Wednesday, July 25, 2012

Mmmhhhh...Hapana

Dada Rose pole kwa majukumu na ninatumaini wewe na wote humu ni wazima, kwakweli ninajuwa kwamba kila binadamu anamatatizo yake lakini matatizo mengine kamwe hayawezi kuvumilika.

Kaka yangu ameoa msichana wa kitanga, sio kwamba anauwezo sana hapana wanamaisha tu ya kawaida wanakaa kwenye nyumba yao ambayo ina vyumba viwili yani chumba na sebule, na wanawatoto wawili wote wa kike, baada ya mwaka wa ndoa wifi yangu huyu mama yao akafariki na baba yao alishafariki zamani sana kwahiyo yeye akiwa kama mkubwa akaamua kuchukua wadogo zake ambao ni wakubwa kuja kuishi kwao, wakati wanaweza tu kupangishiwa chumba kimoja labda na msaada wa kazi na maisha yakaendelea.

Japo wanapata tabu maana inabidi sasa wale wadogo wa wifi yangu walale sebleni yani nyumba ukiingia sebleni kuna mabegi ya nguo, magodoro yani sio sehemu unayotaka ukae upumzike baada ya uchovu, kaka yangu wakigombana na mkewe ndio anaona kama wale kuwa pale ni tatizo lakini kama hawajagombana wewe kama ndugu ukimwambia anaenda kukusemea kwa mkewe basi utafumbiwa taarabu mkikutana kwenye shughuli mpaka uchoke.

Jumapili iliyopita kaka yangu akanipigia simu kwamba ametoka kazini kufika nyumbani akakuta ugeni, na vitu nje yani kama kuna chumba ki wazi kimepata wapangaji, alipomuuliza mkewe vipi mke wake akamjibu mtoto wa mama yangu mdogo kapata matatizo kwenye nyumba aliyopanga ndio amekuja hapa mpaka atakapopata nyumba ya kuhamia!!!!!! na huyo dada yake anawatoto saba, jumlisha wale wadogo wa mkewe tisa, na mkewe na mume kumi na moja, pamoja na watoto wawili kumi na nne, jumlisha mjukuu wa dada (mtoto wa yule dada mmoja anamtoto) kumi na tano wote hao wanaishi kwenye chumba kimoja na sebule!!!!!!!!!!!!imebidi sasa kaka yangu awe analala kwa rafiki yake apishe watu waweze kulala mpaka chumbani kweli hii ni haki???????

Ndoa ndio inavyotufundisha hivi jamani? kisa umeoa ndio ubebe msalaba kiasi hiki??? kweli hii ni akili ya mtu kweli ama kuna mengine hapo yamechovewa???? hali ile inamkera kila mtu lakini kaka yeye amekaa tu kimya hana la kufanya, nyumba yake mwenyewe kushinda anaiona chungu kutwa anashinda kwa marafiki zake jioni ndio anarudi kula halafu aondoke akalale.

Kweli ndoa sio mchezo wa kuigiza.

Leila

Reactions:

3 comments:

  1. Karogwa kakako sio buree!!!na huyo dada amechanganyikiwa jmn mishipa ya aibu imemtoka

    ReplyDelete
  2. Kama nyinyi ni wakristo, peleka maombi kwa Baba mchungaji nakwambia siku au wiki hiyo hiyo utaona anajirudi nakufanya maamuzi sahihi, haiwezekani nyumba ikawa kama behewa la treni, kwanza hata mwenye nyumba akijua watu wengi kiasi hicho wanakaa kwenye nyumba yake lazma awafukuze upangaji., huo ni upuuzi na inaelekea wifi yako kamshika sana kaka yako. Kwa jina la YESU ashindwe kama kuna mambo ya kishirikina.

    ReplyDelete
  3. Inaitwa Tanga line hiyo. Kaka yetu alijitia kichwa ngumu...akashikwa kashikika...alikuja kukumbuka shuka kumeshakucha...anajutia ujana wake alopoteza maana kajizeekea hana mbele wala nyuma

    ReplyDelete