Monday, July 18, 2011

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME SABABU NI NINI?

Wadau..

Dada Rose,

Asante kwa makala zako za uelimishaji...mimi kunajambo hili la upungufu wa nguvu za kiume linanishangaza sana, mwanzo nilikuwa nasikia likiwa kwa wazee lakini hivi sasa waathirika wakubwa ni vijana. Labda nini sababu zake?

James

Reactions:

3 comments:

 1. SIKU HIZI HILI LIMEKUWA TATIZO KUBWA HASWA KWA VIJANA KWA SABABU YA VYAKULA VINAVYOLIWA WATU WANAENDEKEZA SANA VYAKULA VYA MAFUTA KAMA KITIMOTO, CHIPS NA MAZAGAZAGA MENGI.

  UKIACHANA NA CHAKULA ULEVI PIA NI CHANZO KIKUBWA KINACHOSABABISHA HAYO MATATIZO HASWA UNAVYOLEWA SANA UNASHINDWA KUFANYA TENDO LILE NDIPO INAKUWA TABIA NA MWISHOE HATA UKIJARIBU KULIFANYA UNAPIGA MOJA TU HALAFU BASI HUWEZI TENA KUENDELEA.

  ReplyDelete
 2. Dada Rose;

  Nakubaliana na mdau hapo juu. Maisha haya ya deko tunayoyaparamia yana madhara mengi sana yakiwemo kansa n.k.

  Kukosa nguvu za kiume pia kunaweza kusababishwa na matatizo ya kisaikolojia tu - kutojiamini, kuwa na msongo wa akili au matukio yasiyopendeza yaliyojikita akilini. Na nyie wanawake wakati mwingine mnakuwa wakatili. Ukimwambia mwanaume kwamba ana maumbile madogo (aka kibamia) basi unakuwa umemvuruga kabisa kisaikolojia na anakuwa hajiamini tena.

  Pia inaweza kuwa ni dalili tu ya matatizo makubwa zaidi na hata magonjwa ya moyo. Tazama utafiti huu hapa chini:

  http://matondo.blogspot.com/2010/03/utafiti-upungufu-wa-nguvu-za-kiume.html

  ReplyDelete
 3. Cha hajabu ni kuwa nguvu zimepungua lakini uzinzi unaongezeka. Ndio maana ukiwa na mume mzinzi kumshtukia ni ndani ya mwezi maana hana nguvu za kuridhisha wanawake wawili uta notice tu!

  ReplyDelete