Thursday, November 24, 2011

Dada Rose na wenzangu wote natumaini ni wazima leo nami naleta mada kwenye blog yetu hii nikitaka kusaidiwa mimi ni mwanaume na nimeoa, bahati mbaya baada ya kuoa wazazi wa mke wangu wote wakafariki akimuacha mke wangu na ndugu zake wa kike wawili ambao hawana kazi wa shule tegemeo lao ilikuwa mama yao na mke wangu dada yao.

Baada ya mama yao kufariki mke wangu akaniomba kama ndugu zake wangeweza kukaa nasi maana walikuwa hawana msaada nikakubali lakini baada ya muda hawa ndugu wa mke wangu naona wananifanyia mambo nisiyoelewa vituko kutwa haviishi ndani.

Ndugu yake mmoja amepata bwana basi yeye kutwa kwa huyo mwanaume hata na kurudi saa sita za usiku hata mimi mwenye nyumba nimeshalala na imetokea mara kwa mara nikimwambia mke wangu amkanye mdogo wake ananiambia kwanini ninawivu na mdogo wake ama namtaka mdogo wake? yani anakuwa mkali kabisa na wala hamwambii mdogo wake, huyu ndugu yake mwengine yeye ni mchafu sana, yani mpaka ananuka anaweza kukaa hata siku nne hajaoga tena akiwa kwenye hedhi ndio balaa ndani hapakaliki juzi kaniacha hoi baada ya kujisaidia haja kubwa kwenye ndoo ya jikoni na kuyaacha ndani.

Vituko vyao nimechoka sasa, nikimwambia mke wangu anasema nataka kuwafukuza wakati najuwa hawana pa kwenda, na inakuwa ugomvi kubwa sana na mke wangu mpaka nashindwa kuelewa ndugu zangu nifanye nini mwenzenu.

Reactions:

4 comments:

 1. Mhhhh wonders shall never end... I find it hard to believe..umesema kabla ya ndugu wa mke wako kuja nyumbani walikuwa wanaishi na wazazi wao, lakini wazazi kwa bahati mbaya wakafariki, sasa je kwa nini wasiendelee kukaa kwenye hiyo nyumba ya wazazi wao.Kama ni hela matumizi unaweza watumia huko huko maana sioni sababu ya watu kukufanya usiwe na amani wakati upo nyumbani kwako. Kama inawezekana embu jaribu fanya kikao cha familia pamoja na hao ndugu wa mke wako na uwaeleze ni nini hasa unaexpect kutoka kwao. Ukiwa kama baba mwenye nyumba unasauti ya kuamua nini kifanyike hasa katika nyumba yako. Yale yasio mazuri machoni mwako ni vizuri ukayaweka wazi mapema ili watu wakuelewe na yeyote atakayeshindwa kutekeleza basi atafute nyumba yake. Mana katika kila nyumba huwa kuna sheria na watu ni lazima wazifuate.
  Yaani sijui nimuweke mke wako kwenye category ipi ila naoa kama atashindwa kukuelewa mara hii itabidi upate msaada wa ndugu au hata wa kiroho(dini). Pole sana

  ReplyDelete
 2. Mpe likizo mkeo na ndugu zako wakajifunze adabu ya kuishi na watu, inaonekana hao watoto walishashindikana, wazazi wao waliwashindwa na hawataweza kukaa na mtu yeyote kwa tabia zao chafu.

  Je wazazi wao waliwaachia mahali pa kukaa au nyumba? Kama waliachiwa basi wakakae kwao muwe munawasaidia matumizi, kama hawajaachiwa na bado wanasoma waende shule za boarding, ama sivyo wapangie chumba Tandale uwanja wa fisi au kwa Mtogole wakafanye mambo yao huko, maana kama una watoto wadogo ni hatari sana wanaweza kuiga tabia mbaya za mauntie zao. Na huyo mkeo nae ni wa ajabu sana, hivi huyo anayefanya umalaya akianza kuugua maradhi ya kisasa au akipata mimba si ndio itakuwa mzigo mwingine tena ndani ya nyumba? As a man unahitaji kuwa very strong na wewe ni kichwa cha chumba usiache shingo ikawa inakupelekesha kama feni.

  Subira

  ReplyDelete
 3. MWAMBIE AONDOKE NA NDUGU ZAKE, MANA ISIWE TABU NDOA ULIFUNGA NA YEYE HUKUFUNGA NA UKOO MZIMA, AAAAH KWANINI UKOSE AMANI KWAKO KWA SABABU YA WDOGO WA MKEO? MPE MPE HUYO KAMA VIPI ASEPE NAO HAO NDUGU ZAKE,

  ReplyDelete
 4. bila shaka huyo anaejisaidia kwenye ndoo ni mgonjwa otherwise wewe kama baba wa nyumba unatakiwa kuwa na msimamo kuwaita mbele ya dada yao nakuwakanya. wao wanatakiwa kujua kwamba hapo wako kwa dada yao chini yako yakizidi sana tafuta hata ndugu zao wakubwa kama wajomba waupande wao uelezee hali halisi kuliko kukaa tu kimya wakati unaona hata mkeo hachukui hatua mana kama ameshatamka kauli yakuwataka yasije yakawa mengine badae.

  ReplyDelete