Thursday, May 22, 2014

Kweli mke wa mtu anauma mume apige yeye tu mechi za nje akipigiwa...............PART 2

Tulopotosheka tukiwa tumelala kitandani kila mmoja wetu akitafakari tukio lililoisha tulikaa kimya dakika kama kumi huku tumekumbatiana bila mtu yoyote kuongea kitu

Ghafla nikasikia mkono umepita juu ya tumbo langu huku akinipapasa kwa huba akaniambia itakuwaje baada ya hapa,najua hutoruhusiwa tena kutoka na ukirudi utakuwa ugomvi kwakuwa ulimtotoka dereva

Nilikaa kimya nikitafakari cha kumjibu nikajikuta sina la kuongea..tukajiandaa nusu saa baadae na kuondoka kabla sijafungua mlango wa hotel alinivuta mkono akanisogeza karibu yake mikono yake ikiwa inanipapasa shingoni na kwenye nywele zangu akanibusu kwa mahaba na kuniambia ananipenda..nikaondoka

Nikiwa njiani kurudi nyumbani nikawasha simu na kupokea msg kutoka kwa mume wangu dereva amempigia kumwambia sikuwa nyumbani alivyorudi kariakoo nimpigie nitakapowasha simu

Nikampigia na kumwambia mume wangu mgonjwa alihitaji maji ya madafu kwahiyo nikakimba ufukweni coco kumnunulia..mume wangu alinifokea sana na kuniambia hiyo sio kazi yangu ningemtuma dereva atakaporudi niliomba msamaha mume wangu akanikatia simu

Nikamkuta dereva nyumbani akanichukua kunirudisha nyumbani goba, Maisha yakaendelea huku nikiwasiliana na mpenzi kwenye simu tu kama miezi mitano mfululizo tuliumia sana kushindwa kuonana lakini hatukuwa na la kufanya

Mwezi wa sita wake mdogo wangu akatambulisha mchumba nyumbani wakaamua kumfanyia sherehe ndipo nikamuomba mdogo wangu amualike na mpenzi wangu nilikuwa na hamu hiyo jumapili ifike nikamuone mpenzi wa roho yangu

Jumapili ilipofika tukaenda nyumbani kwa ajili ya sherehe baadae mpenzi alikuja kwa jinsi alivyopendeza na nilivyomkumbuka nilitamani kumrukia na kuanza kumbusu..lakini sikuweza tuliishia kuangaliana kila mtu akimtamani mwenziye

Tulijitahidi kuficha hisia zetu sherehe ikaisha kila mtu akaondoka tukarudi nyumbani,  Kutokana na mapenzi kunizidia nje sikujua ndani niliyapunguza mume wangu akaanza kunichunguza kwanzia na simu yangu

Anasema alienda kampuni ya simu na kuangalia niliyoyafanya kwenye simu yangu na kugundua hiyo number inayonipigia mara kwa mara na muda huohuo

Bila mimi kujua mume wangu anafanyaje siku akaniaga anasafiri mimi nilifurahi nikijuwa nimepata wiki nzima ya kuweza kumuona mpenzi nitakapo..mume wangu akaondoka

Mimi siku hiyohiyo nikampigia mpenzi na kwenda nikakaa huko tukifurahia penzi jioni nikarudi nyumbani

Siku ya pili na ya tatu pia hivyo hivyo tulikuwa tunajiachia tukijua tuko peke yetu tunafurahi

Kumbe wakati wote huo mume wangu alinifwatilia nyuma na kujua nyendo zangu siku ya nne nikiwa nimeenda kukutana na mpenzi ile tumemaliza tunataka kuondoka gari ya mume wangu ilisimama mbele yetu ikatukinga na kushindwa kuondoka

MUNGU wangu mume wangu!!!!!! tulibaki tukiangaliana mume wangu akafungua mlango wa dereva bila mafanikio kwakuwa ulikuwa umelokiwa akavunja kioo na kufungua akamtoa mpenzi wangu na kumpiga sana alimpiga sana mpaka damu zikaanza kumtoka puani na mdomoni mpaka alipokua amelala hawezi hata kujitetea mume wangu akanivuta mkono kuniingiza kwenye gari yake tukaondoka na kumuacha mpenzi wangu pale

Mume wangu alikimbiza sana gari huku akihema sana nikajua tutagonga tushindwe kufika nyumbani. Tulipofika nyumbani akanivuya kutok kwenye gari akaniwash vibao viwili vya nguvu sana na kuniacha hapo akaingia ndani

Nikaingia ndani cha kwanza nikaenda bafuni kuoga nilikuwa nalisa sana uchungu mara mbili wa kupigwa na kumuwaza mpenzi wangu sijui huko alipo anahali gani sijui watu walimuokoa

 Sikuweza kumpigia simu nisije kusikia nikauliwa basi nilisali tu na kwenda kulala

Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili napigiwa simu ma mtu anasema alimokota mwanaume akiwa na hali mbaya sana na wakamkimbiza hospital lakini kabla hajafika hospital alifariki
..tumeamua kupiga simu number zilizokwenye simu yake ili ndugu zake wamfwate hapa muhimbili mtatukuta


Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili napigiwa simu ma mtu anasema alimokota mwanaume akiwa na hali mbaya sana na wakamkimbiza hospital lakini kabla hajafika hospital alifariki
..tumeamua kupiga simu number zilizokwenye simu yake ili ndugu zake wamfwate hapa muhimbili mtatukuta


Nilisikia kama nimemwagiwa maji ya baridi nilipiga mayowe na kulia sana nilishindwa kuvumilia..na jana ndio ilikuwa siku ya mwisho kumuona mpenzi wangu

Siwezi hata kumwambia mume wangu.....sidhani kama nitaweza kupenda tena kama nilivyompenda mpenzi wangu...na ninajipanga kuachana na mume wangu maana siwezi kuishi na mtu aliyeniondolea furaha ya pekee kwangu ukiacha mtoto wangu...

*****END*****

0 comments:

Post a Comment