Wednesday, November 16, 2011

MASIKINI SHEMEJI YANGU..

Dada Rose,

Hongera kwa blog yako nzuri na yenye kuelimisha, dada leo nimeamua kuleta mada hii inayomuhusu dada yangu wa tumbo moja japo ni ndugu yangu kwakweli anavyomfanyia mumewe mimi sipendi na kwetu wameshamuonya lakini hata kusikia hataki.

Dada yangu ameolewa miaka mitatu iliyopita kama ndoa nyengine zilivyona mikwaruzo hata yao pia ilikuwa hivyo na dada yangu akaamua kuwa na mwanaume nje ya ndoa, kwasababu yeye ni mtu mzima hakuna aliyemsema kwa kuchukuwa jukumu hilo, mume wa dada yangu ni dereva mara nyingi huwa anasafiri na hukaa huko hata wiki mara nyengine mpaka wikimbili.

Shemeji anapokuwa hayupo dada ndio hupata mwanya mzuri wa kujivinjari na huyo kimada wake na hufanya wazi bila kuogopa, kinachonisikitisha sasa hivi mumewe amesafiri amediriki kumpeleka yule mwanaume mpaka kwake yani analala naye kwenye chumba cha mumewe bila aibu wa kuogopa.

Hii tabia mimi naohopa shemeji akija kujuwa si atamuua dada yangu, nikimkanya dada ananijibu ndoa yake inanihusu nini, mumewe si anajifanya kidume ngoja nimuonyeshe kama kuna mwanaume zaidi yake.

Dada yangu amepotea sijui amechanganyikiwa, hata simuelewi.

Reactions:

2 comments:

  1. Mimi ni mwanaume. Nakushauri ukae pembeni, kila lenye mwanzo lina mwisho. Anaona kama anamkomoa kumbe anajikomoa mwenyewe, anamkomoa vipi mumewe wakati mumewe hajui? Siku akifumaniwa na akitimuliwa kisha huyo mwanaume wake akamkataa atapata akili.
    Viache ndugu yangu

    ReplyDelete
  2. Hell has no fury than a woman scorned. wanaume wanafanya haya kila kukicha binafsi yamenikuta, na nikasamehe. akifanya mwanamke dunia inakwisha why...tit for tat

    ReplyDelete