Wednesday, February 29, 2012

Dada Rose kuna mkaka ameandika mada hapo mwanzo kuhusu mwanamke wake kuwa hapendi kiumbe alichokuwa amebeba alikibeba tu kwasababu ya huyo baba mtoto wake.

Wala sikushangaa nilipokuwa nasoma hiyo mada yake maan ahata mimi ninakaa na mwanamke wangu naye anatabia kama za huyo dada, nimeshamsema nimeshafanya vikao na ndugu na jamaa wanaotufahamu lakini hakuna nililoliona limebadilika, tofauti ya huyu wangu na wa yule jamanaa ni kwamba wangu hataki kabisa kukaa na mtoto wake aliyemzaa.

Yani mpaka majirani wanamshangaa mama watoto wangu mtoto wetu akiwepo yani nyumba inakuwa haina amani, mwanangu akifanya kosa kidogo tu yani anakuja kuninunia na manenoa kibao na nikimtetea mtoto (kweli kabisa mengine sio ya kumgombeza) ananuna mpaka anapaki vitu vyake na kuondoka.

Kuna kipindi nikamtetea mtoto yule mwanamke akaondoka, siku moja nzima, nikawa sina cha kufanya nikijipa matumaini atarudi nilivyoenda kazini nikampeleka mwanangu ambaye anamiaka miwili kwa jirani ili akae nimchukuwe nikirudi nikawa nafanya hivyo kwa wiki yule mwanamke wala hakurudi na simu yake wala haikupatikana.

Ndipo nilipoamua kumpeleka mtoto wangu kwa mama yangu mzazi amini msiamini alikaa kule mpaka akatimiza miaka minne (miaka miwili baada ya mama yake kuondoka) mama yake wala hakurudi wala hakumtafuta, baadaye nikaamua kutafuta msichana wa kazi wa kumlea ili nimrudishe pale nyumbani nikae naye mwenyewe.

Kwahiyo mpaka leo nalea mtoto wangu na msichana wa kazi yule mwanamke hata sijui yupo wapi hajatutafuta wala simu yake haipatikani kwahiyo hao watu wapo humu duniani.

Na watu wanasema hamna watu wenye roho ngumu kama wanawake.

1 comments: