Monday, December 12, 2011

MIUJIZA MUNGU ALIYONITENDEA KWENYE NDOA YANGU..




Dada Rose, nakushukuru kwa kuwa na blog hii ambayo tunajifunza mengi sana kuhusu ndoa unaambiwa kwa kila jambo umshukuru MUNGU.


japo historia yangu ni ndefu lakini na amini kwa atakayeisoma itamfundisha ama kumtia moyo na wengine ambao walikuwa hawamjui MUNGU vizuri basi natumaini watajuwa nini anaweza kumfanyia katika maisha yake na ndoa yake.


Nilizaliwa na kukuzwa katika familia ya kikristu nikiwa msichana wa pili kati ya watatu, baada ya kumaliza masomo yangu nikatamani kweli kuolewa lakini kama wengi wetu katika maamuzi ya ndoa huwa tunatumia akili zetu za kibinadamu na sio za kumuomba MUNGU atutafutie wame na ndio maana wengi tunaangukia matatizo.


Nikapata mwanaume wa kunioa lakini alikuwa muislamu, kitu ambacho mama yangu na ndugu zangu hawakutaka kabisa lakini kwa vile mimi nilikuwa nimeshampenda yule bwana nikawa sisikii wala siambiwi, mipango ya harusi ikafanyika huku mama yangu na ndugu zangu wakiwa na kinyongo moyoni mtoto nikavalishwa shela la kijani nikaolewa na huyo kaka.


Yaliyofwata baada ya ndoa kama nililaaniwa kwanza yule kaka alikuwa anafanya kazi akafukuzwa, na mimi biashara yangu ikawa haiendi vizuri mpaka nikafilisika maana tulikuwa tunatumia hela hamna kinachoingia, nikabeba mimba na kwatabu kwa kuombaomba chakula mpaka nikajifungua watoto mapacha (uupps) nilimshukuru MUNGU lakini nikawa najiuliza tutawatunza vipi hawa watoto.


Hivyo hivyo kwa kubangaiza watoto wakakuwa, mume wangu yeye ikafika sehemu akaona ni bora afe kuliko tuendelee kuishi hivi kwa kuteseka maana ikafika mpaka nikienda kuomba msaada kwa mama yangu mzazi hanisaidii kwakuwa alinikataza nisiolewe na yule kaka sikumsikiliza hata siku moja mama yangu hakuwahi kunisaidia, tunaokoteza yaliyotupwa na kupewa chakula na wasamalia wema mpaka leo wanangu wanamiaka mitano.


miezi mitano iliyopita nikapatwa na balaa ghafla nikiwa chumbani siku moja nikaumwa sana tumbo yani liliniuma kama nilitaka kufa mume wangu hakuwa la kufanya maana hatukuwa na hela mara damu zikaanza kunitoka, na hazikukoma mpaka miezi mitano nikatembea kwa karibia kila mganga ambaye niliambiwa ni mzuri maana hospital kila wakinipima hamna walaoliona basi nikawa nazunguka tu kwa waganga.


Yani damu zilikuwa zinanitoka mpaka kizunguzungu naanguka na kuzimia yani nimepata sana tabu lakini yote haya wakati yanatokea mume wangu na wanagu walikuwa ndio wasaidizi wangu wakuu, basi damu zikawa zinatoka miezi mitano yote kwakweli nilikuwa kwenye hali ngumu sana.


Tulikuwa tunakaa kwenye chumba kimoja tuliuza kila kitu ili nipate tiba, lakini hakuna hata lililotibika, siku moja nikaumwa sana tumbo nilirudi nyumbani nikapiga goti na kusali na kulia hata siku moja sikumbuki kama nilishawahi kusali vile nikamwambia MUNGU kwamba sasa basi nimechoka kuumwa hivi naomba aniponyeshe ni yeye tu ndio tegemeo langu.


Usiku huo jambo moja likanitokea kila ninayemuhadithia haamini lakini MUNGU alinitendea miujiza, nikiwa nimelala tumezima taa chumbani nikasikia naitwa kuamka nikaona mwanga mkali sana akaniambia amka, nikaamka nkajitahidi kumuamsha mume wangu ajionee lakini hakuamka yule mtu akaniambia hawezi kuamka ni wewe tu unahitajika basi nikaamka akaniambia nimesikia kilio chako na leo nimekuja kukuponya ukiniahidi utaacha kwenda kwa waganga nami nikakubali kwasababu niliitaji uponyaji.


