Wednesday, December 18, 2013

Ukweli na uwazi ni jambo muhimu sana katika mapenzi......

katika maisha ya ujana wengi hupitia wanaume/wanawake tofauti kabla ya kuwa na hawa wame/wake zetu

 na wengine kabla wanakuwa wameshapata watoto inawezekana ni mmoja, wawili au watatu ndipo unakutana na mpenzi mpya

lakini je tunapokutana na hawa wapenzi wetu tunakuwaga wakweli kuhusu wapenzi waliopita?? na watoto wetu

ndoa nyingi sana zinamivurugano kwasababu ya hivi vitu na uchumba hata kuvunjika baada ya kugundua mwenzako alikuficha kuhusu maisha yake ya mwanzo

kama kweli huyo mwanaume/mwanamke anakupenda hawezi kabisa kukuacha eti kisa wewe ulikuwa malaya sana enzi zako za kurukaruka ama umezalishwa watoto wawili na baba tofauti au wewe mwanaume una watoto watatu kila mtoto na mama yake hayo ni mambo ya kuongea na kupanga maisha yenu baada ya kukutana

nitaongelea kwa mfano kama kawaida yangu

kuna dada mmoja hivi yeye enzi hizo za ujana alizalishwa watoto wawili kila mtoto na baba yake

kuna kipindi akiwa hana mpenzi akakutana na kijana mmoja mkaka mtanashati anajiweza kwakweli amejiajiri na anahela zake za kumtosha kuongeza mtu mwengine kuishi naye na kuweza kumuhudumia yaani kuoa

katika mapenzi yao yule dada anasema kweli yule kaka alimwambia kwamba anamtoto mmoja ambaye anaishi kwa wazazi wake alizaaga na dada mmoja ila hawapo wote

ujinga alioufanya huyu dada akamwambia kwamba na yeye anamtoto mmoja anaishi na mama yake

basi yule kaka siakaona huyu ndio mke aliyepewa na MUNGU kweli akawa anamuhudumia sana yule mtoto wa mpenzi wake pamoja na familia yake

ikafika kipindi huyu msichana akapata tena mimba ya huyu kaka sasa kwahiyo yeye akawa anawatoto wa tatu na jamaa watoto wawili

huyu kaka akapata uhamisho wa kwenda iringa kikazi alikuwa anafanya kazi bank akaongea na mpenzi wake pamoja na wazazi wake akatolewa mahari na kuvalishwa pete ya uchumba wakahamia Iringa ili baada ya muda fulani warudi kufunga ndoa dada akijifungua

 wakaishi vizuri sana akiwa huko shoga akawa anamdanganya tu mwanaume oohh kwa mama yangu ninavitu vyangu nimeshajipanga nimenunua hiki na kile nina hiki na kile basi mwanaume anamuona mke si ndio huyu anaakili anajua kujijenga kimaisha

jamani nyie wanawake sio mnafanya kazi mnaishia kununua nguo tu na kwenda kwenye starehe muwe mnanunua vitu vyenu mnajitegemea hata kama upo kwa wazazi unaweka tu siku vitakusaidia au kama unakiwanja basi uanjenga siutapangisha nyumba hela zitawasaidia baadae

wanaume wanapenda sana mwanamke anayejitambua kila idara sio unapanua tu miguu wewe na kumsubiri mwanaume akupe kila kitu...mfyuuuuuuuuu

basi bwana sasa shoga akajifungua akakaa huko mwezi na nusu baadae akaomba arudi nyumbani kula uzazi akakubaliwa

akarudi nyumbani MUNGU alivyomwema yule kaka akaambiwa anapewa uhamisho arudi dar..kwakweli alifurahi sana na mwanamke pia alifurahi sana

 basi jamaaa akatuma hela kwa mwanamke wake kwamba atafute nyumba dar then ahamie kabisa amchukue na mama akamlishie uzazi kwao then yeye baada ya wiki tatu atakuwa amerudi jumla pamoja na vitu vyao vilivyopo Iringa

basi akatumiwa hela kweli akatafuta nyumba na akapata sasa katika kuhamia ndio kashesehe atahamiaje na hana chochote watalala chini na mtoto wake????

na huku bwana alimdanganya anakila kitu, basi kila bwana akimpigia anamwambia ndio nimehamia yani huku tunapapenda mno mwanaume bila kujuwa anadanganywa

basi ikafika bwana kurudi akampigie nielekeze nyumbani nije shoga akamwambia njoo tu kwa mama kufika pale shoga ndio kumpasulia bwana habari

basi bwana yule akachoka kabisa na kukasirika sana kwanza kadanganywa na pili kachoka alijua atapumzika kwake sasa inabidi alale kwa wakwe ama aende hoteli..ikabidi tu alale pale baada ya kubembelezwa sana na mama mkwe

wakati yupo pale akawa anashangaa huyu mtoto wa kike anayemuita mchumba wake mama kila kitu mama akamuuliza akamjibu huyo ni mtoto wa marehemu dada yangu amenizoea kama mama yake

siku tatu zikapita siku hiyo jamaa anazunguka tu mtaani akakutana na wambea wa mtaa wakampa habari akiwa amekaa kwenye duka moja anakunywa maji na kusoma gazeti

kwamba unajuwa mkeo ana watoto wawili na huyo wako watatu??? ndio jamaa kushangaa akajibu hapana wakamwambia yule mtoto wa kike ni wake pia

jamaa ndio kuondoka kwenda nyumbani kuuliza vizuri kwa mama mkwe wake ndio kujua ukweli akazidi kukasirika kudanganywa mara ya pili...yule lala akachukuwa kila kilichochake na kuondoka hajarudi tena mwezi sasa na simu haipatikani kibadilisha number

mwanamke kabaki tu kwa mama yake na mtoto wa tatu kila mtoto ba baba yake anajutia tu maisha sasa...

 ******END******

Reactions:

1 comments:

  1. asante kwa stor yako,alexanderfedrick@gmail.com

    ReplyDelete