Tuesday, October 29, 2013

Jamani nyie mnaoolewa hamjamaliza starehe zenu nyie mnaenda kuwatesa watoto wa wanawake wenzenu halafu na nyie mnazaa ngoja ya warudie kwa watoto wenu sikia hii....

basi bwana kuna mdada ameolewa ana watoto wa nne wawili wa ujana wake na wawili amezaa na mumewe ambao ni mapacha

wakawa wanakaa kinondoni na sasa wameamia uswahilini kwetu mabibo wanakama mwaka hivi lakini jamani hakuna kicheko ambacho hatujacheka

kwanza huyu dada mumewe ni wa picha tu kwamba aonekane na yeye kaolewa lakini nje anamabwana kibao na sio kwamba mumewe labda anamfanyia mabaya ambayo yamempelekea yeye kutoka nje hapana yeye ndiye anayetoka nje na kumfanya mumewe aishi kwa mawazo


kwanza mwanamke hapiki wala kufanya usafi kwake kila kitu kinafanywa na msichana wa kazi huyu mwanamke kazi hana anaondoka kila siku asubuhi na kurudi jioni na ndani unyumba mumewe hampi msiniulize nimejuaje ila ndio mambo ya uswazi

huyu mwanamke anakuwa karibu na mumewe pindi anajuwa mshahara umetoka basi utamuona anashinda nyumbani nakuwa mke motomoto lakini sio kwamba ndio watumie wote hela hapana

anachukuwa hela kwa mumewe wenyewe wanasehemu wanapowekaga hela anachukua halafu anaenda kumuhonga hawara yake wanakula starehe na kulala hukohuko anarudi kwake asubuhi

majuzi kabla ya Idd alicchukuwa 150000 kaondoka nyumbani hajarudi mpaka leo ninavyowaandikia hapa hajui watoto wake wanakula nini, shule wanaenda ama hata kama wanaoga

cha kushangaza yeye na hawara yake wanatumia kila kitu yani anabaki hana hata ya kurudi nyumbani anaanza sasa kupigia wapangaji wenzake wamtumie japo 1000 kwenye tigo pesa ili aweze kurudi nyumbani

wakati mwengine nasikia hata vocha ya simu anakuwa hana anakubeep halafu anaomba umtumie hata ya 500 tu aweze kumpigia hata mumewe amuombe hela yani jamani watu huwa wanakasirika

kabla ya sikukuu ya Idd alifanya vurumbati mtaani balaa yeye na mashoga zake wakamleta mpaka gea kwenye huo msuto

mumewe najua kwa mawazo ya mkewe akaamua kugeukia pombe maana mumewe kwao sio walevi ni swala tano dada yenu sasa nishachunguza mpaka familia ya mume ila ni huyu tu ndio anakunywa pombe halafu kwao wanaume ni wapole jamani hawaongei wao ni vichwa chini tu wote waliozaliwa kwenye tumbo la mama yao

sasa alivyokuwa bar kila akienda kulewa akawa anakaa na huyu bar maid mmoja wanapiga sana story wakazoeana akawa anaenda mara kwa mara pale nadhani maumivu yakizidi anayatoa pale kwa shoga na yeye shoga anajua kumtoa bwana maumivu si baadae wakaanza kuwa wapenzi

na hapa ndio sisi wake tunapojisahau unapommpa mawazo mumeo anatafuta sehemu ya kwenda kutoa mawazo yake kwa uzuri ama ubaya kwa uzuri ndio kama hivi kwa ubaya anaweza kukupiga ama kutafuta tu ugomvi nje na kupigana na hawa wanawake nje wanaoletewa matatizo yetu wake weeee wanajua kujishebedua na wame zetu hatari yeye pale ndio anatoa maufundi yote na kwa akili za mwanaume anapata pumziko kweli na kwenda tena na tena na tena

sijui wewe ila mimi nimeshakuwa na wame za watu na ninajuwa jinsi gani nilivyokuwa najituma akija kwangu hata nikimwambia amtukane mkewe anaweza mtukana ndio hivyo mahawara wanavyofanya huko nje tunapojisahau ndani ya ndoa zetu

basi mapenzi yakawa motomoto kati ya mumewe na yule bar maid loooohhh shoga kuona sasa nyumbani bwana mawazo hakuna tena wala akiondoka haulizwi umeenda wapi wala unarudi lini si ndio kuuanza kujiuliza na kufanya uchunguzi

akajuwa kwamba mumewe anamahusiano na huyo msichana siku hiyo sasa kachukuwa mashoga zake wa kinondoni wakakodi bajaji mbili hao mpaka mabibo mishangingi ya mtaa ikafunga ile bar pale kunywa saana beer huku wakiomba waekewe taarabu shoga wakamtafuta mwanamke akaketishwa chini katikati ya hao mashosti

hahahahaha kigoma noma haswa ukiwa unasutwa,shoga akasutwa kasutwa kasutwa kasutwa akaambiwa ukirudia tena tunakuchapa basi na goma likaishia hapo,la yule mwanamke hajaacha bado maruerue yake anayomfanyia mumewe

*******END*******

KAZI KWENU SASA MNAOTAKA KUOA NA KUOLEWA MCHUNGUZE KWANZA MWANAMKE AU MWANAUME UJUWE KABISA YUPO TAYARI HATAKI TU KUOLEWA ILI AVAE GAUNI JEUPE NA YEYE TUMUONE BALI ANAWEZA KUMUDU YOTE YATAKAYOJIRI BAADA YA KUVUA GAUNI JEUPE...


Reactions:

0 comments:

Post a Comment