Tuesday, April 17, 2012

POMBE YAWEKA KUMBUKUMBU KWA MWANANGU...

Rosemary natumaini wote ni wazima, leo naandika kwako nikitoa onyo kwa wenye ndoa wote na hata wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa.

Ijumaa kuamkia jumamosi mume wangu kama kawaida yake mara nyingi kuchelewa kurudi nyumbani alirudi saa tisa usiku akiwa amelewa sana, na katika kugonga afunguliwe mlango ndipo mwanangu wa miaka mitatu akaamka na kunishtua kuniambia "mama baba aita lango" basi nikaamka na kwenda kutaka kumfungulia kelele zake na fujo za kutaka kufunguliwa mlango zikawa nyingi nikamwambia kwani mpaka saa tisa unafanya nini huko kulewa kila mara na ukija nyumbani unasema huna hela ya kutuachia ya matumizi kweli hii ni sawa, na kwanini utembee usiku wote huo mara kwa mara siku ukivamiwa na majambazi kilio kitakuwa cha nani basi mume wangu akasema unakataa kufungua akaupiga teke mlango na kuingia ndani nikiwa bado nashangaa kilichotokea akanza kuzozana na mimi na kuishia kunipiga sana.

Wakati wote huo ananipiga mwanangu alikuwa amekaa tu anatuangalia, baba yake akanipiga na hata kufikia kunikaba yeye anatuangalia tu kumbe yale mambo alikuwa anayaingiza tu akilini baada ya huo ugomvi ambao kesho yake ulikuwa gumzo mtaani baada ya majirani asubuhi kunipa pole walivyoshtushwa na ule mlango kuvunjwa na kusikia nikipigwa.

Niliumwa sana na kulazwa hospital nilivyolazwa wazazi wangu wakanichukuwa na kunirudisha nyumbani kwao ambako nipo mpaka leo naendelea kuuguzwa, huku mume wangu akiwa wala hana shida yoyote ile akisema hakufanya kosa lolote na baba achelewi nyumbani na akiamua kunipiga ataendelea kunipiga maana pale ni kwake na mimi ni mkewe.

Sasa kilichoniuma zaidi kuhusu haya yote jana nilipokuwa nimelala kitandani mama yangu akinichua mgongo kwa dawa nilizopewa hospital nikiwa nimejipumzisha baada ya kuchuliwa aliingia mwanangu akapanda kitandani na kufanya jambo ambalo lilinitoa machozi bila kutegemea akamwambia bibi yake "bibi baba akaba mama hivi (akiwa amenikaba na mikono yake midogo miwili) akarudia akaba mama hivi baba" kwakweli niliumia sana kwa maneno aliyotoa mwanangu.

Naandika hii leo kwenu nyie wenye watoto tafadhalini mkitaka kugombana jifungieni chumbani mkiwa wawili mgombane mpaka mwisho mkitoka nje hata watoto wasigundue kama mmegombana maana mnapogombana mbele ya watoto japo hawawezi sema kitu leo lakini uchungu wao utadumu nao milele na ndio maana tunaona mara nyengine mtoto anakuwa hampendi baba yake kwakuwa tokea anakuwa anaona vurugu baba yake anazomfanyia mama yake.

Tujifunze..

Mwanahawa

2 comments:

  1. Pole sana Dada. Kwakweli inasikitisha sana tena inaumiza. Nakushauri umkabidhi Mwenyezi Mungu ndoa yako ili aweze kusaidia. Yeye husikia sauti zetu na kujibu maombi yetu. Mungu ni mwema.

    Yaani ni bahati mbaya sana hili tukio limetokea mbele ya mtoto. Hakustahili kuona kabisa hiki kitendo. Lakini ndo ivo imeshatokea. Ni ngumu sana kwa mtoto kusahau maana mpaka sasa anaona jinsi gani unavyougulia kitandani na mama akikuuguza.

    Nakushauri ujaribu kumkeep buzy huyu mtoto. Mpeleke acheze na wenzie na afurahi, usimwache akae ndani tu. Mnunulie matoys achezee, kama kuna cartoon za watoto mwekee na si kucheki hii michezo ya watu wazima kwenye Tv. Kama unaweza mtoe out akatembee au hata kumpeleka kwa ndugu jamaa na marafiki ilimradi apoteze mawazo. Jaribu kuiweka brain yake iwe accupied na activities nyingi ili aweze kurefresh kidogo. Kaa ongea naye muadithie hadithi mbalimbali, muimbie , kama kanisani au msikitini mpeleke akacheze na wenzie na kusikia neno la Mungu. Yaani tafuta all alternatives ya kumsaidia mtoto wako. Hii kitu ni serious mana unaweza shtukia na yeye anaanza piga wenzake akidhani ni kitu cha kawaida, so jaribu kila uwezalo kumfanya mtoto afurahi. Ukiona hauko kwenye mood tafuta mtu wa kukusaidia. Jitahidi sana kutomuonyesha machungu yako, kama ukisikia kulia nenda chumbani jifungie au ingia bafuni nawa uso. Jifanye upo ok mbele yake ili taratibu asahau.

    Nakushauri sana Muombe Mwenyezi akusaidie, kama yeye ndie aliyekubariki nakukupa huyu mtoto basi ana uwezo pia wa kumbariki mtoto wako na kumfanya asahau. Na pia anauwezo wa kuibariki na kuilinda ndoa yako.Usiache kumuomba. Peace Jb

    ReplyDelete
  2. Wanawake kila siku tumekuwa tukibaki kwenye uhusiano wa kibabe hivi tukisema nalea wanangu, unamlea au unamharibu hayo anayoyaona hayafai kwa mtoto, ukiona mambo yamezidi jiondoe jamani haaa
    Ndio maana kule kenya wanawamwagia maji ya moto, jitu limelewa linakushindaje??
    AAARRGH

    ReplyDelete