unajuwa kama kuwa mama its a full time job, nilikutana na wamama tofauti ni kawauliza wanachukuliaje swala zima lakuwa mama na ni changamoto gani wanazo zipata wakanipa mawazo yao, ambayo nitayaandika hapo chini na kuruhusu wamama wengine pia kutoa mawazo yao ili wote kama wamama tupeane nguvu na moyo katika watoto wetu na jamii nzima....
MAMA BRIAN: anasema yeye alivyopata mwanae miezi ya mwanzoni hakuamini na alikuwa anakosa usingizi kabisa muda mwingi alikuwa anatumia kumuangalia mwanawe na baada ya muda mtoto kukuwa sasa hivi amekuwa mtundu yani mpaka wakati mwengine mama brian anakaa nakulia hajui amfanyaje mwanae..
MAMA TULY: yeye alijifungua mapacha na anasema kunakipindi kilikuwa kinafika anasahau hata kuoga siku nzima kwa shughuli aliyonayo kuwa kubwa ya kuwalea hao mapacha..
MAMA ZAINAB: anawatoto sita na anasema wote anawapenda sana lakini anawatoto watatu ambao yani mapenzi kwao anahisi yamezidi kuliko hao wengine, je wewe kama mama mwenye watoto zaidi ya wawili unamtoto unayempenda zaidi kuliko wengine?
MAMA RAHMA: anasema yeye kunawakati alijikuta anamchukia sana mume wake kwasababu alikuwa anahisi hamsaidii katika malezi ya mtoto, mume wake anamtaka mtoto pale tu anapokuwa msafi na halii lakini akitakiwa kubadilisha pamper humita mkewe tu, na akianza kulia humpelekea mkewe ndio ambembeleze hichi kitendo kilimchukiza sana mama rahma..
WAZO MUHIMU:
kama mama ni jukumu lako kulea watoto wako vizuri na kuhakikisha wanakula vyakula vyenye afya na wanakuwa katika ghali ya usafi muda wote,kwa afya ya watoto wetu tusipende kuwapa watoto junk foods..
na waume zetu wawe mstari wa mbele katika kutusaidia kwenye malezi ya watoto isiwe kwenye fedha tu bali hata malezi kama kumbadilisha pumpers, kumpa maziwa na mengine mengi..
Mama Mark: my son is the apple of my eye!
ReplyDelete