Wednesday, June 23, 2010

ANAPENDA NISIYOYAMUDU....

mwanamke wangu anapenda mambo ya juu, mambo ambayo yapo juu ya uwezo wangu mimi naendesha starlet akiuona mwanaume amepita anaendesha benz anamuangalia kwa matamanio na kuongea maneno kama "mwanaume wa kweli mwenye pesa zake" na kaa kwenye chumba na sebule mara nyingi tukigombana aniambia unaringa kwa kukaa humu kwenye banda la kuku? wakati mwengine sina hela kwahiyo tunakula ugali na maharage basi yeye anajifanya kama anatania leo naona tupo segerea, sina uwezo wa kumpa laki mbili kwenda kununua nguo mara namuona kila siku sasa anavaa nguo mpya nikimuuliza amepata wapi ananiambia kwani wewe baba yangu mpaka uniulize? halafu akiona nimekasirika anasema kapewa na mama yake
huyu mwanamke wangu kwakweli japo nampenda lakini ana chokochoko nisizo zipenda na ninachowaza haya tu hata kumuoa bado huko mbele itakuwaje?
nisaidieni ndugu zangu

3 comments:

  1. wewe usiwe mjinga jibu ushalipata hapo sasa unamng'ang'ania wa nini,huyo ana tamaa atakukost shauri yako.

    ReplyDelete
  2. Labda unasubiri ushahidi ukamilike, ila data zinatosha kukata fuse. Kama ingekuwa mimi siku nyingi sana, nilishatema.

    ReplyDelete
  3. jali maisha yako acha nae ajali tamaa zake.

    ReplyDelete