Tuesday, July 31, 2012

Msaada Tutani..

Jamani mimi ninaswali haswa kwa waislamu ambao mnaijuwa vyema dini yenu naomba mnieleweshe msikiti ni sehemu takatifu tunalifahamu na pia huruhusiwi kuingia na viatu na mpaka utawadhe ndio uingie je ukiwa kwenye hedhi unaruhusiwa kuingia????

Na je mtu anapoenda kuslimishwa kuwa muislamu akiwa na mimba ni vibaya eti mtoto hufa???? maana nina mdogo wangu anatarajiwa kuolewa na muislamu huku akiwa na mimba ya miezi sita wiki mbili zilizopita alipelekwa msikitini kuslimishwa halafu wiki iliyopita akaumwa uchungu tukamkimbiza hospital na kukuta mtoto alikuwa amekufa wiki moja iliyopita wiki hiyohiyo aliyoslimishwa kuwa muislamu.

Kwetu sisi tunaamini ni mpango wa MUNGU yule mtoto alikufa lakini wapo watu na majirani wanasema ni kwasababu alienda kuslimishwa wakati alikuwa mjamzito!!!!!!!! jamani hili lina ukweli gani?

5 comments:

  1. Hakuna mahusiano mimba na kubadili dini iwe kiislam au kikisto hy ni mipango ya Mungu huyo mtoto kufariki.

    ReplyDelete
  2. Dini ya kiislam haingiliani na malaika akiwa tumboni mtoto alokua tumboni ni muislam automatic mama akisilimishwa anakua muislam na kilichopo tumboni mwake. Kuhusu hedhi ni chafu kama viatu huna ruhsa ya kuingia msikitini kusali,kufunga au kusoma qur an kama una hedhi. Mtoto amefariki kwa matatizo mengine na si kuingizwa mskitini akiwa tumboni.

    ReplyDelete
  3. jamani kuslimisha hakuhusiani kufa kwa mtoto jamani, ukiwa kwenye hedhi huwezi kuingia mskiti,pia asingeweza kufunga ndoa akiwa na mimba yenye umri mkubwa kiasi hicho japo kwa sheria za kislaam hupaswi kufunga ndoa ukiwa na mimba.

    ReplyDelete
  4. Hakuna uhusiano wowote wa mimba na kuslimu hiyo ilitokea mipango ya mungu,mwanamke haruhusiwi kuingia msikitini,wala kutamka quran wala kushika masahafu ananpokuwa katika hedhi.
    Anayekwenda kuslim cna uhakika kama itakuwa tabu kwani ni mgeni na ndio kwanza anaingia uislam

    ReplyDelete
  5. Mpe pole huyo msichana Mwenyezi Mungu atampa aliye bora zaidi ya huyo aliyejiondokea zake bila kuiona dunia kwani yeye ndiye mpangaji na mjuzi wa yaliyo sirini na dhahiri.

    Kwanza kusilimu au kurudi katika uislamu (watoto wote wanazaliwa kuwa ni waislamu kisha wazazi wao ndio wanawabatiza na kuwakuza katika dini nyingine) hakuhitaji lazima kufanyike msikitini, hata uwanjani tu ingefanyika au hata ndani ya nyumba au popote pale ambapo mola wako amekujaalia. Rafiki yangu mmoja mama yake alisilimu ndani ya ndege ikiwa juu angani akamwambia binti yake na mkwewe (mume wa binti yake) kuwa naomba mnisemeshe shahada. Basi huko huko juu akashahadia kuwa hakuna Mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na Muhammad ni Mjumbe/Mtume wake na Issa bin Mariam ni Mjumbe/Mtume wake. Basi ndege imetua na yeye kateremka kwenye ndege akiwa msafi hana dhambi kama ile siku aliyozaliwa kutoka tumboni kwa mama yake! Subhannallah.

    Kwa hiyo huyo mdogo wako aliposhahadia alifutiwa madhambi yake yote na hakukuwa na jambo la yeye kupoteza mtoto wake isipokuwa maradhi au wakati tu wa huyo mtoto. Mpe pole na umwambie awe na moyo wa subira na wala asikufuru kwanini yeye.

    ReplyDelete