Monday, December 19, 2011

Natumaini wote humu ndani ni wazima leo naleta mada hii kwenu yani naandika nikiwa nahasira na uchungu sana moyoni nina mchumba wangu ambaye tunatarajia kuoana mwezi ujao nilikuwa nimesafiri nimeenda mwanza kikazi kwa miezi miwili wakati naruydi sikutaka kumfahamisha nilitaka iwe suprise maana kila siku nikiongea naye kwenye simu ananiuliza unarudi lini nikimuuliza kwanini kila siku unaniuliza ananiambia tu amenimiss kwahiyo anataka kujuwa narudi lini aje kunipokea airport.

Wakati wangu wa kurudi ulipofika nikaona ngoja nisimwambie mpenzi wangu kama narudi nikamfanyie suprice basi nikajinunulisha ndoo ya samaki nilipofika dar cha kwanza nikaenda nyumbani kwa mchumba wangu ili nimpe samaki wake ndio nipeleke wengine nyumbani halafu nirudi kwake baadaye, nilipofika nikampigia simu haikuwa inapatikana lakini gari yake ilikuwepo ndani kuasgiria kwamba yupo ndani.

Maraa baada ya kugonga kama mara tatu akaja kufungua aliponiona mimi akashtuka na kuanza kukasirika kwa nini nimekuja bila kumwambia bada ya kuzozana muda nikamwambia basi nisamehe ngoja nikaweke hawa samaki kwenye friji mara akawa ananigomea nisiingie ndanisindio nikashangaa wewe mimi sindio mkeo mtarajiwa kwanini unigomee kuingia ndani mwangu, akaanza kukasirika kwanini nimerudi bila kumwambia mara ikawa ugomvi kwa uzuri nikamsukuma nikapata upenyo wa kuingia ndani maana alishanipa wasiwasi kwanini hataki niingie.

Ile naingia ndani nakutana na mwanamke kajifunga kanga yangu amekaa sebleni nilichofanya kwa hasira nikambamiza yule msichana ile mbaya mara mchumba wangu kuja akatuamulia akamwambia vaa uondoke huku kanishika yule mwanamke akaondoka kwa uchungu ilinibidi nilie maana mwezi ujao ndio ndoa vikao vimeshafanyika vya maandalizi halafu namfumania mchumba wangu!!!!!!!! nashindwa kumsamhehe na naogopa kuiabisha familia yangu kwa kuwaambia sitaki kuolewa tena kwani zile hela za mchango walishaanza kulipia vitu hii si aibu nishaurini nifanyaje mwenzenu?

Reactions:

8 comments:

 1. Pole sana. Wewe ndo mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu hii kitu mana hapa hata tukisemaje ni sawa na bure tu. Mpaka sasa umeshapata picha ni mwanaume gani ambaye unaye. Kwa uapande wangu nashukuru umemjua mmeo kabla hata ya ndoa kuliko angefanya baada ya ndoa. Kama moyo wako mpaka sasa hivi bado unasita nakushauri usiforce harusi.Michango inaweza kukusanywa na kuwekwa pending, kwa sababu baada ya harusi ni wewe na mumeo mtakaoishi pamajo na si ndugu wala marafiki.

  Si mbaya ukuwaita wazazi wako mkakaa pamoja na kuongea nao mapema kabla hata ya harusi. Mara nyingine inasaidia sana kuwashirikisha watu wa karibu hasa ukiwa na mawazo mengi kichwani mana inakuwa kama relief kwako.Huu ni uamuzi wako na mimi nina uhakika no one will blame you or condemn you for the decision you have made. Hiki ni kipindi kigumu sana kwako na kama wewe ni mcha Mungu sali na kufunga kama inawezekana.Take your time, kwani ndoa haitaji haraka una mda mzuri wa kujipanga.

