Tuesday, September 20, 2011

MWANAUME, MUME, BABA NI NINI....

wanaume mtanisamehe maana najua blog hii mengi sana yamezungumzwa kuhusu wanaume, lakini jueni kilio kikuu dunia nzima katika familia husababishwa na wanaume na ndio mimi kama mwanamke pia huwa hodari sana kuweka visa kama cha huyu dada...

Rosemary,

yani sijui nicheke tena hapa na nyie maana mimi nimeshacheka mpaka mbavu zinaniuma, yani jamani kweli kuna jambo linanishangaza sana, nimeolewa miaka mitano iliyopita na kwakweli kijana huyu alinivutia sana na mwanzo wa uchumba mpaka kuoana tulikuwa vizuri tu na mapenzi tele yani mpaka nikawa na shangaa huyu mwanaume mbona sikumpata siku nyingi.

baada ya mwaka na nusu tukaoana, na ndoa yetu ikawa ya furaha sana mpaka watu nje wanatushangaa japo kindani matatizo yapo lakini tulikuwa tunajitahisi kuyatatua, miaka mitano sasa huyu mwanaume ndio ameanza tabia ya kunishangaza mpaka nashangaa kabisa.

jamani huyu mwanaume anavitabia ambavyo sijawahi kuona mwanaume yeyote akiwa navyo, kabla ya kuolewa na yeye nimeshapita kwa wanaume wengine, lakini huyu kanishangaza, hata washauri wetu wa ndoa na rafiki zake pia wanashangaa tabia za huyu mwanaume.

kwanza anapenda kususa, yani yeye anataka muda wote anachokitaka yeye ndio ufanye yani hatakama wewe hamu ya penzi huna yeye akitaka tu umpe tena hamna kubembelezana anakulazimisha yani nahisi kwenye ndoa yangu nimeshabakwa na mume wangu mwenyewe maana mpaka kubinyana, kukabana yani baada ya hapo mwili wote unauma, jamani!!!!!!halafu akimaliza anaanza kukususia kwanini hutaki kumpa penzi mara ukimtengea chakula hali, anaaanza kurudi usiku mzito yani vituko kibao.

pili kila binadamu natambua hukosea na unaposahihishwa basi ni vizuri kukubali kama umekosa lakini mwenzangu huyu ukimwambia hivi umekosea na kumshauri basi ananuna hata ukimpigia simu hapokei hata upige mara ngapi, siku mtoto akawa anaumwa hajarudi mpaka saa sita nampigia hapokei simu zaidi ya mara kumi ikabidi nimpeleke mtoto kwa daladala (nashukuru weli daladala zipo mpaka usiku) kweli huyu mzima?

sitaki kufurahisha majirani na watoto wajue tumegombana, maana hizi nyumba za kupanga nazo, basi akirudi nikimsalimia anachukua dakika tano nzima mpaka nijibiwe, yani kama hataki salamu yangu.

 MUNGU amemjalia kuwa na gari na hilo gari japo sijatoa thumni yangu lakini  nilimsaidia wazo kubwa sana mpaka leo akawa nalo sitaki kuliweka hadharani lakini lilimsaidia sana, mara tukigombana anasusa nisilipande alikuwa ananipeleka kazini asubuhi mara sikuhizi analala mpaka saa mbili ili tu asinipeleke nami kwa vile mtoto wa mkulia na daladala zimejaa basi mpaka makonda wamekuwa mabesty. amejisahaulisha kabisa mchango wangu kwenye kupata hilo gari.

mara mbili ameshapigwa msuto wa kiume sijui mnaujuwa ile jamaa kaongea kitu halafu ni cha umbea halafu rafiki zake wa kiume wanamuweka chini na kumuelezea sio vizuri nini, nadhani mtaelewa (lakini japo rafiki zake walinieleza nikauchuna tu wala yeye sikumwambia sikutaka aone aibu mkewe nimejuwa).

watoto wake hataki hata kutoa hela ya kuwanunulia nguo, kabla ya kugombana tuliamua kuwafungulia account na tuwawekee kiasi fulani kila mwezi miye natimiza kila mara lakini yeye nikimuuliza anasema hataki (kweli ugomvi wetu watoto unawahusu nini) yani kama sio wake vile.

yani huyu mwanaume anamambo ambayo simuelewi hayo mambo mara nyingi hufanywa na wanamwake sijawahi kuona mwanaume akifanya vitu hivyo mpaka nashangaa usikute namtegemea na juwa ni mwanaume kumbe mwenzangu, nashindwa kumuelewa kabisa, kununa na kususasusa ovyo kama mtoto wa kike huyu vipi.mpaka nimewahadithia rafiki zake wanamshangaa.

SUZANA   M.

Reactions:

3 comments:

 1. pole sana. wanaume wa hivyo wapo tena wengi, hasa wa IRINGA na mwisho wa hiyo ndoa MTAACHANA TU. hapo ni mwanzo atazidisha vituko hadi utaomba talaka bila kupenda. By Mama N

  ReplyDelete
 2. sio wa iringa tu wapo hivyo hata wa kanda ya ziwa, yani tena nasikia hawa ndio haswaa kwa kuoa na kuacha, sijui wanamatatizo gani, lengine naona mwanaume akishaoa anajisahau na kujiamini kwamba yeye ni wa pekee hata akikufanyia vituko gani bado utampenda tu, hawajui hayo yalikuwa zamani sio sikuhizi, dunia imebadilika.
  fanya jitihada katika ndoa yako haswa kwa vile unawatoto endelea kumvumilia huku ukitafuta pumziko pembeni ili mlee watoto, lakini ukiona matatizo yamezidi heri muachane kuliko kuteseka.

  ReplyDelete
 3. Kila pahala wanaume wa aina hiyo wapo. Mtu anaekushauri kutoka nje ya ndoa hana Tofauti na MUUAJI, anayekuua huku anakuonea huruma! Take care, dawa ya tatizo ni kutatua. Pia ningependa niwape neno ambalo watu mumesahau, JAMANI NDOA NI UVUMILIVU, KILA MTU ANA MAPUNGUFU YAKE. Nakuomba sana dadangu, uvumilie mapungufu ya mumeo, hata wewe una mapungufu. No one is perfect under the sun baby.Kila pahala wanaume wa aina hiyo wapo. Mtu anaekushauri kutoka nje ya ndoa hana Tofauti na MUUAJI, anayekuua huku anakuonea huruma! Take care, dawa ya tatizo ni kutatua. Pia ningependa niwape neno ambalo watu mumesahau, JAMANI NDOA NI UVUMILIVU, KILA MTU ANA MAPUNGUFU YAKE. Nakuomba sana dadangu, uvumilie mapungufu ya mumeo, hata wewe una mapungufu. No one is perfect under the sun baby.

  ReplyDelete