wenzangu ninatatizo moja kubwa sana mimi ni msichana mzuri na mrembo nadhani kwa hayo na yatambua sana na ukiachana na hayo nimeambiwa pia ninavutia, ila tatizo langu mimi kubwa ni kwamba wanaume wangu wote ambao hunitaka kimapenzi mimi huwa ni wame za watu tokea nimeanza kumjuwa mwanaume kimapenzi hata siku moja sijapata mwanaume ambaye hajaoa...
na hili kwangu kwa mara ya kwanza nilikuwa sina tatizo nalo lakini sasa umri unaenda nataka na mimi niolewe na hawa wanaume za watu hamna anayetaka kuoa mke wa pili na wala nisinge penda kuolewa mke wapili nataka mwanaume wangu wa kumiliki peke yangu..
nimechoka kuwa na wame za watu kwani utakuta wakati mwengine haswa wa usiku natamani kweli ngekuwa nimelala na mpenzi wangu lakini haiwezekani kwani anakuwa nyumbani kwake, wakati mwengine nataka kutumia muda mwingi kukaa na mpenzi wangu lakini yeye hawezi kwani inabidi aende nyumbani kwake muda mwingi ninaokaa na mume wa mtu ni masaa matano nikibahatika kukaa naye siku nzima labda kama mke wake kasafiri ama wamegombana...
marafiki zangu huniambia hii labda ni laana kwasababu mwanaume wangu wa kwanza kunipa penzi alikuwa mume wa mtu, ndio maana huwa nawapendeza sana wame za watu, kwakweli sielewi ama hili ni jini?
Dada,
ReplyDeletePiga magoti kwa imani ya dini yako utubu dhambi zako. Maana hata kwenye amri za Mungu kakataza kabisa kutamani mali/mume/mke wa mtu mwingine. Ni kweli kbs kama wanavyokwambia wenzako kuwa inawezakana ni laana. Dada hakuna kitu kibaya kama hiyo tabia uliyofanya. Maana usipoangalia hata wewe ukija kuwa na huyo mwanaume wako unayemtaka na yeye atakuwa na mwanamke mwingine, ivi utajisikiaje? Utamlaumu? Piga magoti dada, omba msamaha kwa Mungu mwenzangu, na usirudie tena hiyo tabia. Na hata huyo mwanaume wako unayemtaka ukimpata basi umuombee pia ili asije kuwa na akili kama ya hao wanaume wanaokufwata wewe hali wakijua kbs kuwa wana wake nyumbani kwao.. ACHA KABISA TABIA HIYO!
Binti chukua muda kaa chini uweze kujitambua wewe ni nani ktk dunia hii. Siwezi kukupa pole kwa sababu ninachoona hapa kwako wewe ni mtu unayependa vitu 'ready made' nina uhakika kabisa kutokana na jinsi ulivo jieleza kuna vijana wa size yako wengi tu wanakufuata lakini wewe unaona hawafai na sorry to say this hii haijatokana na uhusiano wako wa kwanza, tangu mwanzo ulikua una-aim too high ama sivyo hata usingeanza huo uhusiano. Kwa hiyo dada usipokubali kujishusha (actually kurudi kwenye standard yako) na kukubali ukweli utaula wa chuya. Usione hao waume zetu huko barabarani wameng'aa mama tunafanya kazi ya ziada! Muulize hata Rosemary atakwambia...!
ReplyDelete