Tuesday, November 12, 2013

Hahahahaha haloooooo eti mwanaume asifiwi kula mwanaume anasifiwa kuingia na kutoka bank kuweka na kutoa hela bibi usipokuwa nazo eti unatupwa kwenye dustbin....

kuna wanawake jamani humu mjini mimi wananiudhi yani mwanamke anapenda pesa mbele kuliko hata ubinadamu..

jamani wanawake japokuwa mnapenda sana pesa lakini kaeni mkijua ya kwamba kuna siku mtu anapata na kunasiku mtu anakosa tena anaweza kukosa wiki nzima mfulululizo sasa wewe ndio kutumia akili yako ya ziada kumpa moyo mumeo au mchumba wako

basi bwana kuna dada mmoja hivi mtoto mdogo tu labda sasa hivi anamiaka 24 nilimjuaga kipindi cha nyuma huko..

huyu dada alikuwaga anamwanaume wake mmoja hivi huyo kaka alikuwa mzuri jamani yani kwanza ni mcha MUNGU, pili ni mzuri wa sura, tatu alikuwa anajipenda yani akivaa unaona eeehhh sasa mwanaume si ndio huyu..

huyu kaka wa watu yeye alikuwa anakazi yake ya kawaida tu kama mtu wa IT katika ofisi fulani ya wahindi huko kama mnavyojuwa wahindi nao hawalipi vizuri kiivyo yani kijana hakukosa hela ya kula, kuvaa, wala kulipa kodi ila alikuwa hana ile hela ya mashauzi na kuhonga saaana..nadhani mnanielewa

basi maisha yakaendelea kumbe yule dada alikuwa yupo na huyu kijana lakini pembeni anamwanaume mwengine yupo mgodini huko ana hela zake anamuhonga anaishi mjini kijana wa watu akawa anajua zile hela dada anatumiwa kutoka nyumbani asijue ya kwamba shoga anahongwa na kidumu

maisha yakaendelea hivyohivyo bwana unaambiwa iba tu ila siku yako ya kukamatwa ikifika utaumbuka basi siku hiyo shoga kamuaga bwana kwamba anaenda kwa ndugu yake iringa kumbe shoga kaenda geita huko kwenye migodi kwa bwana..

huwa yule bwana anamtumia hela ya kwenda na kurudi pamoja na ya kukaa hotelini kwahiyo akiwa kule yule bwana analala hotelini na shoga mpaka mdada akiondoka huyu bwana yeye hajaoa

basi bwana shoga siku hiyo kapelekwa ubungo na jamaa wakaagana vizuri dada akaondoka zake kwa hawara yake akafika mwanza kama kawaida anahoteli anayofikiga na wanamjua akakodi chumba akaingia kujipumzisha kabla bwana hajaja

basi jioni bwana kaja wenyewe wakalala vizuri asubuhi yake bwana akaaga kwamba anaenda kazini atarudi jioni na kwakuwa ilikuwa ijumaa wakapanga kwamba usiku wataenda kula sehemu halafu waende club

basi jioni ikafika jamaa kaja ameshavaa, shoga tena naye ndio kuulamba tena bonge la kimini (namwaga razi miye geita atanijua nani) sijui hii nyimbo mnaijua...basi haoooo mpaka sehemu moja ya kula nyama huwa wanachoma sana nyama na watu kunywa pombe

wakakaa pale kula, wakaja na marafiki wa jamaa wanaofanya wote kazi na wanawake zao basi wakalewaaa na kula mara wakaja wadada wawili wanaofahamiana na hao majamaa wakawa wamekaa meza ya pili wanakunywa jamaa kwakuwa anawajua akaamua kuwaita wakae meza moja wanywe pamoja

basi jamaa yeye na wenziye si wanahela basi wakawa wanazungusha tu round hata kwa wale wanawake waliokuja yani hawajanunua beer hata moja wananunuliwa tu, basi dada akawa ananihadithia nilivyoona vile da Rose nilikuwa natoa macho hawa wanawake wasije wakawa ni mahawara wa huyu bwana mbona anawafanyia hivyo

basi bwana walivyolewa vya kutosha wakaamua kwenda club sasa yule bwana akawaambia wale wanawake twendeni wote club tukamalizie siku shoga tena wale wanawake wakatae ofa haooo na wengine mpaka club

sasa bwana kufika club watu wanacheza wanafurahi shoga akaenda chooni maana tena siunajua ukinywa beer ishu yake ya kwenda chooni kila saa

basi shoga kutoka chooni anamkuta yule bwana anacheza na mwanamke mmoja katika wale waliokuja nao anamshika kiunoni na kumbusu kwenye shingo!!!!!!!

