Tuesday, February 21, 2012

NI KWELI WANAWAKE NI WAKATILI..

ROSEMARY MIZIZI: jamani nataka muelewe picha naweka kunogesha mada zinazotolewa kwani mnafahamu haziji na picha kwahiyo sio walio kwenye picha ndio maada hizo zinawahusu.

Dada Rose, natumaini wewe ni mzima, mada yako ya mwisho uliyoiweka kuhusu huyu kijana mama yake mzazi aliyekuwa anamfanyia vituko kweli kabisa kuna wa mama wa aina hiyo hata kama wanawake wanashangaa wanawake wa aina hiyo ni wengi sana na wapo sema tu jamii haitaki kuweka mambo wazi.

Leo nitakupa kisa kimoja ambacho kimenitokea mimi, kunakipindi kabla sijaoa nilikuwa na mwanamke mmoja ambaye kwakweli tulikuwa tunapendana sana na tulikuwa tukiishi pamoja kama mke na mume japo hata mahari nyumbani kwao sikupeleka siunaelewa tena kimjinimjini?

Basi mimi na yule dada tukaishi kama miaka mitatu hivi ya raha jamani hakuna sijawahi kuona msichana alikuwa na heshima yule yani nilitunzwa mpaka watu wakashangaa, sasa bwana miaka mitatu hiyo siku akanitamkia kwamba anamimba, kwakweli nilifurahi sana kuwa baba lakini cha kushangaza yeye hakufurahi kuwa mjamzito na kuniambia hataki mtoto kwakuwa nilikuwa nataka mtoto na kumuomba sana aiweke ile mimba akaniambia kwamba ataiweka tu kwasababu nataka mtoto lakini sio kwasababu anataka yeye.

sasa nikawa najiuliza huyu mwanamke mbona ananichanganya kama yeye hataki mtoto atailea kweli hiyo mimba mpaka miezi tisa iishe? basi nikawa naye karibu kweli mpaka clinic nikawa naenda naye ili tu nimlinde mwanangu, loohh kunasiku nilichelewa kurudi nyumbani kwasababu kuna deal nilikuwa nafwatilia ya hela mbona nilikuta vidonge mezani na ananiambia ameshakunywa aue huyo mtoto wangu maana ananibebea halafu najifanya mjanja kufanya umalaya barabarani.

kwakweli roho iliniuma sana nilichofanya nikumkimbiza hospiatal nashukuru MUNGU hakuna baya lililompata mtoto, nikawa sasa nawahai kurudi nyumbani na najitahidi kutomuudhi maana itakuwa balaa kweli kabisa yule dada hakuonyesha hisia zozote zile nzuri kwa yule mtoto aliyetumboni mwake, sikuona kama alifurahia ujauzito kama wadada wengine niliokuwa nikiwaona clinic.

Mimba ilivyokuwa na miezi nane yule dada alianza tabia ya kunilazimisha tufunge ndoa, ili mtoto alelewe kwa maadili ya ndoa, sikuona kama ni jambo baya lakini niliogopa kwakuwa kama hana mapenzi na kiumbe kinachokuwa tumboni mwake anawezaje kuwa na mapenzi ya kweli na mimi na mtoto atakapokuja, nilichomwambia ni sawa lakini inabidi kusubiri mpaka mtoto atakapozaliwa alikataa kabisa na akawa mtu tu mwenye hasira na vituko kibao ndani ya nyumba mimi sikumjibu wala kumfanya lolote kwa hofu tu ya kuogopa asimdhuru mtoto wangu.

Ikafika miezi tisa nakumbuka wiki ya kwanza tunaenda clinic doctor anampima njia na kumuambia mtoto kashageuka na yupo salama, basi tukarudi nyumbani siku hiyo vizuri, akanikumbushia tena swala la ndoa nami nikamjibu kama ninavyomjibu mara kwa mara, wala hakusema lolote...hapa ndipo balaa likaja

Kesho yake kama kawaida yangu nikajiandaa kwenda kazini kumbe huku nyuma na yeye anajiandaa, narudi jioni nyumbani sikuti mtu nikajuwa labda kaenda kwao kusalimia, mara saa moja, mbili, tatu mpaka saa saba hamna mtu, wakati wote huo nikiendelea kumtafuta kwenye simu bila mafanikio, nikaamua kuwapigia wazazi wake wakaniambia hakuwa kwao na hajazungumza nao kwa muda mrefu sasa, ikabidi nitoe ripoti polisi huku nikiendelea kumtafuta.

Bila mafanikio sikumpata wiki, miezi,mwaka mara siku moja nikiwa nyumbani nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi mara nasikia hodi kufungua namkuta kasimama mbele ya mlango wangu!!!!! kwakweli nilipata na mshtuko mkubwa sikujuwa la kufanya, kama dakika tano nilibaki tu namuangalia, baadaye nikamwambia aingie na nikaanza kumuhoji nini kilitokea mpaka akaondoka.

Akaniambia alitka ndoa sikumpa kwahiyo akaamua kuondoka kwenda mwanza, mara akaanza kulia na kuniambia alijifungua mtoto wa kiume lakini bahati mbaya akafariki, kwasababu ya safari ndefu ya mwanza wakati akiwa na mimba ya miezi tisa hakutakiwa kusafiri na yeye hakulijuwa hilo!!!!!!! japo jhayo ni maneno yake hata sijui la kuamini maana tokea mwanzo hakumpenda kabisa mtoto wangu..nilichomwambia ni aondoke tu na asiwahi kunitafuta tena katika maisha yake.

Na nyumba nikahama, MUNGU akanisaidia nikapata mwanamke mwengine japo ilikuwa ngumu kuanza kumuamini na yeye tena lakini leo ninafuraha nimeoa na nina watoto wa tatu..MUNGU MKUBWA.

Sasa mtakataa kama kuna wanawake wanaroho ngumu????????

Reactions:

2 comments:

  1. Ubinadamu upo pale pale kuwa binadamu sio mkamilifu,....kila mmoja anao udhaifi awe mke au mume, na kawaida kila mmoja huvutia kamba kwake, ...cha muhimu ni kujirekebisha na kila mmoja ajiangalie mwenyewe jinsi gani anavyotiumiza wajibu wake....au sio.

    ReplyDelete
  2. nakubaliana nawe emu, ubinaadamu upo pale pale, na inawezekana tukamhukumu huyo dada kwa vile tangu mwanzo hakupenda kuuweka huo ujauzito ila inawezekana pia aliyokuwa akiyaongea mwisho (kutaka mtoto azaliwe ndani ya ndoa) yalikuwa ni ya msingi kwake, hapo muhimu ni kujifunza ili makosa kama hayo yasijirudie kwani lawama ni kwa wote wawili. huenda ungekubali ndoa hayo yote yasingetokea na pengine aliikataa hiyo mimba kwa sababu hiyo hiyo ya kuogopa kuzaa nje ya ndoa. muhimu ni kujifunza na sio kumuhesabia kosa mwenzio

    ReplyDelete