Thursday, June 24, 2010

MTOTO WA MIEZI TISA NA UJAUZITO...

mimi nimeolewa na Mungu alinisaidia nikapata mtoto wa kike anamiezi tisa na nilipojifungua nilijifungua kwa kisu, sasa nimegundua juzi ya kwamba nimebeba mimba tena ambayo itakuwa kama wiki tatu, nilipoona kipimo kimekuwa positive nilichanganyikiwa nikataka kwenda kuitoa lakini nikakaa na kufikiria kuua kiumbe kisicho na hatia nikajisikia vibaya sana na nikaamua kuiweka huu ujauzito, kwasababu mwanangu huyu wa miezi tisa alishaacha kunyonya siku nyingi sana na baba yake anataka nibebe huu ujauzito............
kwa sababu nilijifungua kwa kisu na mimi bado msichana wa miaka 24 ikabidi niwa ulize wakubwa zangu kama nitapata madhara nikiibeba hii mimba kwanzia kwa daktari wangu ambaye ameniambia hamna tatizo kabisa kama nimeamua kubeba ni bebe tu na wengine wamenishauri nikaitoe kwani itamdhuru huyu mwanangu wengine wanasema anaweza kuchelewa kutembea, wengine wanasema ataduwaa na mambo mengi tu ya kunikatisha tamaa...............
kinachonichanganya ni kwamba watu niliowaomba ushauri yani wananishangaa wananifanya nione kama nimefanya dhambi, wananisema mpaka nachanganyikiwa japo mama na baba yangu wananiambia kwa vile upo kwenye ndoa na mtoto hanyonyi hamna tabu mbona watoto wa kwanza na wapili hufululiza hiyo ni kawaida..................
nwenzangu nimefanya vibaya kubeba huu ujauzito? ni kweli nitambemenda mtoto wakati hanyonyi?

6 comments:

  1. sasa kama umeshaongea na mume pamoja wazazi wako unataka lipi tena kwa walimwengu? Jali ya kwako huwezi kumfurahisha kila mtu siku zote bidada. Tena umshukuru Mungu kwa kila jambo maana kama plan yako ni watoto 2 imagine in 10 years time utakuwa bado m-bichi ilhali una watoto wakubwa na utapata muda mzuri tu wa kuwalea.

    ReplyDelete
  2. Hujafanya ubaya wowote, yani usiwe na wasiwasi kabisa, mimi kwenye familia yangu nina madada zangu wawili, walibeba mimba watoto wakiwa na miezi 9 na mwingine wa kwake alikuwa miezi 10, na watoto wako poa kabisa. Usijisikie vibaya, enjoy baraka zako kutoka kwa Mungu

    ReplyDelete
  3. Hujafanya kosa lolote na wala hutambemenda huyo mtoto asikudanganye mtu ungekuwa unanyonyesha ungebidi uache ila kwasababu haunyonyeshi so you are good to go goodluck my dear usisikilize ya hao wanaokukatisha tamaa your parents na mumeo are on your side and thats all you need.

    ReplyDelete
  4. kama umewauliza wazazi wakonawakakuambia hamnashida sasa unawasiwasi gani tena? nimbaya kama unaendelea kumnyonyesha mtoto lakini kama humnyonyeshi hakuna ubaya yeyote itakayo mpata mtoto wako wewe usisikiliza yawalimwengu mbona wengi tu wanazaa mtoto akiwa hata chini ya miezi 9 mradi uko kwenye ndoa na doctor wako amezema hakuna ubaya sasa unataka ushauri gani tena?

    ReplyDelete
  5. jamani hili swala la kubemenda huwa hakuna,according to doctors huku ulaya wamesema amna swala kama hilo kwanza walinishangaa sana nilivyowaelezea kuhusu hilo.

    ReplyDelete
  6. you are very luck dada,,siku hizi wengi hupenda iwe hivyo, utapata mtoto wa pili wa kwanza atakapokuwa na umri wa mwaka na nusu,,which is very Ok,,na pia ujue kwamba watoto wanatafutwa kwa sana na ni zawadi kutoka kwa mola...achana na mawazo potofu ya kutoa mimba hiyo,,

    ReplyDelete