yaani ananiambia da Rose nilitaka nife nilishikwa na hasira kilichokuja akilini mwangu ni kwenda duka la jirani pale kununua wembe..simnajua haya maduka karibu na disco huwa hayafungwi mapema hata pale billicanas lipo moja

shoga kuchukua kiwembe kwenda kuanzisha ugomvi na yule dada, yule dada kutaka kumpiga na mwenziye shoga kuchukuwa kiwembe kuanza kumchanjachanja yule dada, chanjaaa ile mbaya yule bwana kuona vile akamchukua yule dada wakaondoka kurudi hotelini kukimbia soo

waliporudi sasa ndio ugomvi tena ukaanza hotelini shoga kugombana gombana na wewe akaanza kukandwa maana yule dada na mwenziye pia walimpiga sana haswa usoni akawa ameviria kama damu na kesho yake alikuwa ndio arudi dar

na asingeondoka kesho yake lazima yule dada angemfwata jamaa agombane na kutaka kuonyeshwa yule msichana yuko wapi walipize kisasi

basi kesho yake asubuhi huyoo kwenda stand kuchukua bus kurudi dar..ubungo huku yule bwana yake anamsubiri kwa hamu tena siunajuwa mtu ukisafiri ukiwa unarudi sasa hayo mahamu ya mapenzi

alivyofika dar bwana kumuona vile akaanza kumuhoji kulikoni huko umegombana na ndugu zako ama vipi? basi dada akatoa visingizio kibao ambavyo bwana bila kujuwa kuwa ni uongo akakubaliana navyo

basi wakaendelea kuishi jamani ya mwizi arubaini yule msichana sijui alipata wapi number ya shoga akampigia simu siku hiyo usiku wakiwa wamelala na bwana yake shoga si hajui number akamwambia mpenzi wake huyu sijui nani ananipigia sasa hivi na number ni ngeni siijui bwana akasema ngoja nipokee

loooooooooo anajuta mpaka leo...shoga sindio kuanza kuchamba yani hajasubiri hata kusikia hallo yani simu alivyosikia tu imepokelewa ni matusiii kumtukana demu tukana na jamaa kakaa tu kimya hakutaka kukata simu demu akamalizia natulivyokupiga bado hiyo ole wako ukanyagi huku tena utajuta..akakata simu

ndio bwana sasa kukata simu na kuanza kumuhoji vizuri shoga na mwanaume asijue unamwanaume mwengine nje utajuta...shoga ugomvi huku ukaanza tena wa haja shoga kesho yake akaambiwa apaki kilichochake aondoke

ndugu kashaharibu kotekote atafanyaje sasa na ndugu zake wako mkoani basi akaomba msamaha lakini yule bwana alikuwa na hasira sana na hakutaka kumuona tena

alikasirika kwasababu ya yeye kuwa na mtu nje na kisa ni kwamba alikuwa anahongwa hela..kwanini hukuweza kunivumilia??? basi shoga akalia na kuomba masamaha pale omba omba na wewe mwishoe kweli alisamehewa na hakufukuzwa tena

basi maisha yakaendelea kama kawaida japo sasa huyu mwanaume alianza kumchunga sana na kumchunguza kila anapoenda na anachofanya

lakini bwana hulka ni hulka tu japo alisamehewa bado alitafuta mwanamme mwengine nje mwenye hela na kumuhonga tena sasa hivi ndio akapata wa hukuhuku dar mwanaume anayejiweza mara mbili ya huyo aliyekuwanaye na alikuwa anaishi tu mwenyewe hajaoa wala hana mtoto

mwanamke akaendelea kula huku na kule bila hata kujali na alikuwa anatumia line nyengine ambayo huyu bwana haijui sasa basi mapenzi kule kwa bwana mwengine yakawa motomoto wanakula bata tu siku nyengine anaaga anasafiri kumbe haendi popote anajifungia nyumbani kwa yule bwana wiki nzima anaenjoy tu

basi mwishoe akaona sasa huyu wa zamani anamzingua tu siku hiyo akarudi nyumbani na kumueleza kwamba hamtaki tena atafute mwanamke mwengine amechoka kuishi na mtu asiyekuwa na hela za kumuhudumia ipasavyo..huyoooo akaondoka

akaachana naye na kuhamia kimoja na yule bwana mwengine, basi maisha yakasonga MUNGU akambariki yule kaka aliyeachwa akapata mwanamke mwengine na muda si mrefu akaoa

basi shoga alivyosikia jamaa kaoa akaanza kuchamba na aoe tu miye maisha ya shida siyataki na siyawezi

mapenzi tena kwa bwana mpa yakawa motomoto mpaka akaamua kumzalia na mtoto mmoja wa kike maisha tena ndio yamepamba moto kwa maraha shoga akawa anahisi kama yupo angani yani anajisikia hatari chini hakanyagiki

baada ya mtoto kufikisha mwaka yule bwana likatokea tatizo kazini akafukuzwa sasa maisha ndio yakaanza kuwa magumu hakuna mfano shoga akaanza kuona junejuly

basi alivyoona zile raha hamna tena saa zingine hawana hata kitu cha kula wanakoroga uji au mpaka jamaa akaombe chakula kwao ndio wale akasema sasa amechoka alichofanya ni kubeba mwanae na kila kilichochake na kuondoka

yule bwana akambembeleza na kumuomba arudi kwamba atatatfuta kazi lakini mwanamke hakuwa anataka kusikiliza kitu miezi ikaenda

siku bwana jamaa akapata kazi sehemu nyengine, mwezi, wa pili, wa tatu jamaa akapata na mwanamke humohumo ofisini kwao wakawa wote wanaendelea na maisha yao

 looohhh jamaa sasa anaoa JUMAPILI hii ya keshokutwa

yani yule msichana kusikia story ya jamaa kachanganyikiwa yani analia kama mtoto mdogo ananipigia simu anasema da Rose nimekosa ndoa ya pili..nikamwambia wee nitolee upumbavu wako nikamkatia na simu sitaki kabisa anililie miye nilimuonya tokea mwanzo usipofunzwa na mama yako utafunzwa na ulimwengo haya cheza sasa segere ulimwengu unaokupigia

******END*****

Reactions:

0 comments:

Post a Comment