  ReplyDelete
 2. my dia, kwanza pole sana kwa yaliyokukuta. haya mambo ni makubwa sana. ila kwa hili fanya jinsi roho yako na akili pia vitakavyokutuma, maana this is your life. Muombe Mungu zaidi akupe nguvu na ufikie a nice conclusion. pole

  pls update us kwa uamuzi utakaouchukua

  ReplyDelete
 3. Acha upuuzi wewe dada yaani unamkuta msichana ndani kwa mchumbako tena kapewa kanga yako uivae kisha unampiga? Kwa kosa gani? Yeye si katongozwa tu na kuletwa humo ndani pengine kadanganywa hakuna mtu, wakugombana naye ni hilo gume gume lako lililowashinda mitume!

  ReplyDelete
 4. Nakushauli soma blog ya harusiyangu kunatukio kama lako na bibi aitwae SONIA amemfumania mchumba wake aitwae Danny,wakati wakiwa katika maandalizi ya mwisho ya harusi yao ambayo ilikua ifanyike mwezi huu wa Desemba 2011.Watu wengi sana wamemshauli nawe pia ushauli huo kwakua matukio yanalingana utakusaidia sana Dada.pole sana kwa kutendwa,mungu akutie nguvu ndio majaribu ya dunia.

  ReplyDelete
 5. pole sana dada kwa yalikukuta, mm naomba nikuulize hvi WEWE NI MSAFI AU ULIKUWA MWAMINIFU KWAKE? km jibu ni ndiyo basi go gal jipange uanze maisha mengine ila km nawe ulikuwa unamcheat pasi na yeye kukugundua MSAMEHE MFUNGE NDOA, ni hayo tu.

  ReplyDelete
 6. mi naona bora nusu shari kuliko shari kamili.ukweli huyo mwanaume ni mshenzi na wala hakuthamini.angekua anakuthamini huo ushenzi angeufanya mbali kabsa au asiufanye kbsa lakn sio nyumbni kwake hapo unapoenda wewe, akikuoa hyo si anaweza kukuletea ndani. The ball z ön ur hands, hapa ni ushauri, fikiria ukukibali kuolewa nae je uko tayari kuvumilia such incidences tena? Kama zikijirudia? Au hatujui anaweza badilika akawa mwaminifu yte yawezekana.jst take ur time 2 think possibilities zzte zaweza tokea.usikimbilie kufanya maamuzi sababu ya harusi, harusi si ndoa,ndoa ni nzito, hayo magarama ya harusi ambayo unaona yame2mika huwezi linganisha na uharibifu utakaotokana kama ndoa inakua haina maelewano wala amani.jst take ur time kulichambua hili swala..tumtum

  ReplyDelete
 7. Usiangalie michango inayochangwa ndugu yangu, anangalia Utu wa Mtu, ni Mungu tu aliona akuonyeshee mapema kabla ya ndoa huyo mchumba ulienae ni wa aina gani, fahamu jasiri haachi asili na heri nusu shari kuliko shari kamili nakushauri angalia ustarabu mwingine huyo si sahihi kwako km utaforce tegemea kulia maisha yako yote!! Pole sana

  ReplyDelete
 8. Kama unajijua kuwa wewe ni mwaminifu kapime kwanza ujue afya yako. Then swalimla kujiuliza ukiweka ndoa pembeni ni kwamba je nitaweza kuvumilia katika maisha yangu ya ndoa, maana bora tabia ijitokeze ikiwa hukuijua hapo mwanzo kuliko kugundua ukasema atabadilika. Wanawake kwa wanaume wengi wameteseka katika ndoa zao kwa kuingia kwenye ndoa wakisema wenzi wao watabadilika. Wakati wa kubadilika ni wa uchumba tu! sasa na wewe muda umeisha amini usiamini ukiharakisha kwa sababu ya ndoa utakuja kujutia maamuzi yako. Ahirisha ndoa hiyo na wanakamati watajulishwa nini kinaendelea wapo watakaosamehe michango na hata ukitaka kuolewa tena watajitoa vile vile. Dada yangu chonde chonde kuwa mvumilivu katika kusolve hili swala, usije ukajuta maishani. MAISHA YA NDOA NI MPAKA KIFO SASA CHAGUA KUSUKA AU KUNYOA.

  ReplyDelete