Wednesday, April 16, 2014

Jamani aibu hizi hawa wanaume hapana jamani...

mimi naamini katika mahusiano mpaka mmeamua kuwa pamoja basi mmependana kama sio kutamaniana na mkataka kuwa pamoja.

na mnapoamua kuwa pamoja ni pamoja na kubebeana misalaba, kuwa pamoja katika shida na raha ambazo baadae huenda kwenye ndoa

Japo baada ya ndoa mara nyingi sasa watu ndio wanaanza kutoa makucha yao ya asili yani mtu mpaka unachanganyikiwa hivi huyu mimi nilimtoa wapi mbona mwanzo hakuwa hivi

Jana kuna rafiki yangu nilikuw naye sehemu akawa ananihadithia story za kuhusu yeye na mumewe akiomba ushauri afanyaje maana amechoka kudharilishwa

kwanza kabisa mumewe hana adabu..mimi ndio nilichomwambia hicho baada ya hizi story zake

huyu dada kwanza alianza kushangaa kila msichana wa kazi akiletwa nyumbani kwake huwa hakai muda anaondoka, mpaka akaanza kujiuliza kwani mimi ninamatatizo gani au sijui kukaa na wasichana wa kazi mbona kila ninayempata anakaa wiki mbili tu nakuondoka

 kumbe bwana mumewe alikuwa anajisevia dada wa kazi, mkewe akiwa kazini huyu baba kwakuwa yupo serikalini basi anatoka kazini akiaga anaenda lunch kumbe anarudi nyumbani kula dada wa kazi

kwahiyo wadada wote waliopita hapo na kuondoka waliondoka tu bila kumwambia mama mwenye nyumba kwanini wanaondoka akawa bado anajiuliza ila anasema hakuona mabadiliko maana kama kitandani mumewe anajiweza anampa mkewe mbili tatu kwahiyo hajakaa kuwaza vyengine

basi bwana yule mama akawa anawaza labda hawa wasichana ninaowapata mimi ni wadogo wanashindwa kazi za nyumbani pamoja na kulea watoto ngoja nitafute dada mtu mzima ambaye tumelingana umri

kweli akatafuta mdada akampata mdada wa tanga ambaye alikuwa amelingana naye umri huyu mama yeye aliachika kwenye ndoa yake tanga akawa anatafuta kazi ndio kuamua kuja kwa huyu dada

 basi kama kawaida ya baba tena mambo yakawa vilevile unaachwa wiki moja uzoee mazingira wiki ya pili unaingia shift...mmmhh yule dada akashindwa kuvumilia na yeye akaamua kumwambia yule mama ukweli

yule mke tena kupanic ndio kwenda kumchamba mumewe mumewe akakataa katukatu na kumsingizia dada labda yeye ndio alikuwa anamtaka, basi yule mama akamuamini mumewe na kuanza kumchamba dada na kumfukuza kazi, dada wa watu akaondoka na kurudi kwao tanga

basi wakaona kwakuwa wasichana hawakai basi wawapeleke watoto boarding school kweli wakafanya hivyo, wakaendelea kuishi wenyewe tu kwa amani na upendo

basi bwana maisha yakasonga, chakushangaza mkewe akagundua kwamba mumewe ameanza kuwatongoza mpaka marafiki zake

huyu dada na mumewe wote wapo facebook yule baba anaingia kwenye account ya mkewe anaanza kuwatongoza marafiki wa mkewe, mpaka siku hiyo akamtongoza mmoja na huyo kumwambia mkewe na kumtumia msg zote bwana alizokuwa anamuandikia

sasa mdada kachanganyikiwa anasema huyu kanionyesha je wale ambao hawajanionyesha ameshatongoza wangapi na kulala nao wangapi

sasa mwanamke amechoka kudharaulika jamani afanyaje, na ni mwenzetu humu ndani kwahiyo kila mtakachokuwa mnamshauri atasoma, na kujifunza.

*******END*******

Reactions:

2 comments:

  1. Amuwekee vikao wazaz nandugu zake kwamba kachoshwa...asipobadilika aangalie njia mbadala huku akihofia naafya yake..wanawake wengine banaa eti unaambiwa kitu chakukusaidia badala yakufanya uchunguz...eti coz nimumeo basi aliekwambia nimbaya..ndomaana mnageukwaga hiv hivi...mwngne ndoangempa penz lahaswa kukukomesha bidada unaeshtuliwa unajiwazimmsha kwamahaba niue..badala yakufanya uchunguz unakurupuka tu...next tym udirudie

    ReplyDelete
  2. Achana nae ukiendelea kusubiri utakufa kwa UKIMWI hawezi kujirekebisha ana pepo la ngono huyo. anza upya thamini utu wako na afya yako kwa ajri ya watoto wako

    ReplyDelete