tumepanga kwenye chumba sebule jiko na choo, wazazi wangu wapo kijijini hata nikiwaambia hawatakuwa na lakunisaidia zaidi tu ya kuniambia niondoke na nitaenda wapi na hawa watoto wachanga!!

Hata baada ya kujifungua baba watoto hakuwa ananiachia hela ya matumizi natapatapa kwa majirani kuomba kufanya kazi nikiwa nimebeba watoto wangu nipate japo hela ya kuweza kula watoto wanyonye, kiukweli mimi sikusoma nilikutana naye kwenye mziki tukapendana maana nilijuwa anakazi nzuri kwamba atanisaidia mbeleni kumbe nilijitumbukiza kwenye mtoto.

Madharau yake yakazidi nikashindwa vumilia nikaamua kuondoka kwenda kwa mama yangu mdogo sinza huko nilikaa kwakuwa hakuwa na mume akanisaidia kulea watoto (sikuwahi kusikia kutoka kwa baba yao mpaka sasa wanamiaka mitano), huku nikifanya kazi katika saluni ya kiume nikakusanya hela nikajiendeleza kusoma kompyuta nikasoma kwa bidii nikamaliza, nikasoma qt nikamaliza sasa nimepata kazi katika stationary moja ambayo ndio nipo, basi mwenyewe nawahudumia watoto na mama yangu mdogo vizuri tu maana sijahama.

Sasa juzi nikiwa natoka kazini nikautana na baba watoto wangu kituo cha basi yani nilivyomuona nilitaka kulia kwasababu alivyokonda na kuchakaa nikamsalimia wakati naondoka akaniomba namba ya simu ili apige aongee na watoto wake na mbaya zaidi kilichonisikitisha akaniomba hela ya kula jioni!!!!!!!!!!! akaniambia tokea nimeondoka maisha yamekuwa magumu sana kazi alifukuzwa nyumba akashindwa kulipa kodi akafukuzwa vitu ilibidi auze ili apate chakula zilipoisha ndio anabangaiza na maisha akitafuta kazi mpaka leo hajapata.

Alivyowapigia akaomba kuja kuwaona alipofika akaanza kulia na kuwaomba msamaha mbele ya mama yangu mdogo akamuomba mama yangu mdogo amuombee msamaha kwangu turudiane tulee watoto!!!! hata aibu hana kasahau kabisa mateso yote aliyonifanyia hana hata aibu

Rohoni sina hata hamu naye, ila watoto tokea wamuone baba yao na anavyojishauwa kuja kuwaona mara kwa mara wanamlilia kila akiondoka, mama yangu mdogo ananiambia nisiwe na roho ya chuma nimsamehe kwa ajili ya watoto kweli mtu unaweza kumsamehe vipi naanzaje???

Stellah

Reactions:

12 comments:

 1. Kwa kweli mimi naomba umsamehe sana tu na mruhusu kuwaona watoto ila kurudiana naye big NO!!! Hana hela hana kazi ndo anakutaka ili na yeye ukamlee hapana huyo sio mwema tena kwako dada.

  ReplyDelete
 2. Weee mwana wee koma tena koma mwanakwetu, kwani alipokuwa anakutenda hakujua kuwa yeye ni baba wa hao watoto?

  Acha nikwambie maisha yangu huwa nasikia wanaume wanatoka nje ya ndoa zao au wanakuwa na wanawake wengine lakini hii yako ni kubwa kuliko, yaani ulale chini halafu yeye alale kitandani na mwanamke wake wanafanya mapenzi unawasikia? Huo ni unyama uliopitiliza mipaka na huo ni ukatili uliopitiliza mipaka na ulikuwa mentally na saikologikali abused to the maximum.

  Hivi unajua kuwa ikiwa mtu atamkuta mumewe au mkewe na mtu mwingine kitandani wanafanya mapenzi pale pale akampiga na kitu au akamchoma na kitu bahati mbaya akamuua anahesabika kuwa ni kuua bila kukusudia kwa sababu unakuwa umepata kama kichaa fulani? Sasa kinachomkuta huyo baba watoto wako ni adhabu yake kutoka kwa Mungu kwa yale yote aliyokutendea.

  Ushauri wangu ni huu, huyo mama mdogo wako hamjui huyo mwanaume na wala hajawahi kuishi nae, wewe ndio unayajua mateso yake, msamehe awe anakuja tu kuwaona watoto wake lakini USIROGWE KURUDIANA NAE. Ukimsamehe na Mungu nae atamsamehe na maisha yake yatatengamaa, na ukijitia kurudiana nae waweza ambulia magonjwa ya ajabu au hata Ukimwi. Hivi si umesikia mwenzio huko chini amepata ukimwi kwa kujing'ang'aniza kwa mwanaume? Unataka na wewe ukaupate uache watoto wako yatima? Lea watoto wako ukibahatika kuolewa sawa usipoolewa kazi ndio iwe mume wako.

  Wanawake huwa mnanishangaza sana mko so powerful lakini kila siku munajitia unyonge. Achana kabisa na huyo mwanaume ndugu zake aliokuwa akilala nao mpaka akapata laana ya Mungu wapo waache wakatibiane wenyewe hiyo laana asijewaambukiza watoto bure!! Shauri yako makabila mengine kama wachawi!!

