Tuesday, June 22, 2010

DADA YANGU HUTEMBEA BILA NGUO...

nyumbani kwetu tunakaa wasichana wa nne wote tukiwa tumezaliwa na mama mmoja, wote tunafanya kazi na tunawanaume zetu lakini kuna tatizo moja ambalo nataka nisaidiwe dada yangu mmoja hupenda sana kutembea bila nguo nyumbani yani mara nyingi anakuwa amevaa nguo ya ndani tu na sidiria.
tumesha jaribu kumsema lakini jitihada zetu hazikuzaa matunda, na mbaya zaidi utakuta akiwa ndani na wanaume zetu wakija kututembelea wala haoni aibu kukatiza kutoka chumba moja mpaka kingine akiwa na nguo yake ya ndani.
mpaka sisi tunaona aibu kwa niaba yake na wivu hutushika pale tunapoona wanaume wetu wanavyomshangaa kwa matamanio, hili linatukera sana. angekuwa mdogo tungemchapa labda kwa kiboko angeelewa lakini ni mtu mzima tumfanyaje?

1 comments:

  1. hapo kina dada hameni nyumba mmwache pekeyake, kwani hana adabu kabisa.

    ReplyDelete