shoga yangu we kwanza hongera sana kwa kupata mume, na hongera sana kwa kitchen party yako ilipendeza sana tena sana mwenzangu kama walivyokufunda kule nenda kaitunze nyumba yako na Mungu akusaidie....
maana manungaembe ambayo hayajaolewa kazi kufwata wame za watu wapo dada tena kibao na kila siku waongezeka, tunza ndoa yako mtunze mumeo kwani kabla ya kutaka kukuoa wewe aliona wasichana wa kila aina akawaona hawamfai kuwa mke wake akakuchagua wewe basi dada chokochoko za barabarani wala zisikunyime amani katika nyumba nakujuwa wewe ni mvumulivu utashikilia mpaka mwisho usiwe mjinga ukajapoteza nyumba yako kwa kupenda ya dunia....
ndoa kazi babu sio kila mtu anaweza kuitunza tumeona wengi wameachikana kubaki kutangatanga na dunia(nadhani unanielewa hapo vizuri) lakini naamini wewe utaituza vizuri sana....
na Mungu akubariki ukapate watoto wenye kufanana na nyie sana wawaletee amani na kuwazidishia upendo tele kwenye ndoa......
0 comments:
Post a Comment