Thursday, January 2, 2014

Kuoa na kuolewa ni bahati au ni Baraka... Part 2

nikiwa ndani sijui kwa nini nilijikuta namuwaza sana, sijui ni lile tabasamu lake au ni ule upole wake aliokuwa nao hata kwa kuongea ni mtaratibu sana nilihisi natamani kuwa naye zaidi na zaidi

alipofika nyumbani akanitumia msg nashukuru kwa siku hii ya leo wewe ni mrembo sana..nakutakia usiku mwema

nilifurahi sana kupata ile msg kutoka kwa konda nami nikamjibu ahsante sana usiku mwema pia

 ikapita siku mbili sijasikia kutoka kwa konda nikawa najisikia vibaya na kujishangaa kwanini najisikia vibaya asipowasiliana nami nikagundua nimeanza kumpenda au namtamani, lakini ndani ya moyo nikawa namkandia mtu mwenyewe konda atanipeleka wapi wazazi wangu si wataniua

japo nilijitahidi sana kumkandia konda moyoni lakini akili na mwili ulikuwa unamuwa za yeye tu, mara nasikia mlio wa msg kwenye simu kuangalia ni konda alikuwa ananisalimia na kuniambia anakumbuka tabasamu langu

nilifurahi sana nikaibusu simu na nikarukaruka nikamjibu hata mimi nimekumbuka maneno yako na sauti yako ya upole..

Huwezi amini ikaishia hapo hakuniandikia tena siku hiyo, nilikuwa nawashwa vidole nimpigie ila najikaza, nimtumie msg ila nasita yani nilikuwa situlii, nikaamua kunywa beer zangu tatu nisinzie nisimuwaze konda maana ningepata uchizi

basi bwana hakuwasiliana nami kesho yake na kesho yake tena keshokutwa yake akanipigia simu kwamba anaomba tukutane tena palepale break point kijitonyama na huwa anapapenda kwasababu ni weekend hataki niwe naenda mbali na nyumbani..uuuwwwiiii nilifurahi mimi moyo ulijaa na furaha nilikuwa nahisi kama nataka kuingia kwenye simu nikamkumbatie na kumbusu..

yani mwili wangu ulishafika sehemu ya kuwa tayari kuwa na konda kimapenzi japo niliogopa kazi yake lakini nilimtaka tu yeye sikutaka tena kujali anafanya kazi gani

Jumamosi tukakutana tena lakini wakati huu nikamuomba mimi ndio nilipe bill, akasmile tabasamu ambalo lilinifanya nitake kupeleka lips zangu kwake nimyonye ile midomo, na alikuwa na meno meupe sana yani hakustahili kuwa konda huyu kaka alitakiwa kuwa bank..

tukala, tukanywa tukaendelea kuongea yani nikaanza kuhisi mwili wangu unabadilika palepale nilihitaji kukumbatiwa na kuambiwa maneno ya mapenzi yani nilimuhitaji sana konda lakini nilijitahidi kuvumilia ili asigundue

nilikuwa nimeweka mkono wangu kwenye meza, mara akaugusa na mguso ule ni mguso wa mahaba alinishika huku akinisifia jinsi nilivyo na vidole vizuri, vidole virefu vilaini huku akiwa ananishika mimi huku nipo hoi nahisi nililoa maana nilihisi kutokwa jasho kwenye mapaja, huku moyo ulikuwa ukinienda kasi sana...nikamshukuru na kumwambia hata wako sio mbaya sana ila unasugu tu ya kudandia mabasi halafu nikacheka...alicheka saaaaaaaana kwa mara ya kwanza hakutabasamu alijiachia na kucheka sana..akasema amefurahi sana kwahayo maneno

lile nililokuwa nalisubiri ama nahisi kulitaka likatokea konda akamwaga moyo wake mbele yangu siku hiyo...

alinieleza ni jinsi gani alivyonipenda tokea siku ya kwanza aliponiona, mda wote huo hakujua la kufanya na hakutaka kwenda kwa pupa ndio maana alikuwa tu ananipigia na kujua hali yangu, baada ya kukutana nami mara ya pili sasa na kuhakikisha sina mtu ameamua aniambie ukweli..ila akaniambia pia sintokulazimisha kama hutaki kuwa na mimi japo nitaumia, na kama haupo tayari kwasasa nitakuacha mpaka utakapokuwa tayari lakini ujuwe tu nakupenda sana

Rose nilitaka kufa, hayo ni maneno niliyokuwa nayataka kusikia lakini nikifikiria kazi yake nataka kuchanganyikiwa..lakini moyoni nikasema potelea mbali litakalotokea na litokee nikaa kama dakika tano kimya na kumjibu nakupenda pia

