Wednesday, October 23, 2013

kila leo tunasikia mume wa mtu sumu na wengine wanasema kama ni sumu basi hawara ni maziwa atailainisha sumu hahahaha jamani kuna sumu nyengine hata unywe maziwa lazima utakufa tu...

basi bwana hizi nyumba za kupanga zinamatatizo,haswa mkiwa mnatumia choo kimoja cha nje..

kuna nyumba moja wamepanga wapangaji wengi tu mmoja wao ni mkaka mmoja na mkewe hawana mtoto na mpangaji mwengine ni mdada tu yupo na msichana wake wa kazi pamoja na wapangaji wengine waliopanga kwenye nyumba hiyo

kumbe bwana yule baba aliyepanga na mkewe akawa anamtaka msichana wa kazi wa huyu dada mwengine sasa

kila mkewe akiwa hayupo na dada wa yule msichana wa kazi akiwa kazini yule baba anatafuta njia yoyote arudi nyumbani ili tu akamtongoze na kuwa karibu na yule dada

yule dada anasema yeye hakumtaka yule baba na wala hajawahi kukutana naye kimapenzi

ikafika kipindi mpaka yule dada akienda kuoga bafuni yule baba anamtegea mkewe hamuoni anaingia bafuni na yule dada

yule dada anasema alikuwa hapendi na alikuwa anamfukuza yule baba na kumtishia kumwambia mkewe kwahiyo yule baba akisikia hivyo anatoka lakini haachi kurudia siku nyengine..mpaka yule dada alipochoka

basi bwana siku hiyo msichana akaamua amtolee baba uvivu kwa mkewe,akaenda kumuhadithia kila kitu mkewe yule mkewe akamsikiliza akamwambia sawa nitalifanyia kazi

mmmhhhh yani na sisi wanawake saa zingine tukiambiwa vitu kuhusu wame zetu huwa tunakurupuka tu bila hata kuchunguza au kumuuliza mwenyewe mnajua yule mama alifanyaje????

kesho yake kaenda kuchukuwa mashoga zake wa nne pamoja na yeye wakawa watano akamuita shosti chumbani kwake shoga sikajua labda anataka kutumwa

shogaaaaa yule dada kuingia ndani akawekwa mtu kati sutwaaaaaaaaaa, chambwaaaaaa mpaka kupigwa

yule mama akawa anamshtumu unajitongozesha kwa mume wangu umeona hakutaki ndio umeamua kuja mumsemea kwamba yeye ndio anakutaka

nakwambia leo nitakukomesha na hizo nyege zako mshindo,basi yule mama na mashoga zake kuchukuwa chupa ya soda na kutaka kumuingiza shoga kwenye k**********

uzuri shoga naye alikuwa anajimudu kidogo kwa nguvu huku na kule vuta nikuvute mara shoga MUNGU mkubwa akapata upenyo wa kuwasambaratisha wale wadada uzuri mlango haukufungwa na funguo ndio kukimbia

akaingia ndani kwao akajifungia mlango,akiwa ndani shetani akamuingia akachukuwa fragile 25 akameza kwa wakati mmoja

basi jioni saa kumi na moja ndio dada yake kurudi gonga gonga na wewe wapi,tafuta tafuta na wewe akajaribu kumpigia simu ikaita kwa ndani ndio kuzunguka nyuma kuchungulia dirishani kumkuta dada wa watu chini anatoa mapovu mdomoni

basi yule dada ndio kutafuta watu kuvunja ule mlango na kumkimbiza palestina pale sinza, huku na kule madaktari kukimbizana kumuokoa maisha akafanikiwa kutolewa ile sumu na kuanza kuhadithia huo mkasa

yule dada yake kurudi nyumbani kuwatafuta wale akakuta yule mwanamke kashakimbia siku nyingi hayupo mpaka jioni hajarudi na hajarudi tena kwenye ile nyumba.Reactions:

0 comments:

Post a Comment