Thursday, June 24, 2010

HEDHI KUBADILIKA.....

Rose, naomba wenye uzoefu wanisaidie, mimi ninatatizo la hedhi kubadilika kila wakati hamna hata mara nikajikuta napata hedhi tarehe sawa hata mara mbili kila wakati inakuja na tarehe yake hii inanipa wasiwasi sana kwani nashindwa hata kupanga siku zangu ili nizifahamu zipi mbaya(ambazo naweza kupata ujauzito) na zipi nzuri(ambazo siwezi kupata ujauzito) hili limekuwa tatizo kubwa sana kwangu...
nishaurini tafadhali mwenzenu....

3 comments:

  1. POLE SANA DADA KWATATIZO ULILONALO, NAMAI NILIKUWA NA SHIDA KAMA YAKO NIKAENDA KWA GYNO PALE MIKOCHENI NAKUSHAURI NENDA HOSPITAL MIKOCHENI KWA KAIRUKI UTASAIDIWA

    ReplyDelete
  2. Mimi pia siku zangu hubadilika kila mwezi ila zinakuja exactly on the 28th day kwa mfano mwezi huu imeanza tarehe 20 mwezi ujao itaanza tarehe 17 na mwezi unaofuata 14 so i suggest uhesabu toka ile siku unapoanza period to nxt period uone ni siku ngapi kama ni siku 28 then mzunguko wako ni 28 days meaning ukianza period hesabu siku 14-17 days toka siku ya kwanza ya period these days arent safe the rest of the days are ok till uanze nxt period wel it has been working for me for sometime I have one kid and has been using this for sometime and it has been working.

    ReplyDelete
  3. Pole dear mzunguko wa hedhi unatofautiana kwa watu tofauti na hata kwa mtu mwenyewe binafsi. Kuna mizunguko mifupi na mirefu. Na mizunguko hii huwa tunahesabu kuanzia ile siku unaanza kuona damu mpaka ile siku utakayoanza kuona damu mara nyingine. Kawaida mzunguko mzima unaweza kuwa kati ya siku 21 mpaka 35 ingawa watu wengi ni wa siku 28. Kwa mfano ukiwa na mzunguko mfupi siku zote utaona unapata hedhi mara mbili kwa mwezi lakini hiyo si tatizo kama siku hizo zinaangukia katika urefu huo niloutaja.. Kwa hiyo kabla hujaenda hospitali jaribu kuweka alama kwenye kalenda kila unapoona siku zako halafu baada ya kama miezi mitatu hesabu uone mzunguko wako ni siku ngapi kama zitaachana kwa mbali hapo unaweza kutafuta ushauri wa Gyno

    ReplyDelete