Friday, June 25, 2010

ANATAKA NIWE MAMA WA NYUMBANI.....

tokea nimeolewa huu ni mwezi wa tano sasa, na mwanzoni nilikuwa na kazi nzuri sana katika kampuni moja maarufu sana mjini Dar es Salaam lakini tokea nimekuwa mke wa mtu mume wangu hataki kabisa nirudi kazini anataka tu niwe mama wa nyumbani, nikae tu wala sio hata kufanya kazi za ndani maana ameajiri wasichana wa kazi watatu siruhusiwa kufanya lolote kazi yangu ni kukaa tu na kumsubiri mume wangu aje nimuhudumie..
hataki hata niende kutembelea ndugu zangu na marafiki zangu nikiwa peke yangu kutwa mpaka niongozane na wifi yangu ambaye amekuja kukaa na sisi ili nadhani awe ananichunga, nikitaka kwenda salon napewa dereva ananipeleka na wifi yangu, siendi kununua vitu vya nyumbani zaidi ya hao wasichana wa kazi kwenda..
sasa hivi nimeamua tu kujipa kazi ya kupika vitafunio vya chai wakati mume wangu akiwa kazini nijichangamshe maana nimechoka kukaa bila kufanya lolote akiuliza nani kapika akijuwa ni mimi anakasirika sana, yani mume wangu anataka nikae tu mpaka hela ya kununua vitu vya kike anipe yeye ama ananinunulia kwa mwezi nashukuru Mungu nyumbani aliweka computer yenye internet ndio uhai wangu...
huu jamani ni wivu ama ujinga? saingine naona kama amenioa kunitoa kafara, maana kwakweli mume wangu anapesa sana sitaki kudanganya lakini mimi badala nizifurahie naona mateso tu..
siwezi kuandika jina langu nisameheni jamani.

2 comments:

  1. pole dada ata me nineolewa na mume wangu yupo kama wako, me nimemsikiliza anavyotaka na nimeamua tu kukaa nyumbani ili nimfurahishe kwa sababu kila kitu ananitimizia na pesa anazo na ninaishi kwenye nyumba nzuri. huna jinsi dada na mume unampenda vumilia tu.

    ReplyDelete
  2. pole dada, kwa maisha ya sasa kila mtu kuchakalika akileta tano na wewe ukileta tano maisha yanakwenda haijalishi ana uwezo au la sasa jaribu kumbembeleza atakuelewa

    ReplyDelete