Kwakweli yani nilikuwa kama naangalia mchezo wa kuigiza mara akanishika tumbo na baada ya sekunde kama mimbili akaondoka na mwanga ukazimika nikajikuta nimekaa chini nikamuamsha mume wangu ndipo alipoamka nikamwambia jambo moja tu NIMEPONA, hakunielewa ikabidi nimuhadithie kila kitu, ghafla tumbo likaniuma saaaana nikajisikia kwenda haja badala niende chooni sijui nini kikanifanya nichukue ndoo nijisaidie huku tumbo likiwa linauma nikajikamua, nikajikamua mara likatoka linyama kama maini kilo moja na ndani ya tumbo sikusikia tena maumivu.


Tulichofanya ni kupiga magoti na kumshukuru MUNGU kwa miujiza, wakati tunalishangaa likaanza kutingisika sasa nikachukua kisu kuanza kulichoma lile damu MUNGU wangu hatukuamini ndani kulikuwa kumefungwa nyuzi na rasta nyingi sana kwahiyo lile damu lilikuwa limevishwa kwenye ule mpira wa nyuzi na rasta. tukaenda kulitupa chooni wakati tunarudi mara tunasikia mlango unagongwa kufungua akaingia baba mmoja akisema ameoteshwa kwamba aje kunipeleka kanisani. na akanihadithia story nzima iliyonitokea mpaka kupona kwangu ambayo alioteshwa ili akija kwangu nipate kumuamini.


Mimi na mume wangu tukaenda kanisani, tukaongozwa sala ya toba mume wangu kwakuwa alikuwa muislamu akakiri kwamba nataka nimfwate MUNGU wa mke wangu kwani nimeona miujiza aliyotutendea basi tukasalishwa sala ya toba na tukaokoka mpaka leo bado tunaendelea kusali na tumeoana tena ndoa ya kikristu na kwakweli MUNGU ni mwema ndoa yangu sasa inamafanikio kanisani walimuajiri mume wangu na amenipa mshahara wake nimeamnza biashara na tunaendelea vizuri sana.


MUNGU NI MWEMA NA HATAMUACHA YULE AMUITAYE.


Mama Brian



7 comments:

  1. Ameen. Mungu ni mwema na husikia sauti yetu pale tumuombapo hasa tukiwa na imani ya kuwa yeye ndo muweza wa yote.Ubarikiwe wewe na familia yako na kamwe msiache kuomba katika maisha yenu.

    ReplyDelete
  2. loh jamani utukufu kwa Mungu kweli yupo ana atenda kazi zake tukimuita na kumuomba!simameni imara ktkt imani na Mungu atawapigania naomba uwasemehe ndugu zako na mama yako ishi bila kinyongo utabarikiwa zaidi....Angela

    ReplyDelete
  3. ubarikiwe sana dada hakuna linalo mshinda Mungu ukimuamini kwa moyo wako wote kila kitu kwake kinawezekana hongera kwa kumrudia muumba wako maana ulikuwa unapotea kabisa endelea kumshikilia muumba wako sheta asipate nafasi tena juu yako utaona maisha yako yatakavyo badilika nautasahau yoote machungu uliyoyapitia ubarikiwe sana endelea kumwomba Mungu na kumwamini yeye hashindwi na jambo lolote yeye jana leo na kesho jina la bwana libarikiwe sana nimefurahi sana kwa huu ushuhuda uliyoutoa na itakuwa fundisho kwa wengine wenye kuamini nguvu za giza na huku wakisahau ya kuwa kwa yesu ndio mambo yote

    ReplyDelete
  4. duuh, am speechless. all i can say is, Mungu yupo and mind u HE IS ALWAYS BIZ FOR OUR LIFES, JESUS IS ABLE.

    ReplyDelete
  5. Ushahidi mzuri na wenye kutia moyo.

    Nilikuwa napita hapa kusema kwamba sasa nimerudi tena rasmi. Tupo pamoja !!!

    http://matondo.blogspot.com/2011/12/wanablogu-wenzangu-na-wapenzi-wote-wa.html

    ReplyDelete
  6. Amen mpendwa wote tunamiujiza ila watu hawapendi kuongea mungu akutie nguvu pia sala sala sala usiache amen

    ReplyDelete