Monday, March 5, 2012

MKE WANGU UTANIFUNGA JELA MIYE...

Jamani wenzangu wa kijiwe hiki, miye nimeoa nina mke na watoto watatu, mke wangu ni mama wa nyumbani na mimi ninafanya biashara zangu za hapa na pale ilimradi tu mkono uingie kinywani.

Kwa utajiri nitasema mimi ni mtu tu wa kawaisa sina uwezo mkubwa, mpaka sasa mke wangu anataka nikafie jela yani, maana mwanamke huyu vituko havimuishi, yani ananinadai vitu vya bei vikubwa mpaka naogopa, juzi kaalikwa kwenye sherehe ya shoga yake naye ni mama wa nyumbani kama yeye sasa hiyo shere ilikuwa ya birthday ya rafiki yake kapewa rav 4 na mumewe mke wangu kurudi nyumbani maneno kibao jinsi mume wa shoga yake anavyompenda mpaka kumnunulia gari.

Mara juzi ananiambia anataka nimnunulie dhahabu na nisipo mnunulia patakuwa hapatoshi, kweli nikajipinda weeee mpaka nikamnunulia.

Sasa pressure ikanipanda jana na kuona kweli huyu mwanamke tunapoelekea atanifanya niozee jela, nimekaa nyumbani mara nasikia hodi kwenda kufungua mjumbe na mbaba mwengine ambaye simjuwi, kaja ananiambia huyu baba anashughulika na mikopo na mkeo amekopa hela kwake na hajalipa kwahiyo tumekuja kukueleza utulipe la sivyo vitu alivyoandikisha mkeo kwenye mkopo vitachukuliwa.

Nikawaahidi nitaulipa wanipe wiki mbili tu, tukaandikishiana wakaondoka, mke wangu alipokuja nikamuuliza kuhusu kukupo jibu alilonipa nilijuta kuuliza "sasa kama huwezi kunipendezesha na kunipa vya gharama niibe?" nimeamua kukopa nami nionekane mtu kwenye watu.

Kwakweli nilijisikia vibaya sana kuona mke wangu anaidharau siwezi kumtimizia mpaka akakope, wakati anajuwa sisi maisha yetu ni ya kawaida tu hao mashoga zake wa gharama sijui ndio wanaomuharibu, sasa leo kakopa dogo namlipia siku akija kukopa pakubwa sipatakuwa balaa?

Mke huyu ni mfanyaje mimi aelewe siwezi maisha hayo atakayo?

4 comments:

  1. pole sana kaka yangu, wanawake tunatofautiana na ukisema umuendekeze ni kweli utajaozea jela kaka. kua mwangalifu na chukua tahadhari mapema either ongea na wazazi wakusaidie, au wazee au whatever hata wamama watu wazima kidogo.

    ReplyDelete
  2. Duuh, pole sana kwa hilo songombingo, well ni ngumu sana ku-deal na mtu kama huyo na mara nyingi ni inategemeana mlianzaje mwanzoni, maana kama mwanzoni mwa mapenzi yenu kuna mahali ulilegea basi ujue HILO UNALOO!!!!!, Well ninachojua ni ngumu sana watu wa namna hiyo, kuna ndugu mmoja ilikuwa kama hivyo sana sana alimwambia mkewe kuwa ukiendelea ni bora urudi kwenu na ndio kidogo akaweza kutulia, maana hapo lazima ukubali kusuka au kunyoa. Akisaha kaa kwao ndio atapata akili kama anaweza kuishi na wewe au hawezi, kama hawezi basi atabaki huko huko, zaidi ya hapo huwa hawasikii hao.
    Ninachofikiri ni kwamba mmeshaongea sana kuhusu hilo ila habadiliki na kama ndio mara ya kwanza basi jaribu kuongea nae na umueleweshe, zaidi ya hapo inaweza kupelekea akakutana na Mapedeghee wa mjini njio wakakusaidia kumpendezesha na kula mzigo pia, Balaaaaa.... na unajua matokeo yake.
    Narudia tena pole sana.
    Ni hayo tuu kutoka kwangu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu yangu pole sana kwa hayo yanayokukuta hiyo ndo faida ya kumweka mama au mke nyumbani asubiri kuletewa ka angekuwa naamka asubuhi huyo na kwenda kubeba mabox sidhani kama angekuwa anakuhurutisha yeye hajuwi uchungu wa kazi au wakutafuta pesa ukweli jitahidi kwenda kwa wazazi au wazee wake mjadiliane hicho ni kifo si kifungo bora ukifungwa utarudi kuliko akuletee mgeni ndani ya nyumba huyo ni limbukeni ,jiahidi mpige marufuku na mashoga na kama hakuelewi wafuate hao mashoga wake wape ukweli na kama unaogopa basi tumia njia za kijasiri jifanye unamzowea mmoja wapo wa hao mashoga wake kisha omba ajira pale kwa utaratibu kisha ukipata ajira mchezo utakuwa umekwisha na ukiamaliza hapo mfuate mwingine fanya kama ulivyofanya kwa huyo ukimaliza genge litakuwa limesambaratika huwaoni tena wanamfuata mkeo na mengi utayapata toka kwao ,ukishindwa mbinu hizo mtimue akasote kwao akiona juwa linamwakia basi ila usimwache kama bado unampenda atakusumbua kwani atakuwa anakufanyia kusudi najuwa mpaka unafikia hapo mambo yanafika shingoni

      Delete
  3. Pole sana. Inasikitisha sana hasa ukizingatia huyu ni mke wako na mmeishi naye kwa muda mrefu.Ila naona anafanya makusudi. Maisha kwa ujumla ni magumu sana ukizingatia mna watoto wa3, sasa yeye asitake kujiringanisha na wengine. Mke wako ni mtu mzima na inabidi tuseme ukweli mana ninacho ona hapa ni ujinga usiokuwa na maana, sorry to say so. Mikono tumepewa ili tufanye kazi kwa nini yeye asitafute cha kufanya na kuona ni jinsigani pesa ilivyo ngumu kupatikana. Labda kama ulimkataza na kama ulikamtaza basi imekula kwako. Mwanamke wa sasa si wa kukaa kupika na kupakua, hapana hizo zama zilishapitwa na wakati. Akina mama sahizi wanajishughulisha na mambo mbalimbali ili kuweza kutunza familia zao na si kujibweteka nyumbani bila kazi yoyote.

    Dina marios anashindanisha wamama wa dar wajasiliamali wadogowadogo ambao kwa jinsi fulani walianza biashara lakini ikafika wakati walikwama. Ukiona historia za hawa akina mama unaweza shangaa. Hawajakata tamaa na bado wanajishughulisha. Sasa wa kwako amekaa nyumbani bila kitu chochote. Ikatokea umeumwa ghafla ukalazwa hospitali itakuaje? Its never too late, mtafutie kitu afanye.Ukiendelea kumwelekeza hatajifunza kitu chochote, mzigo unabaki kuwa wako.

    Nina wasiwasi sana kuhusu hao waliokuja nyumbani kudai pesa zao. Embu chunguza kwa makini kama ni kweli walikopeshana, nenda mpaka ofisini na utafute evidence (risiti au karatasi ya makubaliano na mihuri). Kama hata taka kukusikiliza ita watu wazima waje waongee naye. Sijui we ni dhehebu gani ila katika kipindi kama hiki inakubidi usali sana na kuomba hili pepo chafu lipite na si kuchafua nyumba yako. Mungu ni mwema na husikiliza sala zetu.

    ReplyDelete