Wednesday, June 25, 2014

Loohhh jamani mambo haya tunayoleteana katika familia tunayachunguza kabla ya kuyapokea...

KUNA FAMILIA MOJA YA WAZAZI NA WATOTO WAO WATANO, HAWA WALIKUWA TU NI WAKRISTU WANAOSIHI NA KUABUDU IBADA ZAO ZA KIKATOLIKI TOKEA MWANZO NA KUISHI KWA AMANI

MTOTO WAO MKUBWA WA HAWA WAZAZI NI NESI AKAAMUA KUINGIA KATIKA ULOKOLE KATIKA KANISA FULANI MAARUFU SINTOLITAJA JINA..NA KUANZA KUSALI HUKO

AKAWA ANAENDA HUKO ANASALI MARA KWA MARA YANI MAISHA YAKE YAKAWA NI KUABUDU, KAZINI NA NYUMBANI..BASI MAISHA YAKASONGA

SIKU ZIKAENDA MARA WAZAZI WA YULE DADA WAKAAMUA NA WAO KUOKOKA NA KUHAMIA KATIKA HILO KANISA NI SABABU GANI WALIAMUA MIMI NA WEWE HATUJUI NI ZA KIFAMILIA ZAIDI

NA NDUGU ZAO WENGINE PIA WAKAAMUA KUHAMIA KATIKA HILO KANISA KWAHIYO NYUMBA NZIMA SASA WAKAANZA KUSALI KATIKA HILO KANISA JIPYA LA KILOKOLE

BWANA BWANA KUMBE KATIKA HILI KANISA HAWAAMINI NA ISHU ZA KWENDA HOSPITAL UKIWA MGONJWA WANAKUOMBEA NA KUFUNGA MPAKA UPONE!!!!!

BASI WAKIUMWA KWAO UNAKULA TU VIZURI UNAOMBEWA MPAKA UNAPONA

 SASA BASI KASHESHE IKAJA MIEZI MITATU ILIYOPITA AMBAPO HUYU DADA MKUBWA ALIUMWA TB, AMINI MSIAMINI HAWAKUMPELEKA HOSPITAL WALIMUACHA NDANI TU WAKAWA WANAMUOMBEA TU

YULE DADA KAUMWA YANI KWAUMWA, MPAKA BAADAE SASA WALIPOONA ANAZIDI KUZIDIWA NA WATU LABDA KUWASEMA NDIO WAKAAMUA KUMPELEKA HOSPITAL KUTIBIWA NA KUPEWA DAWA ZA TB AMBAPO MPAKA LEO ANAJISIKIA VIZURI NA MWILI UMERUDI

KIMBEMBE SASA HUYU DADA WAKATI ANAUMWA ALIKUWA ANAUGUZWA NA MDOGO WAKE WA NNE, AMBAYE NDIYE ALIKUWA ANALALA NAYE KIPINDI CHOTE KILE, SASA KUTOKANA HAKUWAHI HOSPITAL MPAKA MIEZI MIWILI BAADAE AKAWA KUMBE AMESHAMUAMBUKIZA TB HUYU MDOGO WAKE

MDOGO WAKE AKAANZA KUUMWA NDANI KWA NDANI BILA KUMWAMBIA MTU, ANAJIKAZA MAANA ANAMTOTO MDOGO WA MIAKA 4 KWAHIYO ALIFICHA UGONJWA KWA KUWA BUSY NA KANISA NA MTOTO, KUMBE ALIKUA ANAUMWA SANA NDANI KWA NDANI

 AKAWA AKIULIZWA MBONA LEO UNAPOOZA OOHH NAJISIKIA TU VIBAYA LAKINI NIPO SAWA KWAKUA TU ALIKUA ANAJUA HATA NIKISEMA NAUMWA SINTOPELEKWA HOSPITAL ZAIDI YA KUFANYIWA TU MAOMBI, NA ALIKUWA HANA KAZI KWAMBA ANAHELA AKAJITIBU PEMBENI KWA SIRI NA BABA MTOTO WAKE HAWANA MAWASILIANO

HIVYO HIVYO UKIMUONA KWA NJE NASIKIA ALIANZA KUKONDA SANA MAANA KUNA JIRANI MMOJA RAFIKI YANGU NILISIKIA ANASEMA ILIFIKIA NIKAMWAMBIA KAMA HUTOFANYA BIDII YA KWENDA HOSPITAL HATA KWENU SINTOKANYAGA..HUYU NI RAFIKI MKUBWA SANA WA HUYU DADA ANAYEUMWA

LAKINI HATA KWA KUPOTEZA MARAFIKI HAKUFUNGUA MDOMO KUSEMA ANAUMWA SANA MPAKA SIKU YA JUMAPILI ALIPOINGIA CHUMBANI KULALA MCHANA NA HAKUAMKA TENA NDIO ILIKUWA SIKU YAKE YA MWISHO DUNIANI

NI MSICHANA MDOGO TU WA MWAKA 1991 AMEKUFA AMEACHA MTOTO WA MIAKA 4..

CHAKUSHANGAZA KWENYE MSIBA HAWA WATU WA KANISA HAWAKUPI POLE KWA KUFIWA WENYEWE WANAKUPA HONGERA KWA KUFIWA

MAUBIRI YALIKUWA TOFAUTI NA YA MSIBA HUKU TULIANZA KUHUBURIWA KUOLEWA, NA KUOA, KAMA UMEFUNGWA BASI LEO UTAFUNGULIWA...NA MAMBO MENGINE YA TOFAUTI

KWAKWELI NILISHANGAA SANA

****END***

Reactions:

0 comments:

Post a Comment