Friday, September 2, 2011

MWENZETU LIMEMKUTA, TAMAA ZIMEMPONZA

kijana mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na mbili amejikuta akishangaza familia yake wakiwemo wazazi wake baada ya........

huyu kijana mtu wa bukoba alikuwa anasoma kwenye shule moja hukohuko, sasa kipindi yupo shuleni akatokea kudondokea penzi la mwalimu mkuu wa shule aliyokuwa anasoma, kwa kuhadithiwa huyu mama alimtongoza kijana naye akisitasita mara siku akamkubalia na kuwa wapenzi.

jambo hilo lilikuwa la siri sana mpaka kijana akamaliza secondary na baada ya kufanya mtihani wa kidato cha nne kijana huyu akafeli wazazi wake wakamshauri kurudia tena mitihani na kujikuta kufeli mara tatu mfululizo.

kwakuwa wazazi wa huyu kijana walikuwa wanajiweza ikabidi wampeleke Dar es Salaam kwa ndugu zake huko ndipo akawa anajifunza mambo ya kupiga picha akawa anajulikana sana kwa kazi hiyo akawa anakodishwa kwenye masherehe mara kwa mara yani kwa kweli maisha yakaanza kumnyookea.

akiwa Dar es Salaam alikuwa akiishi kwa shangazi yake, huku bado akiwa anawasiliana na yule mwalimu mkuu kwani si alikuwa ni mpenzi wake, baada ya mwaka yule mwalimu mkuu akaja Dar kumtembelea kijana akalala kwenye hoteli moja maarufu sana hapa jijini yule kijana akawa anaenda mule kuenjoy na mpenzi wake.

baada ya kukaa wiki yule mama akatakiwa kurudi bukoba kuendelea na kazi zake ndipo alipomshauri yule kijana ya kwamba arudi naye bukoba atamfungulia huko frame ya kufanyia kazi zake na nyumba ya kukaa, kijana akamkubalia mpenzi wake baada ya miezi miwili mama akatuma tiketi ya ndege kijana taratibu na majigambo akakwea pipa kurudi bukoba.

ni kweli akapewa kila kitu kama yule mama alivyomuahidi,na maisha yakawa ya raha kwao na yule kijana akamtambulisha yule mama kwa wazazi wake kama mwanamke aliyeamua kumsaidia kutoka maishani, wale wazazi wa kijana wakamshukuru sana yule mama na kumkaribisha nyumbani mwao wakati wowote akipenda kuwatembelea, yule mama akawa anamwaga misahada sana pale nyumbani na kuwapa wale wazee hela tele mara kwa mara, bila wao kujuwa kama yule ndiye anayemla mtoto wao.

kijana akanogewa na penzi la mama akaamua sasa kumoa, japo yule mama alishaolewa mwanzo na kuzaa mtoto mmoja (ambaye alishaolewa na kuzaa watoto watatu) hakujionea tabu kuolewa tena na huyu serengeti boy wake, akakubali na kuanza kuandaa harusi kwani alitaka kuianda yeye mwenyewe, yule kijana akaenda kuwaeleza wazazi kwamba anataka kuoa na wazazi wakamkubalia na kumpa baraka zote na kumuomba amlete huyo binti aliyempata wa kumuoa ili familia zao zifahamiane.

alipomleta yule mama kwamba ndiye anayetaka kumoa yula baba akadondoka hapohapo na mpaka leo kama amechanganyikiwa, haongei amekuwa kama zezeta kwa ule mshtuko, mama yake hakupata mshtuko wa kumdhuru bali tu alikataa mwanaye kumuoa yule mama mtoto hakusikia la wazee na wala hakumuonea huruma baba yake kwa ghali iliyomkuta ghafla na kuendelea na mipango ya kumuoa yule mama.

wiki mbili kabla ya harusi yule mama aliumwa sana kupelekwa hospital akagundulika ana ukimwi na malaria kali iliyomsababisha kulazwa, baada ya siku mbili akazidiwa sana na hatimaye kufariki, kijana yule baada ya kusikia hayo akadondoka kwa presha naye kulazwa lakini kesho yake akatolewa hospital, baada ya siku mbili yule mama akazidiwa sana na hatimaye kufariki.

kijana akabaki na ugonjwa wa ukimwi, baba yake aliyedhohofika kwa sababu yake, na kinyongo cha mama yake, hana la kufanya kila siku anawalilia wazazi wake wamsamehe.

TAMAA MBAYA, kheri uishi maisha ya marefu lakini ya tabu kuliko maisha mafupi lakini ya raha.



4 comments:

  1. dada rose napenda sana kutembelea blog yako lakini hii rangi ya blog yako dada yangu inauwa macho sana pls badilisha hii rangi kisa hichi nimekipenda na pia fundisho kwa wengine wenye tabia kama huyu nimeisoma hii kisa lakini kwa shida sana hii rangi unaumiza sana macho

    ReplyDelete
  2. asante dada rosemary kwakusikiliza ushauri wa mafans zako asante kwakusikia ushauri wa kubadilisha ile rangi maana ilikuwa hatari sana kwa macho ubarikiwe dada tunaomba uwe unatuwekea viza vingivingi tu mimi ni mpenzi wa blog yako sana kazi njema

    ReplyDelete
  3. vijana wa siku hizi ndo walivyo.wanapenda sana kulelewa..sasa kwa wale wamama wanaoweza kazi hiyo always nao huwazawadia mengi zaidi hao wapenda kulelewa a.k.a serengeti boys....sasa nani wa kulaumiwa? nadhani mwanaume kama mwanaume naturally ni mtu ambae ameumbwa na siku zote anakuwa regarded kama bread earner, kichwa cha familia, nk hasa kwetu sisi huku africa. sasa globalization and gender equalities zinatumiwa vibaya kiasi kwamba inafikia wakati watu kwa udhaifu wao wana taka switch position....na ndo hapo kuna wakati is not necessary serengeti boys vs sugar mama...ila pia mdada anakuwa na mtu tena wa rika yake but upuuzi wanaosema hao vijana wa kisasa ni kwamba wao wanatafutwa hivyo swala zima la mahusiano mwanamke lazima amhudumie mwanaume ili aweze kuwa naye...jamani what a rubish! hivi tunafika? basi aprovide na umheshimu hakuna matangazo mtaani...simu sipigi mimi yeye ndo apige...au la amwekee airtime ktk simu....na utasikia anaweka loud speaker washkaji wamsikie dada wa watu anvyoongea naye..mana kijana kishajisifia yeye anapendwa, anahangaikiwa hana time so wasikie mdada anaulizia u hali gani...uko wapi and all that stuff! nampa pole sana huyu kaka lakini katika jamii wapo wengi mno...hope watajifunza kupitia kisa hiki...na wajue always cheap is expensive

    ReplyDelete