  ReplyDelete
 3. du polesana lakini ongela sanaaa niwachache sana wanoweza kuendelea, ikiwa mungu anasamee basi nakushauli na wewe umsamee huyo baba watoto wako, mkapime kwanza, ila ninavyoona kama umemsamee hadi kumruhusu kuona watoto mungu akubaliki

  ReplyDelete
 4. dear Stellah,
  samahani kwa yaliyo kupata,tena umefanya vizuri hata kumleta ndani kwa mama mdogo kuwaona watoto,kitu ambacho hukutakiwa kufanya,mama mdogo ni mzazi na ana zile adabu za kizamani)not in a bad way) lakini wewe nyuma usirudi dada songa mbele,huwezi kum trust him again,na hapo anakupenda na kuomba msamaha kwani huenda wewe tu ndo ulibaki kusikia hizo story zake za kijinga,sasa mwache ajue jiji huyo wifi,sijui dada wa mama mkubwa yuko wapi na wangapi uso wajua,asije akakupa matatizo bure ushauri wa bure hata bibble inakataza jambo alofanya so achana nae nenda shule zaidi kuwa mfano mzuri kwa wanao,piga kitabu usihame kwa mama mdogo ili aweze kukusaidi ulinzi wa watoto,ukiwa shule na kazini na achana na watu kama hao mumeo style watakudidimiza chini daima,hunijui si kujui lakini usije ruka majivu ukakanya moto,achana nae
  maria

  ReplyDelete
 5. pole dada uliyepatwa na haya majaribu haya majaribu wanadamu tumeumbiwa na siyo wewe peke yako uliyepitia haya majaribu hapana kila mmoja chini ya jua anamajari ya aina yake sasa ni hivi ushauri wangu ni huu wewe sijui ni dini gani vyovyote maana woote tunamuabudu Muumba mmoja dada wewe rudisha roho yako usikumbuke ya nyumba kwani mzazi mwenzie ameshajuta sana mpaka hapo alipo anajiona yeye ni msaliti na mjinga kupita kiasi mtu mzima kudanganywa na hawara kkibaya zaidi anamleta mpaka nyumbani ktkt kitanda mnacholalia wote na huku tena una mimba hakuonei hata huruma lakini unaona Mungu alivyo mwema kwako ukaweza kuzaa salama na kumudu kutunza hao malaika na yeye sasa anataabika kweli malipo ni hapahapa duniani mimi kwa ushauri wangu mpokeee kwa masharti unayojua mwenyew na umwangalie kwanza kama amejifunza au lah na pia akapime afya yake asije akukuletea maradhi basi tu kwa vile mmechanganya damu rudisha roho japo inakera sana urudshe roho utabarikiwa zaidi lakini kupima afya ni lazima sana good luck n.b na huyo mama mdogo nampa hongera sana kwakukusadia sio wote wanye moyo kama wake Mungu ambariki sana

  ReplyDelete
 6. no hard feelings but umsamehe mpka apate kazi coz km ni jobless mzigo huo utakua wako!

  ReplyDelete
 7. yaani hadi nimetaka kulia msamehe 2 maisha ndo yalivo ndugu yangu mungu alimuadhibu baada ya kukutelekeza na watoto

  ReplyDelete
 8. Pole dada kwa mtihani huo mkubwa katika maisha yako. Huyo kaka alikuona wewe ni mjinga na ulikuwa hujiwezi kwani ulikuwa unamtegemea kwa kila kitu ndio maana alikufanyia huo ushenzi. Hata hivyo tabia haina dawa amini usiamini akipata kazi tena atarudia yale yale. Chonde chonde usirudiane naye kabisa. Kama watoto aje tu kuwaangalia. Mark my words atakuja kukuumiza tena kama unarudiana naye. Kazi kwako maana huo ni mzigo kubwa zima hilo uaanze kulilea.

  ReplyDelete
 9. Usimrudie kabisaa mruhusu tu kuwaona watoto. Asije kukuletea Ukimwi ukashindwa kuwalea watoto. Ni hayo tu.

  ReplyDelete
 10. pole kwa yote Stellah,nakushauri msamehe mzazi mwenzio ila usirudiane nae kimapenzi asilan maana utarud kule kule! wanasemaga tabia ya mtu huwa haibadiliki, ss hv hana hela hapo anakuwa mpole utamsamehe na kumtunza akija kupata kaz na hela tena utatendwa vile vile kama mwanzo! cha muhimu mruhusu awe pale kwa ajili ya watoto wake,atakapotaka kuwaona sawa na akipata kipato ili awasupport wanae ww mruhusu tu maana anafanya wajibu wake pia kwa kuwa amejitambua kwa hlo. ni hayo tu dada,mwisho wa siku mwenye maamuz ni wewe.

  ReplyDelete
 11. Usimsamehe kabisa lea wtt wako kwa amani akipata tena atakutelekeza

  ReplyDelete
 12. Unanisikitisha,yaani unaweza kuwa kurudiana na huyo mwanaume baada ya mambo yote aliyokufanyia. Ana interest now,coz hana kitu na wewe unaweza kumuhifadhi. Mungu alikuonyesha live kuwa yeye is chaguo lake,chapa mwendo dada.pigana utunze wanao

  ReplyDelete