Wednesday, May 28, 2014

Nimekwanyua huko uswahilini, Yanawezekana haya kwenye ndoa zetu?
Usifanye haya
1. Usimpige
2. Usimpe maneno ya kumnyanyasa
3. Usimfanye aone kudharauliwa
4. Usimfanye aone hapendwi
5. Usimbake
6. Usimdanganye na kuwa na wanawake wengine
7. Usiichukie au kutoipenda lugha yake ya
mapenzi.
Fanya haya
Mpe utofauti atakupa upendo
Mpe tabasamu atakupa furaha
Mpe moyo wako atakupa maisha yake
Mpe nyumba atakupa familia bora
Mpe wazo lako atakupa mpango wa kutimiza
wazo lako.
Mfanye malkia atakufanya mfalme
Mpe mapenzi naye atakuwa wako tu
Ila mdanganye na utaona jinsi atakapoyafanya
maisha yako kuwa magumu zaidi ya jehanamu
hapa duniani

Reactions:

0 comments:

Post a Comment