Monday, October 17, 2011

YA CHUMBANI YALINIPONZA NI.....Dada Rose,


japo najionea aibu kukuandikia hili lakini najuwa kwa kutuma hapo nitapata msaada mkubwa sana maana yaliyonikuta ni makubwa sana.


kipindi cha usichana kwangu kutoa mimba ilikuwa kitu kidogo sana, sijisifii lakini kwa aibu nataka nieleze ukweli nilishatoa mimba tano, maana kila nitakaye kuwa naye nikimueleza nina mimba hataki kuelewa inabidi nitoe hayo ni matokeo ya kuwa na wanaume watatu nikatoa mimba tano, najuwa wengi watauliza kwanini kila mwanaume nilikuwa najisahau na kurudia kosa, hilo sio jambo nalifurahia ila ilitokea tu labda sikujuwa madhara yake baadae ni yapi lakini sasa natambua.


nimepata mwanaume wa kunioa, amenioa na tunaishi maisha mazuri tu ya kupendana sana,na ninamshukuru MUNGU ya kwamba nilibahatika miezi kadhaa baada ya kuoana kubeba mimba, lakini jamani mimba imekuwa fimbo yangu ninayochapiwa makosa yangu ya nyuma.


yani sikai kwa raha naumwa kila siku huu ni mwezi wa tatu sasa kutwa nashinda hospital na kunywa madawa, yani sina raha ya kubeba mimba, siku moja doctor akaja na kuniambia kwamba nakuwa hivi kwasababu kizazi changu kipo wazi kwasababu ya kutoa sana mimba!!!!!!


natakiwa kuwekwa bedrest mpaka miezi tisa, jamani napata tabu leo naandika humu pia kutoa ushauri kwa wasichana wenzangu, tusiponzeke kwa maneno matamu tunayopewa kutufanya kulala bila condom na kutoa mimba baadae ni kashese kubwa sana.


muda wote nipo hospital mara nyengine najisikia nafuu naweza kufanya vitu kama kawaida hata kunyoosha miguu lakini mara nyengine naumwa karibia ya kukata roho, daktari nilimuomba asimwambie mume wangu maana najuwa ataniona mimi vipi????? yani namuonea huruma sana anavyohangaika kunitunza.


sasa najiuliza mpaka miezi tisa nitaficha huu ukweli???? ama nimwambie tu mume wangu ukweli maana mama yake anakuja kunilea hospital sianaweza kugundua ukweli?? nifanyaje mwenzenu, najua nimekosa sana lakini nawaomba mnishauri.

Reactions:

7 comments:

 1. pole dada na matatizo yaliyokukuta kosa ulifanya lakini wewe tubu kwa muumba wako akusamehe hayo ni manbo ya ujana na afya ulipima kweli maana ulikuwa hutumii mpira sasa mimi kwa upande wangu nakushauri usimwambie mtu maana hata ukimwambia haitasaidia kitu sanasana itakuletea matatizo zaidi kama ulisha mwonya doctor asiseme sasa unatakumwambia mama mkwe aumume wako ya nini na hawa hata dawaw ya kukutibia wewe kaa kimya tu huku ukimwomba mungu akuwezeshe ujifungue salama

  ReplyDelete
 2. pole sasa dada, kweli yameshatokea na waswahili wanasema majuto ni mjukuu kikubwa ni kukabiliana na hali ya sasa.
  Sijui mume wako yukoje lakini kwa mtazamo wangu naona usimwambie ila hakikisha hajui; iwapo utamwambia pia hakikisha atatawala hisia zake na kukuelewa mkaishi kama zamani.Daktari wako hakikisha hakusaliti kwa namna yeyote ile.
  Huo ni mtazamo wangu tu, mwamuzi wa mwisho ni wewe mwenyewe.
  pole sana; tatizo la utoaji mimba kwa sasa ni kubwa mmno kuwa msaada kwa wengine kupunguza tatizo hili.

  ReplyDelete
 3. pole, nibora umetoa ushuhuda huu ili iwe fundisho kwa wengine. Wanawake tujifunze kuzuia, siyo kutoa. Mbona njia za uzazi wa mpango ni nyingi na zipo ambazo ni salama zaidi. Bedrest siyo mchezo. Ila vumilia, watoto ni faraja sana katika ndoa.

  ReplyDelete
 4. wewe sali muombe mungu na shukuru mungu hata umepata huyo wenzio hawana kabisa nausimwambie baba wa watu utamtoa amani na wewe

  ReplyDelete
 5. Naumie mateso ya mume wako kutokana na upumbavu wako wa zamani. Sipati picha ukimwambia itakuwaje!. Ila kaa ukijuwa, penye uwongo, ukweli hujitenga na kukaa kando. Ipo siku atajuwa

  ReplyDelete
 6. mimi nakushauri umweleze ukweli kumbuka yeye ni mtu mzima pia anajiuliza maswali.kwa hiyo jenga msingi imara kuanzia sasa, kukosea kupo duniani na usiwe mnafiki kwa mtu unayeishi naye kila siku.
  Mungu Anaona.

  ReplyDelete
 7. Pole sana dada,me ushauri wangu ni kama ifuatavyo maana mimi pia ni daktari na ni mwanamke
  Kupewa bed rest sio lazima uwe umetoa mimba nyingi zamani,kuna sababu nyingi za kufanya cervix isifunge na pia kuna matatizo ya hormones yanaweza sababisha,kwaa maana hiyo mumeo na mama mkwe si lazima wajue sababu halisi ya wewe kuwa na bed rest
  Mimi binafsi sijawahi toa mimba hata moja ila kwa sasa nina uja uzito wa miezi mitatu kama wewe na hadi sasa nipo bed rest naanza kazi kesho
  Sababu kubwa ya bed rest yangu ni hormone imbalance
  Ukitoa tu siri kwa mumeo atakuona malaya maisha yenu yote,na daktari hawezi kumwambia mumeo sababu atakuwa amekiuka patient confidentiality na unaweza kumshitaki
  Pole sana dear

  ReplyDelete