Thursday, March 15, 2012

SOMO......

Somo la leo ni kwako wewe mwanamke, jamani nimeona na kila siku nalia na wanawake ninao wajuwa, jamani mwanamke ukiwa jikoni vyombo tele vya nini??????utakuwa mwanamke anaunga mboga labda nyama mara ana vibakuli sita ama vitano kimoja kimewekwa vitunguu, kingine nyanya, kingine hoho, kingine carrot, kingine nyama, jamani mwanamke kutumia vibakuli vyote hivi maana yake unajuwa wewe?

Mwanamke kutumia kibakuli zaidi ya kimoja ni kwamba anauwezo wa kumiliki mwanaume zaidi ya mmoja, kwa wamama wanaojuwa wakikuona watakuangalia na kusonya kwa siye tunaojuwa tutakunanga bibi.

Kama unataka kupika nyama imeshaiva iweke kwenye sufuria tia mafuta yako pale ikaange mule kwenye sufuria chukua bakuli lako moja tia kila kitu carrot, nyanya, kitunguu, hoho ikifika muda wa kuweka kitunguu unakimenya moja kwa moja unakikatia kwenye sufuria na vyengine vyote vilivyobaki, unakuwa wa kujiamini bwana hata jikoni, unapika ki mwanamke na kutenga kimwanamke.

Kama hukujuwa ulitambue shosti.

Reactions:

3 comments:

  1. Huo sasa ni uchafu - utawezaje weka kila kitu pamoja? Kama mwanamke malaya malaya tu bwana! hiyo haihusiani kabisa kila mtu na mazoea yake

    ReplyDelete
  2. huyu aliyoandika comment chini atakuwa mwanaume wewe haya ni maneno wadada tunayopewa kwenye kitchen party kwa akili yako wewe umeshafikiria ni bakuli za kupikia, hapo anamaanisha kama mwanamke unaweza kumudu mwanaume zaidi ya mmoja sio mpaka kila mtu ajuwe wewe unabaki na mumeo huyo kama haelewwki unatafuta wengine lakini katu mtu asijuwe watu wakijuwa watakucheka na kukuona malaya, ndio maana ya alivyoandikia.

    ReplyDelete
  3. aksanteeee, maneno kuntu haya, wachache wenye kuweza kuyatoa na wachache wanaooweza kuyaelewa.asante rose kwa somo, akuu babuu mie na kibakuli chango kimoja, na sufuria yangu safiii mboga haijatapakaa sufuria nzima, iko kati kati, na mwiko wangu msafii haulali na mboga mboga wala maugali. he he hehe hehe uwamawake sio lele mama... shauri yako!!

    ReplyDelete