Tuesday, September 17, 2013

KWA NINI ASILIMIA KUBWA YA WANAUME WANATOKA NJE YA NDOA ZAO?

Mwanaume anapotoka nje ya ndoa, hatoki kwa sababau anataka sana kutoka, hutoka zaidi kwa sababu kuna msukumo wa kutoka. Hatoki nje kwa sababu anampenda huyo anayetoka naye nje, hapana. Anatoka nje kwa sbabau anasukumwa na asichokijua.
Kwa nini mwanaume anatoka nje na anafumaniwa, anaomba radhi, anasamehewa na halafu anatoka tena nje. Mke akitaka kuondoka, anatumia kila gharama kumzuia. Kama hampendi anamzuia wa kazi gani? Kama ingekuwa kutoka nje ni sawa na kupenda kwa mwanaume, si angeachana na mkewe na kubaki na huyo hawara?
Ni kweli kwamba, baadhi ya wanaume hutoka nje kwa sababau wamewachoka wake zao, lakini wengi hutoka nje kwa kusukumwa na mauambile tu. Mwanaume huvutwa na mwili tu wa mwanamke, siyo kitu kingine. Kwa namna anavyovaa tu, mwanamke huweza kumvuta mwanaume kwa kiwango cha juu sana. Nikisema kumvuta nina maana ya kumtamanisha.
Wataalamu wengi wanasema nguo zenye kuchokoza kama vile zile za kubana au nusu uchi kwa ujumla, huamsha hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume kwa kiwango kikubwa zaidi, kuliko mwili wa kike ulio uchi.
Kwa hiyo wanawake wana changamoto kuhakikisha kwamba, wakati mwingine wasione aibu kuwalinda waume au wapenzi wao, kwani linapokuja suala la kutamani na kutenda, wanaume zao ni sawa na Beberu la mbuzi. Hadi wamalize au kukamilisha kiu yao, ndipo akili zao za kibinadamu zinaporejea.

Imeandikwa na E. Kimambo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment