Tuesday, December 6, 2011

Dada Rose,

natumaini u mzima yani mimi kwakweli ninakasheshe kwenye ndoa yangu mapaka nasikia kuchanganyikiwa, mume wangu amekuwa mlevi sana halafu kazi hafanyi anategemea kula hela ninazofanya mimi biashara ambazo hazitutoshi maana mpaka watoto na walipia mimi ada, yeye kazi yake kwenda kukaa tu vijiweni na marafiki zake, akija nyumbani amelewa usiku wa manane hajui hata kugonga kwa ustaarabu yani akigonga mara mbili hujamfungulia anaingia na mlango yani kila siku sisi kwetu tunakazi ya kutengezeza milango mpaka aibu kwa majirani. nikimwambia atafute hata kibarua ananitukana na kuniambia kama siwezi kuwa mke wake niondoke. nimeamua kuondoka na kuanza maisha yangu mwenyewe napata tabu lakini najuwa siku yatanyooka.kuliko kuishi kwenye ndoa iliyo na makaraha.

3 comments:

  1. Nakuunga mkono 100 kwa 100. Huyo mwanamme hakufai. Ni bora uamuzi ulio fikia. We fanya biashara, lisha na somesha watoto wako. Mungu yupo anaelewa na atakujalia tu utapata mwingine zaidi yake huyo.

    ReplyDelete
  2. Pole mdogo wangu pia nami nakuunga mkno ungekuwa umetoka sababu ya kurubuniwa na mwanaume ningesema hutofanikiwa lakini kaanza yeye wewe piga kazi mungu atakusaidia

    ReplyDelete
  3. Mamii Piga mzigo kwa kwenda mbele..kama ni biashara fanya, kama ni kazi fanya ilimradi watoto wako hawalali njaa. Watoto wasome wale na wavae vizuri mana hiyo ni haki yako. Huyo mwenzio siku akili ikimwingia kichwani na kujua ini maana ya maisha hasa ukiwa na familia atajua pa kukupata. Mwache apunge upepo

    ReplyDelete