Sunday, January 22, 2012

MWENZENU SIPEWI...

Dada Rose, habari yako natumaini wewe na wengine wote wa humu ni wazima, dada mimi leo nataka nipewe ushauri kutoka kwenu, mke wangu ni mlokole mimi sijaokoka naishi tu maisha ya kawaida jambo ambalo silielewi na nimeshatijitahidi sana kumwambia mke wangu simuelewi ni hili yeye huingia katika maombi mara nyingi na kila maombi anayofanya yanamfanya afunge yani anakula mlo mmoja tu kwa siku pamoja na kusali sana.

Sasa mwezi uliopita ameniambia yupo katika maombi ya kuombea ndoa yetu, nikamwambia sawa lakini sikujuwa kama ningepata kasheshe nina wiki tatu sasa kila nikimuomba mzunguko hataki ananiambia mpaka atakapomaliza kufunga, jamani utakuta muda mwengine ninahamu sana na mke wangu lakini kila nikimuomba hanipi kwasababu anafunga anatakiwa kuwa msafi haswa haya maombi yanayotuhusu sisi kwamba tusikutane mpaka atakapomaliza.

Jamani hii ni sawa? maana nimeamua kuwa mlevi sasa maana bila hivyo nitajikuta natoka nje ya ndoa, na yeye anaona ni kitu cha kawaida tu.

2 comments:

  1. hebu jaribu kukaa naye na umueleze kuwa ww na yy ni mke na mume hata akiwa kwenye maombi anatakiwa kukupa, usikute hajui hilo, pole sana grace ngopola

    ReplyDelete
  2. kila siku ndoa ni maelewano, mkiwa na ongea na kuelewana hamna jambo lisiloweza kutatuka, hata sisi waislamu tunapofunga haturuhusiwi ku do, ila jioni ile mpaka usiku b4 alfajiri
    (kuna mda maalum)ndo tunaweza kufanya, kwahiyo kama mume na mke hua mdajadiliana kabisa ili siweze haribu funga zenu.
    jaribu kuongea na mkeo, inawezekana anaona kama vile hujali maombi, sasa basi jaribu hata na wewe kufunga na kuomba nae hilo litampa moyo kuonyesha unajali na eventually hutanyimwa.
    jaribu kwa kila njia kuonyesha uko nae kwenye hayo matatizo na imani utafanikiwa.

    ReplyDelete