Friday, October 11, 2013

nilishafundisha kuhusu gubu la ndoa linalosababishwa na waolewaji sasa leo nataka tusome gubu la ndoa linalosababishwa na waowaji..

kila familia jamani inautaratibu wake wa malezi..kuna familia nyengine wanapenda ushirikina hatari,familia nyengine ni wezi hatari,familia nyengine ni wambea na wanamidomo hatari,na familia nyengine malaya hakuna mfano kwanzia babu mpaka kijukuu ambae ndio mumeo.

GUBU la kwenye ndoa maranyingi husababishwa na ndugu wa mume, ni mara chache usikie gubu la ndoa linasababishwa na ndugu wa mke.

sasa wewe unapoolewa unatakiwa ndani ya mwaka uwe umeshaisoma familia ya mumeo kwa 80% hiyo nyengine iliyobaki ni kwa wale wa vijijini ambao hata hujawahi waona zaidi tu ya kuwasikia.

na ukishawasoma na kuwajua basi anza kupanga mikakati yako na mikakati yako ipange 90% kwa mume wako hizo nyingine zilizobaki waachie wao.

wewe uliolewa na MUMEO tu hujaolewa na wengine japo hiyo isikupe sababu ya wewe kuwanyanyapaa ndugu wa mumeo

peleka mapenzi sana kwa mumeo na umuache huru kuwa na ndugu zake, azima kwenye ndoa utambue mida..kuna muda wa wewe kuwa na mumeo na kuna muda mumeo kuwa na ndugu zake

na kwakuwa umeshajua nani anachokochoko katika wakwe zako wewe unapokuwa na mumeo muue ndugu yake kwa mumeo lakini kwa silaha ya upendo na uchungu kwa muda mmoja..utafanyaje

labda mama mkwe wako ndio hakupendi hakupendi kufuru..utalipeleka vipi hili kwa mumeo

mume wangu nina vitenge hapa nilikuwa naomba umpitishie mama nyumbani, siunajuwa tena mimi na mama hatujakaa sawa kimapendo ukifika mwambie nimempa zawadi namshukuru kwa kunizalia mume wangu na amekulea vizuri sana ninafurahia mapendo na mapenzi unayonipa mume wangu..

umemchapaje mama mkwe wako: kwanza umempa matenge, pili umemsifia mama mkwe wako kwa mumeo, na tatu umemsifia mama mkwe kwa malezi aliyomlea mumeo...hebu niambie hapo mumeo na mama mkwe wako watakuwa wamejisikiaje???????

ukifanya hivyo kila baada ya miezi mitatu huyo mama bado atakuwa na gubu na wewe??? tena siku hiyo ukiwa unaenda kumsalimia unafungasha hatari hata kama akikuona anatema mate wewe usiwe na habari habari yako moyoni ni mumeo tu

jamani si ukipenda boga lazima upende na jani lake hata kama linamiba linakuchoma shoga utalishika kwa umakini...

twende kwa mawifi sasa....

mawifi bwana wao huwa ni moja shoga huyo ni kaka yangu miye na yeye damu moja nikimwambia hiki lazima atanisikiliza..wewe wa kuja utanibabaisha nini

chokochoko za mawifi ni hatari zaidi kuliko chokochoko zozote zile kwasababu wale si mmelingana na kama kakupita sana sio miaka zaidi ya mitani kwahiyo bado mpo sawa kimwili na kimaisha

mawifi bwana wao kwanza ni kuangalia yale unayoyafanya mema wewe na kuitumia kwao kama silaha ya kukuangamiza

mfano shoga tena umeolewa tu mumeo kanunua gari ya kisasa halafu akakufundisha wewe kuendesha utasikia mfyuuuuuu unaringa kwa jasho la kaka yetu eti na yeye anaendesha haloooo asingeolewa angeendesha nini labda tumbo...

na ukiolewa ikipita mwaka hujabeba mimba utajuta...nyooo amekaa tu kwa kaka yetu anamaliza sembe na kujaza choo hatuoni akitema mate wala akilamba ndimu mfyuuuuu...hahaha mawifi hao

sasa hao fimbo yao unawachapaje..

kama nilivyowaambia wewe ni kwa mumeo tu..mume wangu nawapenda sana hawa dada zako lakini naona kama nahitaji kukaa nao mbali ili nizidi kukutunzia heshima yako wanamaneno mengi sana wanasema juu yangu tena hakuna hata lililojema na mimi ni binadamu mpenzi nisijinikakwazika nikajikuta nimewajibu vibaya ndugu zako maana nikiwaona wale ni kama nakuona wewe nyie ni damu mmoja nikiwatukana na kuwachukia wale ni kama nimekutukana na kukuchukia wewe mume wangu na mimi sipendi..basi naomba nikae nao tu mbali ukiwa unawahitaji naomba tu uwafwate kwao mpenzi

na kama wakija hapa basi watambue hapa ni kwako na mimi waje kwa heshima hata kama hawanipendi chuki wafanyie huko nje..

sasa siku wajiloge waje nyumbani kwako ujishebedue mtoto wa kike kila kitu mume wangu hiki, mume wangu kile, mume wangu huku basi mpaka wa kereke wapate la kuongea tena wala usiwanunue, usiwatukane tena wakija kama na zawadi ya kuwapa unayo wape hata kanga doti mojamoja zile za urafiki

ukishafanya hivyo vyote na bado wanakuchokonoa siku wakija nyumbani kwako mumeo hayupo watie adabu, wape lako la moyoni chambaaaaa hatari ila sio kwa jazba kitaratibu tu..na uwaambie unaweza ukawapiga marufuku kuja hapo na kaka yao asifanye lolote

wenyewe watakaa sawa...wataona kumbe hiki nacho kiberiti kikitingishwa sana kinaweza lipuka...mfyuuuuuuuuu mawifi wote manopenda kuchokonoa ndoa za kaka zenu popote mlipo

ninamshukuru sana MUNGU kwakunipa maarifa ya kuishi katika ndoa sio kwamba chokochoko za mawifi na mashemeji sina ila naishi kama panya unang'ata na kupuliza...pakuwachamba nachamba pakuwapa raha nawapa raha..

kazi zangu za kupika nafanya na wifi zangu na wake wa shemeji zangu, kazi zangu za ukumbini mziki nafanya na shemeji yangu yani ndio majembe yangu naamini mnaokujaga kwenye mafundo mnawaonaga pale ukumbini..na kama bado basi mwezi wa kumi na mbili nikifunda tena mtawaona MUNGU akipenda na nitawaruhusu kuwauliza maswali wanavyoishi na miye

na sio kwamba nakaa nao mbali ndio maana tunapatana hapana na kaa nao nyumba moja...yani wote wamejenga kwenye kiwanja kimoja wote waliotoka tumbo moja na mume wangu na wapo sita kwahiyo tunaonana kila dakika, na kila siku tupo wote..

TUJIFUNZE..

Reactions:

0 comments:

Post a Comment