wanaume wote mnaoishi na wanawake nyumba moja kama mke na mume kuweni makini sana ikija kwenye hili swala la hela mnazoacha za matumizi nyumbani, hivi wewe ukiwa kama baba unafahamu jukumu lako ni kutunza familia na kuhakikisha wanapata yote wanayohitaji hata kama huwezi basi kidogo unachopata utumie vizuri nyumbani sikia mkasa huu...
kuna baba mmoja alikuwa anaishi na mke wake bahati mbaya hawajapata watoto bado, sasa huyu baba kila alipokuwa akienda kazini alikuwa anamtindo wa kumuachia mke wake Tshs 1500 kama hela ya matumizi pale nyumbani, sijui ni kwasababu ya wivu anajua mke wake atajipangia safari atakapokuwa amempa hela nyingi, ama ni kwasababu yule baba alikuwa hana hela..
huyu baba alikuwa ni mtu wa kulewa na alikuwa mvutaji sana wa sigara, kwahiyo akishatoka kazini hupitia kwenye vilabu vyake vya pombe ndipo anarudi kula nyumbani, hata siku moja hali nje huyu baba zaidi ya nyumbani kwake..
cha kushangaza huyu baba kila alikuwa akirudi nyumbani anakuta mke wake ameandaa chakula kitamu na chenye bei kuliko hela aliyoiacha yeye, na sio hicho tu atakuta na box la sigara mezani pamoja na nauli ya kwenda kazini kesho asubuhi.. hehehe na hiyo ni kila siku
yule baba yani nje anavyomsifia mke wake kwa rafiki zake utamkuta anasema yani mke wangu jamani anavyojuwa matumizi yani namuachia hela kidogo lakini nakuta vitu vya hatari(vizuri), wenzake wanashangaa inamaana hujui ama hutaki kuamini kama unasaidiwa? wenzake wanamuuliza lakini jamaa haelewi chakuamini ni kipi anachojuwa yeye ni kwamba mkewe anajuwa matumizi lakini sasa kwa hela anayoiacha kila siku na jinsi vitu vilivyopanda bei wewe msomaji unasemaje?
0 comments:
Post a Comment