Tuesday, November 15, 2011

NATUMAINI HILI HULITENDEA KAZI..


Raha ya mzunguko uwanja uwe msafi jamani nani anataka kucheza kwenye uwanja wenye majani mchezo utachezeka kweli maana utakuta pengine majani yanaota mpaka golini huoni unapata tabu mara huku, mara kule mpaka usogeze majani uchungulie ulione goli ndio upige mpira mmmmhhh jamani hata hamu ya kucheza tena utakuwa nayo!!!

Mume ni jukumu lako kuhakikisha uwanja upo safi mara zote najuwa wanaume wengi husema raha ya uwanja wao uwe na majani kidogo hawataki kukata sana utakuwa kama wa mwanamke wao hutaka majani majani yabaki kidogo basi hata kama ndio hivyo siyo ujisahau hayo majani majani yakaja kuwa msitu.

Lakini pia ni jukumu la mke kuhakikisha uwanja wake na wamumewe upo kwenye usafi ni jukumu lako mama hata mara mbili kwa mwezi weekend ambayo mpo nyumbani mlaze mumeo kitandane mpe raha ya kumsafishia uwanja wake, nani anataka kumuona mume wake anatembea kama sokwe barabarani ukimuona nje mtanashati ukimvua suruali ghafla unaweza zimia, mmmhhh haipendezi.

Sio uwanjani tu hata ndevu pia, unajuwa mumeo anapendeza akiwa na ndevu za kiasi gani basi mweleze akakate kama unajuwa basi msaidie na kama hujui usijaribu kisa cha kumtia kovu mtoto wa mwanamke mwenzio nini, makwapani pia maana wanaume wengi sana ni wavivu sana kukata hizi za makwapa yani akisema akupe hi kama amevaa vest utashanga halafu vile hubeba jasho sana na kukufanya unuke jasho, mara nyengine hata ujitengeneza viuchafu vyeupevyeupe, utamkuta mwanamke anavaa nguo kata mikono makwapa hajanyoa jamani hata ukiambia cheers kupifa vizuri huwezi unaona noma haipendezi unatakiwa siku zote uwe mtanashati na msafi sio kumpa mwenzio mtihani wakati anataka kujipa raha inahusu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment