Thursday, October 3, 2013

nyie mnaoendekeza kukaa na ndugu zenu wa kike mkiwa mmeolewa mjifunze na wanaume pia mjifunze..

basi bwana kuna mdada mmoja hivi uswahilini kwetu kwao wamezaliwa saba na baba yao ameshafariki kwahiyo wanakaa tu na mama yao..wanne wa kike na watatu wa kiume bahati mbaya wa kiume pia wote wamekufa na wakike mmoja kwahiyo sasa walio hai ni mama na watoto wake wakike watatu..

huyu dada yao mkubwa yeye katika cheza cheza zake dansi za ujana akazaa watoto wa wili na wanaume wawili tofauti

kwa bahati nzuri MUNGU akamjalia akapata kijana wa tatu ambaye makazi yake ni mtwara akampa ujauzito na kumtolea barua ili amuoe

uswahilini kwetu ukitolewa barua tu ni dili yani tutakesha kigodoro wewe tuntacheza haswa maana yani unaolewa???? kuna wengine wamezaliwa na kukuwa pale hata barua iliyokosea nyumba hamna leo wewe umepata basi tutasuguaje kisigino kwenye mchanga usiku kucha tukicheza taarab

 basi shoga tena katolewa barua huku anamimba yake changa tu...

mimba ilivyoanza kukua bwana akamwambia njoo huku mtwara tukae wote maana yeye si mzaliwa wa huko utatunzwa na mama mkwe maana hakai mbali na mimi..na kijana kidogo wanauwezo kuliko wakina shosti maana wakina shosti mama yake mjasiriamali wa biashara ndogondogo na jamaa kwao wana kampuni ya kusafirisha mbao

basi bwana shoga huyo kajipaki paaaaa mpaka mtwara mimba hapo inamiezi minne ndio alipoenda mtwara akakaa huko wee alipofika huko si akaona jamaa anazo akamshauri amlete mdogo wake anayemfwata huko ili akaenae amsaidie kufanya kazi ndogondogo na pia bwana akasema atakuwa anamsomesha hotel management

 bidada tena kwavile alimaliza form four na division 4 ya mwisho na kukaa nyumbani kwakuwa mama yao alikuwa hana uwezo wa kumsomesha akaona lohh bora hapa ndio penyewe ngoja niende zangu nikasome miyeee...ahsante shemeji shosti huyo kwenye bus mpaka mtwara

shoga mdogo mtu kafika mtwara wakaishi vizuri tu akawa anasomeshwa anaenda shule asubuhi akirudi mchana anamsaidia dada mtu shughuli nyengine hivyo hivyo hivyo hivyo mpaka dada mtu akajifungua mtoto wa kike

basi bwana simnajua tena wanawake ukijifungua hata kama unaenda kula uzazi kwa mama mkwe unatamani tu ungeenda kwa mama yako akulee??? shoga naye akatamani kulelewa na mama yake wakati wa uzazi bila kipingamizi bwana akamruhusu shoga akarudi daslam kwa mama yake akamuacha mdogo wake kule na mumewe

basi maisha ya kasonga mwezi, wa pili, wa tatu shoga tena tukasikia ameacha shule kule mtwara hataki kusoma tena anataka kurudi nyumbani dar.

yule mume ndio kumpigia mkewe kumwambia mdogo wake hataki shule dada mtu kumpa mama yake simu mama yake akaanza kulia na mdogo mtu wewe siunajua jinsi tulivyo masikini siwezi hata kukusomesha umepata mfadhili unadengua kusoma na nisikuone nyumbani kwangu yani kama hutaki kusoma usirudi huku

basi wakata simu siku zikasonga mashoga zangu

siku hiyo mdogo mtu kapiga simu mama shule tumefunga nakuja likizo nyumbani..sawa wakakubaliana akarudi vizuri jamani mtoto kapendeza, anawaka kang'aa...tukasema kweli shemeji mtu anajua kutunza

basi bwana shoga kakaa mwezi mmmhhh tukaanza kumuona shoga anatabia za ajabu mara anapenda sana vitu vya kukaanga, yani hapendi kula ugali wala wali

hivyo hivyo mara tukaanza kumuona analala sana na akiamka anatema sana mate na alikuwa hapatani na dada yake huyu mwenye mume ila anampenda sana mtoto wa dada yake huyu aliyezaliwa kutwa kumbeba

basi minong'ono ya chini kwa chini ikaanza shoga ana mimba

ndio siku hiyo mama mtu kumtolea uvivu wewe mjamzito akakubali hiyo mimba ya nani akasema ya kaka mmoja hukohuko mtwara...sio ya shemeji yako akasema sio

huku na kule wakafanya juu chini wampate yule kijana shosti anayesema ndio mwenye mimba

basi wakampata inayesemekana kuwa ni mwenye mimba

wakaongea naye kwamba unamjua fulani akasema ndio unamjuaje namjua kwasababu ni jirani yangu mabibo

eeeehhhhh kumbe unakaa mabibo si mtwara akasema huwa naendaga mtwara ila nakaa mabibo wakamuuliza kwahiyo hivi tunavyoongea upo wapi akajibu nipo mabibo looohhh kila mtu alifurahi wakamwambia siunapajua kwakina ****** akasema ndio basi tunakuomba uje mwanetu utusaidie jambo akasema sawa nitakuja mida ya saa moja

basi saa moja kijana huyooo akaenda wakamkaribisha akaingia ndani wakaanza kuongelea hilo jambo

amaa akasema kweli huyu mwanamke nimeshawahi kulala naye tena mara moja tu sasa hiyo mimba itakuwaje yangu hiyo mimba sio yangu akakataa katukatu

basi bwana kama mnavyoelewa uswahilini nyumba zimekaribiana watu tukasikia makelele hao tukaenda kusikiliza wakaanza kubishana mwanaume anakataa hiyo mimba sio yangu na wala siiudumii...huyo akaondoka

mimba tena haina baba, siku zikaenda shoga baadae akapasua jipu kwamba mimba ni ya shemeji mtu

loooohhh asalaleeee mtaani pakavurugika kwa ngumi na matusi kutoka kwa dada mtu ugomvi ukawa mkubwa sana kumpigia shemeji mtu anakataa sasa hakuna anayejua la kuamua

aliyeambiwa mwenye mimba kakataa mwanamke aliyesema mwenye mimba kiukweli mwenyewe kakataa sasa nyumbani hapakaliki kwa ugomvi kila kukicha...

baadae wakakalisha kiutu uzima wale wadada ndugu wamalize ugomvi wao wakasema tunasubiri mtoto akizaliwa tujue ukweli

lakini dada mtu siye tulimshauri asimuache jamaa japo inauma kama ni kweli ni mimba yake mtatafuta la kufanya lakini mume haachiki..


 ************END***********

kwanza hizi tabia za wewe shoga kuolewa ukambeba mdogo wako aje kukusaidia kazi hata kama unamimba zimetoka wapi???? kwani umesikia huyo ni house maid kwanini usitafute msichana wa kazi akakusaidia kazi ukamlipa..

sawa umeolewa mume anavijisenti unataka kumsaidia mdogo wako kwanini usimsaidie akiwa kwenu unataka ukae naye wewe mama yake, au mwanao huyo unataka kujua maendeleo yake kwa karibu...ni vizuri kutoa msaada lakini tolea hukohuko nyumbani kwenu

au unadhani kisa wewe umepata mume ndio kila mtu kafurahi shoga siku hizi mumeo akiwa na wewe ukimpa mgongo tu wa jirani yako anamtaka na wanaume akipewa tu tena bila vurugu na akaona kuna maua pamepambwa vizuri anakula wala haachi walivyokuwa hawana adabu wanakula mpaka mama zao wa kuwazaa sembuse mdogo wa mkewe!!!

huna aibu mwanaume mzima kwani wanawake barabarani wameisha huko hapo mnyamani kuna wanawake mpaka wa 1500 chukua toa maugando yako rudi kwa mkeo kama unataka kupiga nje

acha kumdharilisha mkeo unavyolala na mdogo mtu unamshushia mkeo thamani yake wanaanza sasa kuchukuliana kama mtu na mke mwenzie...ndio sasa uume unaolala nao kila siku na miye naujua ukiwa haupo nalala nao miye sasa hapo kutakuwa na heshima kweli???

unasababisha ndugu kwa ndugu wagombane, familia itetereke kisa dakika kadhaa za kumwaga huo mgando wako nje....mfyuuuuuuuu

na nyie wadogo na ndugu wa mwanamke mnaoenda kukaa huko na kuanza kujishebedua kwa shemeji nyie waone kwanza

utakuta mdogo wa mke amekaa sebleni na shemeji umevaa kimini mipaja yote nje, umeitanua miguu yako unajifanya hujui kinachoendelea basi tu umtege bwana wa watu

unajichekesha kama nini sijui dada akikutuma ukamwambie kitu shemeji unalegeza sauti na kujichekesha pumbavu kabisa nikikukuta miye ndio dada yako chapa bonge la kofi kaza sauti mtoto wa kike ongea kwa heshima huyo ni shemeji yako

mfyuuuuuuuu

0 comments:

Post a Comment