tumesikia matatizo mengi sana kwenye ndoa, ndoa za wazazi wetu, ma bibi zetu ndoa zote hakuna ambazo hazikuwa na matatizo, hakuna ndoa ambayo kila siku wao ni watu wa raha tu kuna siku waligombana, kutukanana, hata kupigana mara nyengine na kuhama vyumba ama nyumba kazisa....
sasa basi nataka kuchukuwa muda huu kwenye hii topic kuenzi ndoa zote tuache tofauti zetu pembeni hebu tujipe raha kwa wote walio olewa na kuoa tuwaandike mazuri hapa wenza wetu na tunayoyaona kwenye ndoa zetu ili tuwape wengine wanaotarajia kuingia kwenye ndoa moyo wa kujua ndoa ni sehemu ya raha na baraka tele nitaanza mimi:
ROSEMARY MIZIZI: nashukuru Mungu kwa kunipa ndoa yangu, na mapenzi tele kwa mume wangu mpenzi Innocent Mizizi, leo nataka kumwambia hatakama saa zingine nakuwa pasua ajuwe nampenda sana na namshukuru kwa kuwa mume na baba bora na mwenye mapenzi sana nasi, wenye wivu shauri yao na wanaoleta maneno ili tugombane imekula kwao na kwa wale wanaopenda kujipendekeza kwake madai mnataka kuwa vidumu nawaambia siku zote mtaishia kula ukoko tu wali nakula mwenyewe na mnaojipitisha endelea tu mzidi kumpa ujuzi anipe mie raha na wenye chokochoko mtaendelea kuongea kwani hamjui kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji ulipopashindwa kapata muuguzi wa kumtibu endelea tu na huo ukoko maana wali huuwezi ulishakukaba(wangu nimemdhibiti hasikii wala haoni humu hamuoni ndani, wacha wacha waseme watasema mchana usiku watalala)
raha ya ndoa ni pale tendo linapokuwa tamu na mkapeana bila kunyimana huku kila mmoja akihangahika kumlidhisha mwenzie, hapo ndoa huwa taamu ila mkiboana duh, huwa mnanukiana vibaya
ReplyDeletekwani sio kweli??
wewe utamu wa ndoa ni kupeana vitu na kuhakikisha nyooote mwafurahia wewe
ReplyDelete