Sunday, January 15, 2012

Dada Rose, kuna jambo linanitatiza sana ninashoga yangu ninakaa naye jirani yani ni rafiki yangu sana, ameolewa na anawatoto kwa namna moja ama nyengine sijui ni kwa nini amekuwa mama wa nyumbani maana najuwa amesoma vizuri tu.

Sasa dada tatizo ni hili mimi ninapoenda kazini mara nyingi ninapoelekea kwenye kituo cha bus ninamuona huyu baba anampakia msichana kwenye gari lake yani kama mara nne kila siku msichana huyohuyo!!!!!!! najuwa hayanihusu lakini najisikia vibaya kweli haswa ninapoongea na mkewe maana najuwa juhudi zake za kuimarisha ndoa yake. halafu ukizingatia ni mtaa huohuo anapoishi na mkewe jamani huku si kukoseana heshima?


Reactions:

1 comments:

  1. mmh mtihani nao huu, what u can do usimwambie mke wake moja kwa moja, na kwanza hauna hata uhakika huyo mume anafanya nn na huyo msichana, tusipende kuweka mawazo negative siku zote, kwavile una doubt,chunguza kwanza kwann hasa nampandisha huyo dada. na ukikuta anafanya kitendo kibaya,jaribu kuongea na huyo mume wake na umkanye au hata huyo msichana uongee kistaarabu na aelewe. ukiona ana endelea ndo uweke mazingira ya mkewe ajionee mwenyewe na achukue uamuzi gani. usimuamulie chochote zaidi ya ushauri. lakini kua makini sana usije gombanisha watu bila sababu ya msingi.

    ReplyDelete