Thursday, June 10, 2010

NIMSIKILIZE NANI KATI YA MUME NA MAMA MZAZI....

wenzangu jamani, nimeolewa na kwa bahati mbaya wakwe zangu wote wawili wamefariki lakini wazazi wangu wote wapo hai, kinachonichanganya ni kwamba kunawakati mimi na mume wangu tunaweza kugombana tena sana, na kwavile sina wa kuongea nae najikuta naenda kuongea na mama yangu kwani ndio bestfriend wangu wa pekee maana marafiki wasikuhizi ukimwambia tatizo lako la ndani siku moja tu utalikuta barabarani lakini kwa mzazi anajuwa kutunza siri ya mwanae.......
kwa kweli wakati mwengine ugomvi kati yetu anakuwa amesababisha mume wangu na hata tukijaribu kuliongelea yeye hataki kabisa kunisikiliza, ndipo huenda kwa mama anisaidie na mara nyengine ushauri anaonipa mama japo unauma lakini huwa wamatumaini na wakati mwengine hata kufikiria kutaka kumuacha mume wangu kwani maji yanakuwa shingoni........
nampenda sana tena sana mama yangu lakini pia nampenda mume wangu japo muda mwingi hatuelewani kabisa na mume wangu, nifanyenje jamani maana mpaka mume wangu anakasirika sana hataki hata niende kwa mama yangu kwa kujishuku yakwamba nitakuwa namuongelea lakini hapana sio hivyo..........

0 comments:

Post a Comment