Monday, August 1, 2011

IKIFIKA MIEZI SITA TU INATOKA...

kuna dada mmoja nimekutana naye juzi yeye katika maongezi alikuwa anahuzunika ya kwamba japo anafurahia kuolewa ni mwaka wa tano sasa lakini hajabahatika kupata mtoto, na sio kwamba hazai ama mumewe hashughuliki hapana tatizo ni kwamba anapata mimba lakini ikifika miezi sita inatoka..


anasema ameshamaliza dawa zote za kienyeji alizopewa na mama mkwe mimba tatu zimetoka kila ikifika miezi sita anasema mpaka anaogopa tena kubeba mimba nyengine maana anaona mambo yatakuwa tu yale yale, ndugu wa mume wanamshauri mume wake kwenda kuzaa nje maana muda unaenda kwakweli kwajinsi alivyonisimulia nilimuona na uchungu sana..


hajui tatizo hili kwanini linampata yeye maana ndugu zake wa kike hawajawahi kupwa na tatizo kama hili na wanawatoto, anahisi labda amelogwa ama kisayansi zaidi hili ni tatizo???

Reactions:

2 comments:

  1. aende mico sinza palestina kn hosp. inaitwa micoupande wa msikiti amuulizie dr. nkumbi she wont regret ni maspecialist wa ukweli.pia azid kumuomba mungu!

    ReplyDelete
  2. pole sana sikiliza mwambie aende muhimbili fest track amuone dr kamugisha mimi kuna dada nafanya nae kazi alikuwa hivyo yeye zimeharibika mbili baada ya kumuagizia akaenda na sasa ana ujauzito wa miezi nane anaendelea vizuri asijali atapata mtoto no ya dr ni 0754382072

    ReplyDelete