Habari zenu kwa ujumla, dada Rose nakupongeza kwa blog yako hii kwakweli inatufundisha mambo mengi na kwa kupitia hii blog leo nimeona bora nitoe shida yangu iliyonikaa moyoni miaka sasa najuwa kwa namna moja ama nyengine nitapata msaada kutoka hapa.
kwasasa nina miaka 29 nilipokuwa na miaka 25 nilibakwa na vijana wawili siku moja nikitoka kwenye starehe usiku, ilikuwa ni experience mbaya ambayo sitakaa kuisahau nashukuru sana familia yangu waliokuwa upande wangu wakati huo wote, na ninamshukuru MUNGU kwakuwa sikuambukizwa magonjwa yoyote na wala sikupata mimba.
Tatizo tokea nilivyobakwa sikuwa tena na mwanaume maana sikuwafurahia, na nilikuwa sina tena hamu ya kufanya mapenzi nilihisi nitakuwa nakumbuka nilivyobakwa kwahiyo miaka yote hiyo niliishi tu single.
Sasa ndugu zangu wameniambia nilazima maisha yaendelee lazima siku moja niolewe na nije kuwa na watoto wangu, wakati umefika wa kuachilia moyo upende tena mwanaume, kweli nilijitahidi na sasa nimepata mwanaume, ni mwezi wa tatu sasa na sijamuhadisia yaliyonitokea na ninapokuwa naye wakati mwengine akinikumbatia nakos amani na kujikuta namwambia aniachie, hata siku moja hatujawahi kukutana kimwili na akionyesha dalili ya kutaka labda akianza kunikiss na kunipapasa namsukuma na naondoka kabisa anabaki tu kushangaa lakini hajawahi kuniuliza.
Kwakweli nahisi yaliyonitokea nyuma yananiathiri sana naogopa hata kumwambia huyu mwanaume si anaweza kuniacha kuna mwanaume atakayesikia hayo na kukaa na mimi? na sasa kushindwa kwangu kufanya naye mapenzi si atachoka kunivumilia na nifanyeje labda niweze tena kufanya mapenzi tena bila uoga?
Hi Dada yangu, kwanza nakupa pole kwa hayo yaliyo kukuta, ila ni jambo la kujifunza hasa kwa wengine ambao hawajakutwa na tatizo kama hilo kuwa wawe waangalifu, kutembea usiku kwa mwana mke siyo vizuri hasa ukiwa pake yako, ikikulazimu sana basi omba mtu akusindikize.
ReplyDeleteKuhusu uhusiano wako na huyo mpenzi wako, kwa kweli hawezi kukulaumu na ni siku nyingi zimepita. Kama kweli unampenda basi huna jinsi, ni kumueleza tu, lakufanya tafuta muda mzuri wakati mmekaa sehemu tulivu mueleze unavyo mpenda na ambavyo ungependa muishi pamoja kama mke na mume, ila umueleze kuwa kunatatizo moja ambalo ina bidi umushirikishe na siyo vizuri bila kufahamu hicho kitu. Basi hapo mueleze kila kitu na umueleze kuwa ndicho kilikuwa kinapelekea tabia yako kutokueleweka. Nina imani kama anakupenda atakuwa mtu wa msaada sana kwako kuondokana na hangover ya tatizo hilo. Ila ninakushauri kama kweli unapenda mje kuoana basi USIMKUBALIE KUFANYA NAYE MAPENZI HADI AKUOE, VINGINEVYO ANAWEZA KUTUIA HIYO NAFASI AKIISHA KUKUPATA AKAKUTOSA NA UKABAKA KUJILAUMU. NJIA PEKEE YA KUMPIMA MWANAUME KAMA ANAKUPENDA KWELI NA ANATAKA KUWA NA WEWE KIMAISHA? NIKUMUAMBIA TUSIFANYE MAPENZI KAMA AKIKUBALIANA NA WEWE HADI KWENYE NDOA BASI UJUE AMEKUPENDA? MWINGINE ANAWEZA KUJIFANYA AMEKUBALKI LAKINI KADRI MNAVYOSOGEA AKABADILIKA KUWA KAMA KWELI UNANIPENDA KWANINI USINIPE? KAMWE USIKUBALI USIJE JUTA.
Nakutakia maisha mema katika mahusiano yako.
I refuse to let a tragic past ruin my life’s story Living |nation.co.ke, www.nation.co.ke
ReplyDeleteDa rose kama unaweza kukopy na kupaste hii story ya huu mama kutoka kwenye hiyo website ya daily nation naona inaweza saidia akina mama wengi na hasa huyo dada mwenye tatizo na past yake. Ni story nzuri na itamsaidia kuona jinsi gani mwenzake mwenye tatizo kama lake aliweza kukabiliana na past yake, tena yeye tatizo lilikuwa kubwa kuliko lako. I hope dada rose anaweza kushare hii story. Pole sana
pole sana, pale jitihada zetu zinaposhindwa ni dhahiritunahitaji msaada mimi nakushauri nenda kwenye maombi ufanyiwe deliverance, huyo ni shetani anapenda kushikilia watu kwenye past,Mungu wetu ni mwema baada ya kupokea uponyaji wako utakuwa sawa kabisa.
ReplyDeletenakushauri nenda kituo cha agape kilichoko mbezi morogoro road,tafadhali.
Dear, pole sana na yaliyokusibu. Pia hongera sana kwa hatua uliyopiga ya kuingia katika mahusiano. Ninaamini kuwa wewe ni mtu mwenye imani, kaa chini usali kumshukuru Mungu kwa kumpata kijana huyu kisha mwombe Mungu akuonyeshe jinsi ya kumweleza yaliyokusibu. Ninaamini endapo mtaweza kulizungumzia hili na kumweka Mungu kati yenu, itawaweka karibu zaidi na utamwamini mwenzio. Katika kumwamini huku, mnaweza kujiandaa kuwa pamoja faraghani. Nakuombea ili yote yaende sawa. Kila la heri na Mungu akubariki
ReplyDelete