 Rose nilitaka kufa, hayo ni maneno niliyokuwa nayataka kusikia lakini nikifikiria kazi yake nataka kuchanganyikiwa..lakini moyoni nikasema potelea mbali litakalotokea na litokee nikaa kama dakika tano kimya na kumjibu nakupenda pia

alifurahi sana, yani alitabasamu tabasamu zito zuri ambalo linazidi kunichanganya kwa mara ya kwanza akanibusu kwenye lips, uuwwwiii sikutaka atoke maana alinikiss kwenye lips kwa sekunde kama kumi hivi bila kutoka..moyoni nilikuwa tu nasema nadondoka nadondoka uuuwwwiiiii

akatoka tukakaa kuendelea kunywa wote tulikaa kimya bila hata kuwa na cha kuongelea alibaki kuniangalia na mimi kuangalia chini kwa aibu, mpaka alipoamua kuanza kuongea na kuniuliza sasa itakuwaje baada ya hapa

nikamuuliza unamaanisha nini??

akaniambia utawaambiaje marafiki zako kuhusu bwanayako konda, maisha yako hayatabadilika??? uatweza kuja kwetu uswahilini hayo ndio yalikuwa maswali ya konda...nikamjibu tu sijui ila nitajua huko nitakapoulizwa

basi kama kawaida yetu tukatembea akanirudisha nyumbani ila wakati huu ilikuwa tofauti alinishika mkono tulipotembea njiani, na tulipofika nyumbani alinikumbatia na kunibusu tena mdomoni kwa juu nilipotaka kuingia ndani

sasa kwa akili zangu nikaanza kujiuliza mbona huyu hanipi busu la ukweli ananibusu tu mdomoni juu au hajui haya mambo ya malavidavi..kasheshe

basi akaondoka nami nikaingia ndani moja kwa moja kitandani kuanza sasa kufikiria uuuwwwiii nampenda ila sijui itakuwaje

 miezi ikapita, sikumoja konda akaniambia anataka niende nyumbani kwao nikawasalimie wazee wake wala sikukataa basi siku hiyo nikavaa nguo yangu ya heshima huyo nikaenda mpaka kwao mbagala rangi tatu nikapita kona hado kona mpaka nikaiona nyumba

ni nyumba tu ya kawaida nilipofika kupaki nikamkuta mpenzi yupo nje ananisubiri akaja kunifungulia mlango na kunikumbatia na kunibusu, siku hii nilipewa lile busu nililokuwa nalihitaji akanikaribisha ndani

kufika ndani nikawakuta wazazi wake wamekaa, pamoja na wadogo zake kwakeli maisha yao ni ya kawaida saaaaaaaana wakanipokea vizuri sana nikakaribishwa soda na baadae tukala chakula kwa pamoja

tulipomaliza kula wazazi wake wakaanza kuongea na kijana wao kwamba tumemuona mpenzi wako ni msichana mzuri sana na kwa maisha uliotuhadithia bado tunashangaa amewezaje kukupenda mwenetu ambaye huna maisha mazuri na wala kazi nzuri

nikawaambia ni mapenzi tu...wakamuuliza tena unampango gani na huyu mtoto sio unamchezea tu na baadaye kumuacha

ndipo mpenzi wangu akaawaambia wazazi wake kwamba leo alinialika pale ili wazazi wake wamsaidie kumuomea kwangu kwamba anataka kunioa..

eeenheeee chinekeeeee...nilifurahi sana kusikia nataka kuolewa ila huzuni ulinijaa moyoni ya jinsi nitakavyowaambia wazazi wangu wanielewe

nikajikuta nalia pale nilitokwa na machozi mengi sana mpaka nilijishangaa nilijitahidi kuyazuia lakini hayakukatika walishangaa sana na kuanza kuniuliza kwanini nalia

nikamwambia mpenzi wangu nakupenda sana na ninakubali kuolewa na wewe lakini nilazima tuwe imara kwa yatakayokuja mbele wazazi hawatakubali na watafanya vurugu sana ukishindwa kuvumilia mpenzi hutanioa

wazazi wake waliogopa sana na kukaa kimya, mpenzi akaniambia nimeamua nataka uwe mke wangu nitavumilia yote mke wangu...sauti ya kuitwa mke wake ilizidi kunipandisha hamu yakutaka kuwa naye

basi akanikumbatia na kunibembeleza nikakaa pale mpaka jioni nikaaga na kuondoka, mpenzi wangu alinifwata nami mpaka nyumbani akahakikisha nimefika salama akanibusu na kuniambia ananipenda sana hawezi fikiria maisha yake bila mimi..tukakumbatiana akaondoka

siku zikaenda kasheshe zikaanza nilipomwambia mama nataka kuolewa..alifurahi sana na kutaka kujua zaidi kuhusu huyu kaka nikamuhadithia kila kitu kuhusu mpenzi wangu..mama alinipiga bonge la kofi nikahisi nakufa


SUBIRIA PART 3 KUJUA SEKESEKE LA MTOTO WA TAJIRI KUTAKA KUOLEWA NA MTOTO WA MASIKINI KONDAAAAAA

Reactions:

0 comments:

Post a Comment