unawezaje kumsaidia huyu dada?
mimi ni dada na nimejifungua mtoto wa pili sasa, kwa mtoto wakwanza mwili wangu ulipendeza sana nikanawili na wala sikua mnene kwa vile nilifunga tumbo basi nikawa na mwili mzuri wala tumbo halikuwa kubwa..
baada ya kubeba mimba ya mtoto wa pili alikuwa wakiume, mwili ulibadilika kwanza nilibabuka uso ukawa mweusi wa mabakabaka, nikaotwa na chunusi nyingi ambazo mpaka leo hazijaisha japo nimeshajifungua, na nikanenepa kwa sababu ya kumnyonyesha mtoto nililazimika kula chakula vyenye mafuta ili maziwa yatoke kwa wingi na huu unene umekataa kabisa kutoka na kwavile mtoto wangu alikuwa mnene nilivyojifungua sikuweza kufunga tumbo ile miezi ya kwanza kwasababu niliumwa baada ya uzazi sasa mwanangu anamiezi sita nimesharudi mpaka kazini...
kinachonisikitisha ni kwamba mume wangu haridhiki kwa huu mwili niliokuwa nao utakuta mara nyengine ananisema kuhusu tumbo langu, na mabaka yangu yani mpaka roho inaniuma sana, yani mume wangu ananikosesha raha sana kama vile hakumbuki mimba niliyobeba ni ya kwake..
naombeni ushauri wenu wenzangu...
DADA UKUTAKIWA KULA CHAKULA CHA MAFUTA NDIO MAZIWA YATOKE NIKO USA NINA WATOOTOO WAWILI WAKIUME MMOJA ANA 2YRS NA NUSU MWINGINE 3MONTH NI KWELI MWILI UNAHARIBIKA ULICHOTAKIWA KUFANYA NI KUNYWA MAJI 1 GALLON A DAY AU JUICE KWA WINGI NA MAZIWA NA CHAKULA CHA KWAIADA TU ASLONG UNADRINK MAJI TOSHA MAZIWA YANAJAA SANA MPAKA YANAMWAGIKA NA PIA KUFANYA MWILI WAKO URUDI UNATAKIWA KUKIMBIWA MALA 3 AU 4 KWA WEEK KWA MDA WA NUSU SAA AU ONE HOUR MAZOEZI YANASAIDIA NGOZI YAKO KUWA NZURI ZAIDI NA KUTONE MWILI WAKO PIA. NA UKIWA NYUMBANI FANYA SITUP KWA WINGI NA KAMA UNAPATA BIA INAONGEZA TUMBO HOPE NIMESAIDIA KIDOGO KWA MAWAZO
ReplyDeletepole sana shostito hayo mabadiliko lazima yawepo nimeon awengi sana tena baada ya kujifungua mtoto wa pili, sasa wewe ulikosea sana pale mwanzoni ianwezekana ulikuwa unajishindilia saan ile misosi si unajua ukiwa na akina mama karibu nao wanzidisha kweli kukupakia,mi naoan cha muhimu sasa hv punguza kabisa hivyo vyakula acha kunywa hayo mauji na masupucozmtot kashakua, mi mwenyewe nimemaintain baada tu ya kujifungua nilikua nakula lakini sio sana tena baada tu ya miezi 3 nikaacha kabisa mauji na supu yani pale nilipoanza tu kazi, ila unjitahidi kumpa mtoto maziwa na vyakula vingien anashiba na kwako ananyonya jion na usiku maaana mchana si unakua job?
ReplyDeletepia kama unaweza anza na mzoezi ya kutembea kila jioni, ruka sana kamba itakusaidia. kunywa sana maji ya moto, acha kbisa vyakula vya mafuta.
Take care shost wanaume ndo walivyo ukicheza vibaya hapo mwenzio atatafuta dogodog sasa hv.